Friday, 25 January 2019

K SHARKS BALAA...WAICHAPA MBAO FC


Wawakilishi pekee wa timu kutoka Tanzania ambao wamebaki hatua ya nusu fainali kwa sasa ni Mbao wamecheza na K Sharks hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa Cup.
Dakika 90 zinakamilika kwa timu zote mbili kumaliza bila kufungana hali inayopelekea kumtafuta mshindi kwa mikwaju mitano mitano ya penalti.

Mbao FC  5 -   K Sharks 6 


Share:

MANARA AWACHANA SIMBA KUTOLEWA SPORTPESA


Mchezo kati ya Simba na Bandari FC

Baada ya Simba kutolewa na Bandari FC katika nusu fainali ya michuano ya SportPesa jioni ya leo, Afisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara ameonesha waziwazi kusikitishwa na matokeo hayo.

Simba imeambulia kichapo cha mabao 2-1 katika uwanja wa taifa baada ya kutangulia bao moja katika kipindi cha kwanza lililofungwa na Meddie Kagere katika dakika ya 45, huku mabao yote ya Bandari FC yakifungwa katika kipindi cha pili kupitia kwa William Wadri dakika ya 59 na Wilberforce Lugogo katika dakika ya 72.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Afisa Habari huyo, ameandika akionesha kusikitishwa na matokeo hayo huku akiwatakia pole mashabiki wa klabu hiyo.

"Togwa limeingia nzi!!. Ukisikia kuharibiana siku ndio huku Okey poleni Wanasimba wote #SportPesaCup2019", ameandika Manara.

Kwa matokeo hayo sasa Simba inasubiri kucheza mchezo wa mshindi wa tatu na timu itakayofungwa mchezo mwingine dhidi ya Mbao FC na Kariobang Sharks.
Share:

ASKOFU AMFAGILIA JPM KUKUTANA NA VIONGOZI WA DINI

NA DANSON KAIJAGE, DODOMA ASKOFU wa Jimbo la Dodoma na Nyanda za Juu Kusini,Kanisa la Mlima wa Moto,Jijini Dodoma,Slvanus Komba,ampongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kukutana na viongozi wa dini. Akizungumza na waandishi wa habari kanisani hapo jana,alisema kitendo cha Rais kukutana viongozi wa dini kutasaidia kujua kero mbalimbali za wananchi na kulifanya taifa kufanikiwa kwa kiwango kikubwa. “Nampongeza Sana Rais Dk.John Magufuli kwa kufanya mkutano na viongozi wa dini amefanya kitendo Cha ajabu Sana,tunasikia nchi jirani Rais anafuta makanisa yeye anawaita nakuzungumza nao.” Alisema mikutano Kama hiyo itamfanya Rais…

Source

Share:

WATENDAJI WA VIJIJI NA KATA WANAOTOROSHA MAPATO NJOMBE WAWEKEWA MTEGO

Na Amiri kilagalila Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Njombe limewatuhumu baadhi ya watendaji wa vijiji na kata kushirikiana na wafanyabiashara kutorosha mapato kwa kusafirisha mizigo nyakati za usiku kwa kutumia njia zisizo na mageti hali ambayo imesababisha hasara kubwa halmashauri hiyo na kushindwa kufikia lengo katika ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha nusu mwaka. Mwongozo wa serikali kila halmashauri inapaswa kukusanya asilimia 80 ya mapato kiwango ambacho kimeshindwa kufikiwa na halmashauri ya wilaya ya Njombe ambayo imekusanya asilimia 47 pekee ambayo ni sawa na bil 10 kati…

Source

Share:

DC MSAFIRI AAGIZA WATUMISHI KUACHA KUTUMA BARUA PEKEE KATIKA OFISI ZA KARIBU NA KUKAA WAKISUBIRI MAJIBU

Na Amiri kilagalila Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri amewaagiza watumishi na wakuu wa idara kuacha uvivu wa kuagiza barua zinazohitaji utekelezaji wa haraka katika ofisi zilizopo karibu na maeneo yao badala yake waweze kwenda nazo mikononi ili kupata majibu ya utekelezaji kwa wakati. Mkuu huyo wa wilaya ametoa maagizo hayo wakati wa kikao cha baraza la madiwani lililofanyika mapema hii leo katika ukumbi wa wilaya hiyo na kutolea mfano wa kuagiza barua katika ofisi za Tanesco zilizopo mita chache kutoka katika wilaya hiyo huku zikipitia mlolongo mrefu na…

Source

Share:

BANDARI WAIGONGESHA SIMBA 2-1


Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere ameiandikia bao la kuongoza katika dakika za nyongeza kipindi cha kwanza na kuifanya Simba kwenda mapumziko kifua mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Bandari katika mchezo wa nusu fainali SportPesa Cup Uwanja wa Taifa.

