Thursday, 17 January 2019

MWANAMKE AUAWA KWA KURARULIWA NA MAMBA SHAMBANI

Mnyama huyo aliwekwa pasipo kibali katika shamba kaskazini mwa Sulawesi.

Mwanamke mmoja raia wa Indonesia ameuawa na Mamba huko Sulawesi baada ya kuanguka karibu nae.

Deasy Tuwo, 44, inasemekana alikuwa akimlisha Mamba huyo kwenye shamba huko Sulawesi mahali anapofanyia kazi na sehemu ambayo mamba huyo alihifadhiwa bila kibali.


Mamba huyo mwenye kilo 700 aitwae Merry inasemekana alimng'ata mkono na sehemu kubwa ya tumbo.

Mnyama huyo amehamishiwa katika hifadhi wakati mamlaka ikimtafuta mmiliki, Tuwo alivamiwa na mamba wakati akimpatia chakula

Bi Tuwo alikuwa ni msimamizi wa maabara katika eneo hilo na alikuwa akimpatia chakula Merry tarehe 10 mwezi januari ambapo aliangukia mikononi mwamnyama huyo.

Wafanyakazi wenzie waliuona mwili wake asubuhi ya siku inayo fuata.

Chanzo:Bbc
Share:

SERIKALI YAMJIBU LISSU

Mbunge wa Singida mashariki (Chadema) Tundu Lissu.

 Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas amemjibu mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu, akidai kuwa mwakilishi huyo wa wananchi anazungumza uongo kuhusu maendeleo ya Tanzania.

Dk Abbas amesema kwamba licha ya kuulizwa mazuri ya Serikali lakini Lissu alishindwa kujibu na badala yake aliishia kubabaika.

Akihojiwa na kituo cha Utangazaji Uingereza (BBC) jana Januari 16, 2019, Lissu amezungumza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na maoni yake kuhusu maendeleo ya nchi, utawala wa katiba na mpango wake wa kugombea urais.

"Unakwenda Ulaya unaponda nchi yako eti haifuati Katiba wakati wewe mwenyewe kuanzia ubunge wako, sifa za ubunge wako na taratibu za uchaguzi wa ubunge wako vyote vipo kwenye Katiba na ndio maana ukawa mbunge,” alisema Dk Abbas.

Dk Abbas amedai Lissu hata alipoulizwa mazuri aliyoyaona licha ya changamoto zilizopo, alishindwa kujibu vyema.

"Angalia alivyoshindwa si tu kueleza jema moja la nchi yake baada ya kupewa fursa hiyo, bali kashindwa hata kueleza jema moja alilofanya yeye binafsi jimboni kwake, kaishia kubabaika tu," amedai Dk Abbas.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina dhamira tofauti na ile waliyonayo watu wa aina ya Lissu, hivyo itaendelea kutekeleza wajibu wake katika kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.

"Sisi tunapigania maendeleo na Watanzania wanaona kazi kubwa inayofanyika kote nchini iwe reli, maji, viwanda, umeme na mambo mengine. Hakuna wa kutuzuia katika kuiletea Tanzania maendeleo. Hakuna,” amesisitiza.

Chanzo:Mwananchi
Share:

WAJASILIAMALI KATA YA MWANGATA IRINGA WAUNGA MKONO JITIHADA ZA JPM WACHANGIA MILIONI 2.

NA Francis Godwin,Iringa WAJASILIAMALI wa kata ya Mwangata katika manispaa ya Iringa wamechanga jumla ya shilingi milioni 2 kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Dkt John Magufuli kwa ajili ya uendelezaji wa sekta ya elimu nchini. Wajasiliamali hao ambao walitumia pesa hizo kununua mifuko ya saruji 130 walikabidhi msaada huo kwa naibu meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Lyata kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi Jana. Akizungumza kwa niaba ya wajasiliamali hao Diwani wa kata ya Mwangata Edward Chengula mara baada ya kongamano la wajasiliamali alisema…

Source

Share:

BABA MZAZI WA MSANII ALI KIBA AFARIKI DUNIA.

Na Bakari Chijumba, Mtwara. Baba mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Alikiba Mzee Saleh amefariki dunia alfajiri ya leo Januari 17, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.. Inaelezwa kuwa, Mzee Kiba ambaye pia ni baba mzazi wa msanii Abdu Kiba na Zabibu Kiba amekua akiugua kwa muda sasa huku akiendelea kutibiwa. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Kariakoo mtaa wa Muheza jijini Dar es salaam (unaingilia China Plaza) ambapo mipango ya mazishi inafanywa. Kwa mujibu wa Ndg wa Marehemu, ratiba ya Mazishi ni kwamba, Maiti itaswaliwa katika…

Source

Share:

SPIKA NDUGAI : ZITTO KABWE ANANIPA TABU


 Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema mbunge anayempa shida pale anapotaka kumwadhibu ni Zitto Kabwe.

Ndugai ametoa kauli yake hiyo leo Alhamisi Januari 17, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.

Ndugai amesema amekuwa akichelea kumfukuza bungeni mbunge huyo wa Kigoma Mjini kwa kuwa ndiye pekee anayewakilisha Chama cha ACT-Wazalendo.

"Unajua niseme ukweli, huyu mbunge amekuwa akinipa tabu sana, ananipa tabu sababu ndio mbunge mmoja wa chama chake,” amesema Ndugai.

“Hawa wengine huwa nafukuza sababu wenzao wapo, sasa huyu (Zitto) ni mmoja tu wa chama chake (ACT Wazalendo).”

Na Kelvin Matandiko Mwananchi 
Share:

NAIBU WAZIRI WA MADINI STANSLAUS NYONGO AMEAGIZA WAMILIKI WA MGODI KUKAMATWA

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameamuru kukamatwa kwa Wamiliki wa mgodi wa Nyakavangala unaomilikiwa na Thomas Masuka and Partners kufuatia wamiliki hao kutofautiana juu ya taarifa waliyoiwasilisha kwa Naibu Waziri kuhusu namna mgodi huo unavyoendeshwa ikiwemo ulipaji wa kodi na mrabaha wa serikali.

Naibu waziri amewataka wamiliki hao kutoa maelezo ya kina kuhusu ni lini watalipa kodi zote wanazodaiwa na serikali baada ya kuonekana kuwa mgodi huo unadaiwa zaidi ya shilingi milioni 128 za mrabaha ambazo imedaiwa kuwa, wapo baadhi ya wamiliki ambao wamekuwa wakikusanya fedha hizo lakini zimekuwa hazilipwi.

Katika ziara yake mkoani humo, Naibu Waziri alisema kuwa pamoja na kujionea shughuli za uchimbaji katika migodi ya dhahabu ya Ulata na Nyakavangala, amebaini ukwepaji mkubwa wa kodi pamoja na mrabaha wa serikali.

Amemtaka Afisa madini kutoa maelekezo ya kina kuhusu suala zima la ulipwaji wa kodi na mrabaha wa serikali, huku akiagiza zoezi hilo pia limuhusishe Afisa Msimamizi wa madini aliyekuwepo katika kipindi ambacho fedha hizo hazikulipwa.

Hatutaki ugomvi hapa kwenye migodi. Tunataka mgodi ufanye kazi. Dhahabu ziuzwe mahali panapoonekana. Hapa naona hesabu za viroba tu. Mnunuzi wa dhahabu hapa ni nani”, alihoji Naibu Waziri Nyongo.

Wakati akizungumza na wachimbaji katika mkutano wa hadhara, amewataka wachimbaji hao kuchimba kwa kuzingatia usalama huku akisisitiza suala la kufuata sheria na taratibu huku akiwataka kutoa taarifa za uhakika kwa wale wote wanaokikuka sheria ikiwemo watoroshaji wa madini huku akisisitiza utoaji taarifa hizo usiwe wa majungu.

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwataka wamiliki hao kukaa chini na kukubaliana namna ya kulipa kiasi cha fedha ambacho wanadaiwa na serikali huku akimtaka afisa kutoka halmashauri anayehusika na masuala ya usimamizi wa fedha kuhakikisha kwamba fedha ambazo mgodi huo ulipaswa kuzilipa kama mrabaha zinapatikana.

Mgodi huo wa Nyakavangala unamilikiwa na Thomas Masuka kwa ushirikiano na wawekezaji wengine wazawa wapatao 20. Wakati akiagiza kukamatwa kwao, wamiliki 8 kati ya 20 ndiyo walikuwa wamehudhuria kikao kati yake na wamiliki hao.

Naibu Waziri Nyongo alitoa agizo hilo Januari 15 wakat akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
Share:

WAFANYAKAZI WA AIRTEL WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUINGILIA MFUMO WA MTANDAO

Wafanyakazi wawili wa kampuni ya simu ya Airtel na wengine tisa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya kuingilia mifumo ya mawasiliano ya kampuni hiyo.
Akiwasomea mashtaka, Wakili wa Serikali, Ester Martin akisaidiana na Erick Shija, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kelvin Mhina kuwa kati ya Septemba 9 na Desemba 24 mwaka jana, jijini Dar es Salaam washtakiwa walikula njama ya kutenda kosa la wizi.

Katika shtaka la pili alidai siku na mahali hapo, washtakiwa hao huku wakijua kuwa ni kinyume cha sheria walijaribu kutenda kosa la wizi.

Katika shtaka la tatu, washtakiwa Laizer na Mwenda kwa makusudi na kinyume cha sheria walisababisha kuingilia mfumo wa mawasiliano wa kampuni ya Airtel bila ya kuwa na kibali.

Shtaka la nne alidai kuwa washtakiwa wote walitoa taarifa za mfumo wa mawasiliano wa kampuni hiyo kinyume cha sheria.

Waliofikishwa mahakamani ni Rodgers Laizer na Nancy Mwenda ambao ni wafanyakazi wa Airtel, Erick Fidelisi, Zephaniah Maduhu, Anthony Masaki, Lumuli Stanford, Ndeshiwonasiya Malle, Davis Waseda, Goodluck Nyakira, Michael Onyango na Sylvester Onyango.


Washtakiwa walikana kutenda makosa hayo na mshtakiwa Masaki, Stanford, Eased na Mwenda walipata dhamana na wengine wamepelekwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kesi ime iatatajwa Januari 29, mwaka huu kwa kuwa upelelezi haujakamilika.

Chanzo:Mpekuzi
Share:

ALI KIBA AFIWA NA BABA YAKE MZEE SALEH KIBA

Hali ya simanzi na huzuni imegubika familia ya msanii wa bongo Fleva Ali Kiba baada ya babake kufariki dunia mapema leo.

Mzee Saleh Kiba alifariki katika hospitali ya Muhimbili ambapo alikuwa amelazwa.

Kulingana taarifa za  mdogo wa mwanamuziki huyo ambaye pia ni msanii Abdu Kiba alithibitisha habari hizo.

Msanii huyo amesema kuwa msiba unafanyika katika mtaa wa Kariakoo eneo la Muheza ambapo ndio nyumbani kwao.

Kulingana na afisa wa Uhisiano mwema katika hospitali ya Muhimbili Neema Mwangomo amesema kuwa Mzee Saleh alifikwa na mauti yake saa kumi na mbili alfajiri.

Aliongezea kuwa marehemu alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo tangu tarehe 27 mwezi Disemba.

Chanzo:Bbc
Share:

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO ALHAMISI 17.01.2019 HIGUAIN KUTUA DARAJANI

Chelsea wameamua kumsajili Gonzalo Higuain baada ya Juventus kukubali ofa yao. Mshambuliaji huyo raia wa Argentina alikuwa akichezea AC Milan kwa mkopo. (Telegraph)

Atletico Madrid wanakaribia kumsaini mshambuliaji wa Chelsea lvaro Morata, 26, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa euro milioni45. (Sky Sports)

Arsenal wako tayari kutumia sehemu ya mshahara wa Mesut Ozil endapo watafanikiwa kumuuza ili kumsajili mchezaji mwingine.

Ozil ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika klabu hiyo. (Mirror)

West Ham wanapania kumnunua mshambuliaji wa Celta Vigo na Uruguay Maxi Gomez, 22, kujaza pengo litakaloachwa na Marko Arnautovic. (Sky Sports)

Manchester City huenda wakapoteza nafasi ya kumsajili Frenkie De Jong kutoka Ajax baada ya Paris St-Germain kuonyesha azma ya kutaka kumununua kiungo huyo.

Chanzo:Bbc
Share:

RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU ZAIMULIKA SAUDIA NA CHINA

Saudia na China zamulikwa katika ripoti ya dunia ya haki za binadamu

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch limekosoa ukiukaji wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia na China katika ripoti yake ya dunia ya mwaka 2019, yenye kurasa 400.

Ripoti hiyo pia inazikosoa nchi za Ulaya, lakini Mkurugenzi wa shirika hilo nchini Ujerumani Wenzel Michalski anasema licha ya yote hayo kuna sababu ya kuwa na matumaini kidogo.

Shirika la Human Rights Watch limekuwa likichapisha ripoti hiyo kila mwaka tangu mwaka 1989, mataifa yenye uongozi wa kidikteta ambayo haki za watoto, wanawake na wanaume zinakiukwa ndiyo yanayolengwa.

 Mwaka huu kama anavyosema Wenzel Michalski wanaharakati wa haki za binadamu hawajajikita tu katika baadhi ya nchi kwa ujumla bali kwa watu binafsi.

China inajaribu kuiuza sera yake ya ukiukaji wa haki za binadamu duniani

Chanzo:Dw
Share:

ZITTO KABWE AITAKA CHADEMA KUTOA TAARIFA ZA UGONJWA WA MBOWE

Share:

IDADI YA WALIOUAWA KENYA YAFIKIA 21,WENGINE 50 HAWAJULIKANI WALIPO

Inspekta Jenerali wa Kenya Joseph Boinnet

Idadi ya waliouawa katika shambulizi la kigaidi nchini Kenya imefikia 21, baada ya serikali ya Kenya kutangaza kuwa miili mingine 6 imepatikana kutoka katika kifusi kilicho kuwa katika eneo hilo.
Pia taarifa iliyotolewa inasema kuwa afisa polisi mmoja alifariki kutokana na majeraha wakati akipewa matibabu maalum.

Akizungumza na vyombo vya habari Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Kenya Joseph Boinnet ametoa taarifa hiyo Jumatano jioni.

Amefafanua kuwa kati ya waliouwawa kuna Wakenya 16, Muingereza moja, Mmarekani mmoja na wengine wa mataifa mbalimbali.

Hata hivyo IGP ametahadharisha vyombo vya habari kujiepusha kutoa ripoti ambazo zinaweza kuhatarisha uchunguzi ambao unaendelea baada ya shambulizi hilo.

Mapema Jumatano asubuhi Rais Uhuru Kenyatta amesema alisema kuwa watu wenye silaha waliovamia eneo la biashara la hoteli na kuuwa watu 14, “wameuwawa” baada ya takriban masaa ishirini ya mapambano ambapo mamia ya raia waliokolewa na wengine wanaokadiriwa kuwa 50 bado hawajulikani walipo.

Kikundi cha Al-Qaeda chenye mafungamano na kundi la Al-Shabaab kimedai kuhusika na shambulio hilo. Kikundi hicho kimekuwa kikilenga kuishambulia Kenya tangu ilipopeleka jeshi lake nchini Somalia Octoba 2011 kupambana na kikundi hicho cha wanajihadi.

Chanzo:Voa
Share:

FAINALI 7 ZA KIBABE ZILIZOAMULIWA NA RONALDO


Cristiano Ronaldo katika matukio mbalimbali.

Baada ya kufunga bao la ushindi jana katika fainali ya Kombe la Italia, mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronalado sasa amefunga mabao 8 katika fainali 7 zilizopita.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 33, jana usiku aliiwezesha timu yake kutwaa taji la Copa Italia kupitia bao lake alilofunga dakika ya 61 dhidi ya AC Milan huku Juventus ikifikisha makombe 8 ya Italia na kuwa ndio klabu iliyoshinda mara nyingi zaidi ikiipiku AC Milan yenye mataji 7.

Fainali ambazo Ronaldo amefunga mabao

Ronaldo alifunga mabao mawili kwenye fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya msimu wa 2016/17 Real Madrid ikishinda 4-0 dhidi ya Juventus.

Ronaldo pia alifunga bao 1 kwenye ushindi wa 2-1 iliopata Real Madrid dhidi ya Barcelona kwenye fainali ya 'Spanish Super Cup'.

Ronaldo pia amefunga jumla ya mabao 4 katika fainali mbili tofauti za Klabu bingwa ya Dunia. Alifunga mabao mawili dhidi ya Kashima Antlers mwaka 2016. Pia akafunga mabao mawili dhidi ya Gremio mwaka 2017.

Bao lake la jana limekuwa bao la nane katika fainali 7 zilizopita huku fainali zote timu alizokuwa akizichezea yaani Real Madrid na Juventus zimetwa ubingwa.
Share:

Maajabu : KUTANA NA MTU HUYU ANAMALIZA MARA 50 BILA KUFANYA TENDO LA NDOA


Msichana Amanda Gryce, mkazi wa Florida nchini Marekani, anasumbuliwa na ugonjwa ambao sio wa kawaida, unaomfanya afikie mshindo takriban mara 50 kwa siku, bila ya kufanya tendo la ndoa na mtu yeyote.

Msichana huyo mwenye miaka 22, anasema alianza kugundua ana tatizo hilo akiwa na miaka 6, na amekuwa akikabiliana nalo bila kujua hatma yake ni nini, na amekuwa akikutwa na hali hiyo muda wowote na mahali popote bila kufanya tendo la ndoa.

“Ilitakiwa iwe ni kitu kizuri kama ambavyo inatakiwa, imekuwa maumivu kwangu, kwa sababu inatokea sana, inaweza ikatokea hata mara 50 kwa siku au mara tano mpaka kumi kwa saa moja, inatokea nikiwa na rafiki zangu, au nikiwa sehemu tu na watu wengine, nikipanda gari ndio inazidi kutokana na mtikisiko wake, ni aibu sana”, amesema Amanda.

Tatizo hilo ambalo mwenyewe anadai limekuwa likimtesa maisha yake yote na kumfanya asifurahie maisha ya kimapenzi, kilimfanya awahi kuwaza kujiua, lakini mpenzi wake Stuart Triplett, amekuwa akimpa ushirikiano sana wa kutafuta tiba na kumfanya awe na tumaini.

Kutokana na hali hiyo, Amanda ameshakutana na baadhi ya madaktari kujaribu kupata tiba, lakini mpaka sasa hajapata ufumbuzi kutokana na ugonjwa huo kutokuwa na tiba ya moja kwa moja, hivyo kumpa njia mbadala za kukabliana nao, ikiwemo kufanya mazoezi.

Tatizo hilo kitaalamu linajulikana kama 'Persistent Genital Arousal Disorder'ambalo hutokea mara chache sana kwa binadamu. Mpaka sasa haujajulikana tiba sahihi ya kuweza kumaliza tatizo hilo, lakini madaktari wa masuala hayo wameshauri iwapo mtu atagundulika kuwa na tatizo hilo, atatakiwa kuhudhuruia tiba ya mwili 'Physiotherapy'.
Amanda akiwa na mpenzi wake Stuart Triplett
Share:

TUNDU LISSU : NIPO TAYARI KUGOMBEA URAIS...SINA MPAMBANO NA LOWASA

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu ameendelea kusimamia msimamo wake kuwa yupo tayari kugombea urais mwaka 2020 endapo chama chake kitaona anatosha kusimama katika nafasi hiyo.

Akihojiwa na Shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) Lissu amesema kauli hiyo haina maana yoyote kwamba anapambana na Edward Lowassa ambaye alisimamishwa na Chadema mwaka 2015 kuwania nafasi hiyo.

“Kama chama changu pamoja na vyama tunavyoshirikiana navyo na Watanzania wanaotuunga mkono watasema kwamba mimi nafaa kuwawakilisha nitakuwa tayari kufanya hivyo.

Alisema, “Sina mpambano na Lowassa uamuzi wa kugombea urais sio wangu wala Lowassa wala Mbowe ni vikao vya chama. Inaweza kwenye vikao viongozi nikaambiwa sitoshi nitakubali na inawezekana vikao vikamwambia Lowassa aniachie mimi nipambane kwa sababu mapambano ya sasa yanahitaji nguvu inawezekana kabisa”.

Kuhusu kwamba ni lini atarejea nchini alieleza, “Daktari wagu atakaposema sasa una uwezo wa kurudi kwenu nitarudi Tanzania.

Lissu alieleza kuwa licha ya kwamba hadi sasa Serikali imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwabaini waliomshambulia atarudi na itawajibika kumlinda kwa saa 24.


Na Elizabeth Edward,Mwananchi
Share:

RADI YAJERUHI WANAFUNZI 14 MULEBA

Wanafunzi 14 wa shule ya sekondari Rulongo wilayani Muleba Mkoa wa Kagera wamelazwa katika hospitali ya Lubya wilayani humo baada ya kujeruhiwa na radi.

Akizungumza jana Jumatano Januari 16, 2019 mganga mkuu wa hospitali hiyo, George Kasibante amesema tukio hilo limetokea leo na kwamba kati ya wanafunzi hao, watatu wana hali mbaya baada ya kuungua sehemu kubwa mwilini.

Amesema mwanafunzi mmoja amepoteza fahamu na madaktari wanajitahidi kuhakikisha anarejea katika hali yake ya kawaida, kwamba wengine walipata zaidi mshtuko.

Amesema radi hiyo ilipiga vyumba vya madarasa ya kidato cha pili na tatu, kwamba shule hiyo ipo mlimani eneo ambalo radi hupiga zaidi na kuwashauri wanafunzi kutojikinga na mvua katika maeneo yenye miti mirefu.


Na Shaaban Ndyamukama, Mwananchi
Share:

MWILI WAOKOTWA UKIWA UMEFUNGWA KWENYE KIROBA

Mwili wa mtu mmoja umeokotwa eneo la sayansi jirani na Chuo cha Ustawi wa jamii ukiwa umefungwa kwenye kiroba.

Kwa mujibu wa ITV, Mjumbe wa mtaa huo Bi Fortunata Mshindo amesema jana mchana yeye na wananchi wengine walipita katika eneo hilo na hakukua na kitu chochote huku pia akisisitizia uongozi wa manispaa kuweka taa katika eneo hilo ili kupunguza matukio ya kihalifu.


Maafisa wa Jeshi la Polisi walifika eneo la tukio wakauchukua mwili huo kwa uchunguzi zaidi


Chanzo ITV

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger