Ndiyo, wanaume huongopa zaidi ya wanawake, hayo ni matokeo ya utafiti mkubwa uliofanyika kuhusu udanganyifu.
Taarifa za tafiti 565 zikihusisha watu 44,000 zilichakatwa na taasisi ya Max Planck na Technion za Ujerumani na Israel.
Lakini,wanawake si wakweli kihivyo. 42% ya wanaume waligundulika ni waongo,ikilinganishwa na 38% ya wanawake.
Utafiti huo pia umebaini kuwa vijana ni waongo zaidi ya wazee.
kila mwaka kiwango cha ukweli hupanda kwa 0.28%.
Habari ndio hio.