Kagere amefunga bao hilo baada ya Simba kufanya mashambulizi bila mafanikio na ndipo kabla ya mwamuzi kupuliza kipyenga cha mapumziko akawanyanyua mashabiki wa Simba kwa kufunga bao la kwanza akimalizia pasi ya Clatous Chama.

Mnamibia ambaye ni mshambuliaji mpya wa Simba ameshafanya makeke yake kwani amesababisha faulo moja karibu na 18 baada ya kufanyiwa madhambi alipokuwa anataka kushambulia lango la wapinzani.

Kipindi cha pili Bandari wamepata bao dakika ya 59 na William Waydi kwa penalti baada ya Mzamiru Yassin kfanya madhambi eneo la hatari na anatolewa nje baada ya kuumia nafasi yake inachukuliwa na Jonas Mkude.

Dakika ya 75 Bandari wakaiandikia bao la pili na kuifanya Simba kuwa nyuma kwa bao 1.

Kuwa Mjanja..Download App mpya ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari za michezo moja kwa moja Kwenye Simu yako

Share:

MWANAMKE ANG'ATWA NA NYOKA KWENYE MAKALIO AKIJISAIDIA

Chatu wa urefu wa futi tano akitolewa chooni

Mwanamke mmoja nchini Australia "ameruka kutoka kwa kiti cha choo" baada ya kung'atwa na nyoka aina ya chatu.

''Nilihisi kama nimedungwa kisu kwenye mkalio ilikuwa uchungu sana, ghafla nilijipata nimeruka juu na kukimbilia nje nikiwa nusu uchi'' Richards aliviambia vyombo vya habari.

Bi Richards, 59, aling'atwa nyoka huyo katika nyumba ya jamaa zake mjini Brisbane mapema wiki hii.

Mtaalamu wa kushughulikia nyoka Jasmine Zeleny, aliyemtoa nyoka huyo kutoka chooni hapo amesema ni kawaida kwa nyoka kutafuta maji chooni hasa wakati wa msimu wa joto kali.

Zeleny amesema kuwa Bi Richards ametibiwa na kupewa dawa ya maumivu,akielezea kuwa aina hiyo ya chatu haina simu.Nyoka huyo huenda alikuwa anatafuta maji asema mtaalamu wa nyoka, Jasmine Zeleny

"Njia ya nyoka huyo kutoka chooni ilizibwa wakati Helen alipokuwa akijisaidia, ndipo akamng'ata akihofia kudhuriwa," Bi Zeleny aliiambia BBC.

Chatu aina ya 'Carpet python' hupatikana sana katika pwani ya mashariki mwa Australia.

Huwa hana sumu lakini anapomng'ata mtu inapendekezwa adungwe sindano ya pepo punda.

Wiki za hivi karibuni Australia imekuwa ikishuhudia joto kali ambalo limevuja rekodi.

Wanyama wengi wa porini wameripotiwa kufa ikiwemo popo na samaki.

Chanzo- BBC
Share:

MATOKEO YA MTIHANI SHULE YA 'MASELA' GUMZO...WAMEACHA MSELA WAO MMOJA


 
Baada ya Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) kutangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, kuna mambo mengi ya kushangaza na kufurahisha kuhusu matokeo hayo yaliyoibua mjadala mitandaoni.

Mathalan, shule ya sekondari Tumaini iliyopo Morogoro kutumia polisi kufanya udanganyifu.

Wahusika katika shule hiyo walivunja ukuta wa chumba cha kufanyia mtihani na kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha pili ambao siku ya mtihani walikuwa wakipewa mitihani na kuwapeleka walimu.

Sasa achana na hiyo ya sekondari ya Tumaini, kuna hii ya Shule ya Sekondari Masela.

Baada ya matokeo hayo kutangazwa wapo waliofananisha maana ya neno ‘masela’ wanavyolitumia mtaani, na matokeo ya shule hiyo.

Msela ni mtu ambaye haoni matatizo, yaani hufanya anachotaka na hajali watu watafikiri nini.

Kwa matokeo ya shule hiyo wapo waliofananisha na maana ya neno msela ingawa kiuhalisia jina la shule hiyo halina maana ambayo watu wanadhani.

Shule hiyo ina watahiniwa 15, kati yao ni mmoja tu ndio amepata daraja sifuri.

Watahiniwa wawili walipata daraja la pili, waliopata daraja la tatu wawili na waliopata daraja la nne wanane.

“Masela wamemuacha msela wao mmoja tu, yaani wao wamefaulu ila msela wao mmoja kabaki (akimaanisha aliyepata daraja sifuri),” amesema mmoja wa wafuatiliaji wa matokeo hayo mtandaoni.

Share:

Video Mpya: PROFESSOR JAY FT. VICTORIA KIMANI - WOMAN

Professor Jay Ft. Victoria Kimani - Woman


Share:

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUCHAPISHA UONGO KUHUSU RAIS MAGUFULI

Mfanyabiashara Henry Munisi mkazi wa jiji la Mbeya mwenye umri wa miaka 30 amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa shtaka la kuchapisha taarifa za uongo zinazomhusisha Rais Dkt, John Magufuli na upotevu wa Sh 1.5 Trilioni.

Munisi anashtakiwa kwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook taarifa za uongo zinazomhusu Rais Magufuli akizihusisha na ununuzi wa ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL).


Wakili wa Serikali mwandamizi, Patrick Mwita akitoa madai yake mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi, Salum Ally amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 28, 2018 akiwa Jijini Mbeya.


Mshtakiwa huyo anadaiwa kuchapisha katika ukurasa wake wa Facebook taarifa inayosomeka “Jinsi Magufuli alivyochota Tril, 1.5 za ATCL akitumia ujanja wake wa kuleta ndege ili atuibie.”


Wakili Mwita ameiambia Mahakama kuwa mshtakiwa alifanya hivyo huku akijua taarifa hizo ni za uongo na zina lengo la kupotosha umma.


Baada ya kusomewa mashtaka alikana kuhusika na tukio hilo, ambapo wakili wa serikali, Mwita alidai kuwa upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa kwa shauri hilo.


Hakimu Ally aliagiza mshatakiwa awe na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho watakaosaini bondi ya sh. 500,000, ambapo alifanikiwa kutimiza na kuachiwa kwa dhamana.


Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 6, mwaka huu.
Share:

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU TIDO MHANDO

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa TBC, Tido Mhando, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake. 

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha mashtaka yake.

Tido alifikishwa Kisutu kwa mara ya kwanza Januari 26, 2018, kujibu mashtaka matano.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 7/2018, Tido alikabiliwa na mashtaka matano, mashtaka manne ni ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.
Share:

NAIBU WAZIRI WA MAJI AMKALIA KOONI MKANDARASI WA MAJI

Naibu waziri wa maji mheshimiwa Jumaa Aweso (MB) amesikitishwa na kitendo cha mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji Chalinze kampuni ya Overseas Infrastructure Alliance (INDIA) Private Limited kusuasua katika kutekeleza mradi huo pamoja na kwamba serikali imekwishatoa fedha za mradi huo kitendo kinachosababisha wananchi wa Chalinze kuendelea kukosa maji kwa mda sasa. Akiwa katika ziara ya ukaguzi wa mradi wa maji Chalinze siku ya jana kufuatia malalamiko ya uchelewaji wa mradi Naibu Waziri huyo aligundua mapungufu kadhaa ikiwemo mkandarasi mkuu huyo kutowajibika ipasavyo kitendo ambacho kinapelekea wakandarasi wasaidizi kushindwa…

Source

Share:

MADIWANI WILAYA YA NJOMBE WAUNGANA NA WANANCHI KUPAMBANA NA MAUAJI YA WATOTO

Na Amiri kilagalila Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoani humo wamesikitishwa na vitendo viovu vya utekaji na mauaji ya watoto wadogo yanayoendelea wilayani humo na kuahidi kuunganisha nguvu zao kwa kushirikiana na wananchi ili kupambana na Mauaji hayo. Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe na diwani wa kata ya Ikuna Valentino Hongoli akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, amesema kuwa kuna umuhimu wa kuunganisha nguvu zao kwa kuwa vitendo hivyo vinazidi kutishia usalama huku vikiludisha nyuma maendeleo ya wananchi wao. “Niombe…

Source

Share:

HUYU NDIYO KINARA WA MTIHANI KIDATO CHA NNE 2018 ..AFUNGUKA KILA KITU SIRI YA USHINDI...TAZAMA MATOKEO HAPA

Mwanafunzi Hope Mwaibanje (18), aliyeibuka kinara katika Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) uliofanyika mwaka jana, ameeleza siri ya ufaulu wake.

Matokeo ya mtihani huo yalitangazwa jana jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk. Charles Msonde, huku Mwaibanje akitangazwa kuwabwaga watahiniwa wenzake 322,964. 

Akizungumza na Nipashe jana akiwa jijini Mbeya muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Mwaibanje alieleza jinsi ilivyokuwa ngumu kwake kuwa miongoni mwa wanafunzi 10 walioongoza kitaifa.

Alisema mara kwa mara walimu wao walikuwa wakiwaeleza kuwa, wakiweka juhudi katika masomo, watafanya vizuri kitaifa, ikizingatiwa shule yao (Ilboru) inasifika kwa kufanya vizuri na kutoa wanafunzi bora kitaifa mara kwa mara.

“Maneno haya ya walimu ndiyo yaliyonifikisha hapa nilipo, ingawa matarajio yangu hayakuwa haya, nilikuwa napambana niwe miongoni mwa wanafunzi 10 bora kitaifa, lakini Mungu ameamua kuniinua zaidi, namshukuru sana,” alisema.

Mwanafunzi huyo alisema ndoto yake ni kuwa daktari wa magonjwa ya moyo, anayoona ni changamoto kubwa nchini kwa sasa.

"Niseme ukweli, sikutegemea kama ningeongoza kitaifa, nilichokuwa napambana kusoma sana ni kuhakikisha kwenye wanafunzi 10 bora kitaifa sikosi, namshukuru Mungu, yeye ameamua kuniinua zaidi na kunifanya niongoze kitaifa,” alisema.

“Ratiba ya kuingia darasani ilikuwa inaanzia saa moja asubuhi hadi saa nane mchana, baada ya kutoka darasani kuanzia saa tisa alasiri hadi saa 12 jioni, nilikuwa najisomea mwenyewe. Baada ya hapo dini, tukimaliza kuanzia saa mbili usiku hadi saa sita nilikuwa najisomea.

“Niseme ukweli kutoka moyoni, walimu wetu pia walikuwa karibu na wanafunzi, walikuwa wanatufuatilia hatua kwa hatua za ufaulu wetu. Pia ninamshukuru Mungu kwa kuwa hakuniacha kila hatua.

“Endapo mwanafunzi akiamua kuachana na mambo mengine na kufikiria yale tu ambayo yamewapeleka masomoni, kwanini basi mwanafunzi wa namna hii asifikie lengo lake la kupata ufaulu wa juu, ila wasimwache Mungu."

Kinara huyo wa ufaulu alibainisha kuwa, kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, akiwa Shule ya Msingi Lioto, Mbeya Mjini, alikuwa miongoni mwa wanafunzi watatu bora, lakini alikutana na wakali zaidi alipojiunga na Ilboru na changamoto kubwa kwake ilikuwa lugha ya Kiingereza.

“Si unajua, unapotoka shule za msingi za serikali, lugha ya Kiingereza huwa changamoto, lakini hili halikunifanya nirudi nyuma, mwaka wa kwanza ulikuwa na changamoto na ufaulu wangu haukuwa mzuri, lakini kuanzia kidato cha pili nilifanya vizuri," alisema.

Mwaibanje alisema alipata taarifa ya kufanya vizuri kwenye mtihani huo jana asubuhi baada ya rafiki yake, Allen Diadoni kumpigia simu kumjulisha kuwa ameongoza kitaifa.

“Wakati huo nilikuwa nyumbani, sikuamini kwa sababu hayakuwa matarajio yangu, nikajua ananidanganya, lakini simu ziliendelea kupigwa za kupongezwa na baada ya muda nilihakikisha mwenyewe baada ya kuona matokeo yangu namshukuru Mungu," alisema.

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2018 NA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2018 YAMETANGAZWA.YAANGALIE HAPA CHINI KWA KUBONYEZA LINK





Share:

SERIKALI KUTOA BILIONI 5 KUKAMILISHA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFANI SHINYANGA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inatarajia kutoa zaidi ya Shilingi bilioni tano kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Shinyanga, ili ianze kufanya kazi ya kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi, na kuwaepushia gharama kubwa za kwenda kutibiwa kwenye hospitali ya Bugando, jijini Mwanza. 

Hospitali hiyo ilianza kujengwa rasmi mwaka 2014, ikiwa imeshakamilika jengo la utawala pekee kwa gharama ya Sh. bilioni 1.6.

Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu, alisema hayo wakati alipofanya ziara ya siku moja mjini hapa kukagua ujenzi huo, Kituo cha Afya Kambarage na huduma za matibabu katika hospitali ya mkoa huo.

Alisema ukamilishwaji wa ujenzi wa hospitali hiyo ni muhimu, hivyo serikali itatoa Shilingi bilioni tano, ili kukamilisha majengo muhimu ya kutolea tiba, na ifikapo Julai Mosi, mwaka huu ianze kufanya kazi ya kutoa matibabu kwa wananchi.




"Mpaka sasa tumeshatenga Sh. bilioni 2.5 ambazo zitajenga majengo mawili ya mama na mtoto na Sh. bilioni 3.7 bado tunasubiri fedha zake ambazo zitajenga jengo la uchunguzi lenye vyumba vitatu vya upasuaji," alisema Ummy.

"Nataka niifanye hospitali hii ya rufani ya Mkoa wa Shinyanga kuwa ya kisasa kabisa, na wananchi kutokwenda kutibiwa Bugando tena, nitaweka vifaa tiba vya kisasa ikiwamo CT-Scan, pamoja na kuajiri madaktari bingwa wanane wa magonjwa mbalimbali ikiwamo ya wanawake na watoto ili kumaliza vifo vya uzazi," alisema.

Katika hatua nyingine aliwataka wananchi wa mkoa huo kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii CHF iliyoboreshwa, ili kuwapunguzia gharama kubwa za matibabu na hasa pale wanapougua ghafla na kujikuta hawana pesa, hali ambayo itasaidia kupata tiba bure na kuokoa maisha yao.




Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Rashid Mfaume, akisoma taarifa ya mkoa huo, alisema kuna jumla ya zahanati 199, vituo vya afya 22, hospitali sita na ujenzi wa hospitali hiyo ya rufani ambayo imekoma kwenye jengo la utawala, pamoja na upungufu wa watumishi asilimia 52 na madaktari bingwa 21 na waliopo sita pekee.

Na Marco Maduhu - NIPASHE
Share:

RADI YAUA MAMA NA MWANAE WAKIWA SHAMBANI


Mama na mwanawe mwenye umri wa miezi sita wamefariki dunia papo hapo juzi baada ya kupigwa na radi wakati walipokuwa shambani katika Kijiji cha Msasa,wilayani Geita. 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi, Diwani wa Kata ya Busanda, Elias Kisome, aliwataja waliofariki kuwa ni Zainabu William (30) na mwanawe wa kike mwenye umri wa miezi sita, Happiness Bahati.

Akizungumzia mazingira ya tukio hilo, Diwani Kisome, alisema lilitokea saa 10 jioni wakati mama huyo na mwanawe alipokuwa shambani, akipanda mpunga.

Alisema mvua iliyoambatana na radi ilimpiga Zainabu na mwanawe aliyekuwa amembeba mgongoni na kufariki papo hapo.

Oktoba 17 mwaka jana wanafunzi sita wa darasa la pili na tatu katika shule ya msingi ya binafsi ya Emaco Vission English Medium School, iliyopo kata ya Nyankumbu katika Halmashauri ya mji wa Geita walifariki dunia baada ya kupigwa na radi na wengine 23 wakiwamo walimu wawili kulazwa katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Geita.

Chanzo- NIPASHE
Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO JANUARI 25,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 25, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger