Rais wa Marekani Donald Trump ametishia ‘kuiangamiza Uturuki kiuchumi’ iwapo taifa hilo litawashambuliwa vikosi vya wakurdi nchini Syria baada ya wanajeshi wa Marekani kuondoka Syria. Katika ujumbe wake alioutuma kwenye mtandaoi wa kijamii Twitter, Trump amesema hakutaka Wakurdi kwa upande wao nao pia waichokoza Uturuki. Vikosi vya Marekani vimepambana kwa ushirikiano na wanamgambo wa Kikurdi kaskazini mwa Syria dhidi ya kundi la Islamic State (IS). Rais Recep Tayyip Erdogan amezungumza kwa hasira kuhusu Marekani kuliunga mkono kundi hilo, na kuapa kuliangamiza. Kauli ya Trump Jumapili inafuata shutumza zaidi dhidi ya…
Monday, 14 January 2019
Picha:KANISA LA P.A.G.T LATOA MSAADA KWA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KISHAPU
Na Malaki Philipo- Malunde 1 blog
Kanisa la Pentekoste Assemblise of God Tanzania (P.A.G.T) limetoa msaada wa nguo na vifaa vya shule kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kata ya mwadui lohumbo Wilayani Kishapu.
Msaada huo umekabidhiwa wakati wa ibada maalumu ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu iliyofanyika jumapili Januari 13,2019 .
Akikabidhi msaada huo Askofu wa kanisa la P.A.G.T Nyenze Mchungaji Robert Joseph ameiomba jamii pamoja na taasisi zisizo za kiserikali kuunga mkono juhudi za serikali kutoa misaada mbalimbali kwenye jamii, pia utoaji ni agizo la mungu linaloashiria upendo kwa wahitaji.
“sababu Mungu anatupenda wote hivyo yatupasa kuwasaidia wahitaji na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuwasaidia wanyonge,” alisema Joseph.
Akizungumza kwenye ibada hiyo kaimu afisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Kishapu Ndola Masunga ambaye amemuwakilisha mkuu wa wilaya kishapu Nyabaganga Talaba amewapongeza walezi ambao wamechukua jukumu la ulezi bila manyanyaso kwa watoto .
“Tunashuhudia kwenye ofisi zetu za maendeleo ya jamii vihoja vingi vya kuwanyanyasa watoto wanaoishi mazingira magumu,niwapongeze walezi waliochukua jukumu la kuwalea watoto bila ya kuwanyanyasa na kuwapatia mahitaji muhimu,” alisema Ndola.
Kanisa hilo limetoa msaada wa nguo na vifaa vya shule kwa wanafunzi wanaoishi mazingira magumu lengo ikiwa ni kuwasaidia wazazi na walezi , diwani wa kata ya Masengwa Nicodemas Simon amesema msaada huo ni chachu ya kufanya vizuri kimasomo kwa wanafunzi hao.
Askofu wa kanisa la P.A.G.T Nyenze Mchungaji Robert Joseph ameiomba jamii pamoja na taasisi zisizo za kiserikali kuunga mkono juhudi za serikali kutoa misaada mbalimbali kwenye jamii yenye wahitaji.. Picha zote na Steve Kanyefu-Malunde 1 blog
Kaimu Afisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Kishapu Ndola Masunga ambaye amemuwakilisha mkuu wa wilaya kishapu Nyabaganga Talaba amewapongeza walezi ambao wamechukua jukumu la ulezi bila manyanyaso kwa watoto .
Diwani wa Kata ya Masengwa Nicodemas Simon akisisitiza juu ya umuhimu wa msaada huo huku akisema kuwa msaada ni chachu ya kufanya vizuri kimasomo kwa wanafunzi hao.
Baadhi ya watoto waliopatiwa msaada wakiwa kanisani .Mgeni rasmi kaimu afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Kishapu Ndola Masunga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba Akikabidhi msaada kwa watoto hao.
Zoezi la kukabidhi msaada huo likiendelea
Baadhi ya Wazazi/walezi wa watoto hao wakifuiatilia kwa umakini zoezi la utolewaji msaada kwa watoto hao
DE GEA KWA KIWANGO HICHO BADO SAANA-SOLSKJAER
David de Gea huenda akajijengea hadhi ya kuwa mlinda lango bora zaidi kuwahi kuichezea klabu ya Manchester United hasa baada ya ustadi wake Jumapili, kwa mujibu wa kaimu meneja wao Ole Gunnar Solskjaer. Mhispania huyo mwenye miaka, 28, aliokoa mipira 11 na kuwawezesha United kuwalaza Tottenham 1-0 katika mechi iliyochezewa uwnaja wa Wembley. Katika miaka 11 aliyokuwa Old Trafford akiwa mshambuliaji, Solskjaer alicheza na magolikipa stadi kama vile Edwin van der Sar na Peter Schmeichel. “Tumekuwa na magolikipa wazuri sana katika klabu hii na nafikiri kwa sasa anawatishia wote wawili…
MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA UPINZANI TANZANIA
Mahakama nchini Tanzania imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na vyama vya upinzani nchini humo kupinga Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018. Shauri hilo, lilifunguliwa na muungano wa vyama 10 vya upinzani wakidai unakiuka haki za Kikatiba za kisiasa kwa kuzifanya shughuli mbalimbali za kisiasa kuwa jinai. Wanasiasa hao wanadai muswada huo unampa mamlaka makubwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuingilia mambo ya ndani ya vyama hivyo ikiwemo uchaguzi wa viongozi na kusimamisha uanachama kwa wanachama wa vyama hivyo. Pia walikuwa wanapinga kifungu cha…
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 15.01.2019: WILSON, AKE, LLORENTE, NEVES, ARNAUTOVIC, BABEL
Bournemouth iko radhi kumuuza mshambuliaji wa England Callum Wilson kwa Chelsea kwa pauni £75m – mara 25 zaidi ya kiwango walicholipa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mnamo 2014. (Star) Wolves watapambana na Chelsea katika kuwania kumsajili Wilson, ambaye amefunga mabao 10 kufikia sasa msimu huu.(Birmingham Mail) Chelsea pia inataka kumsajili upya beki wa kati wa Bournemouth Nathan Ake, miaka miwili tu baada ya kumuuza Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa Cherries. (Sun) Mshambuliaji wa Tottenham na timu ya taifa ya Uhipania Fernando Llorente, mwenye umri…
DC KIZIGO AWAKARIBISHA WWF NAMTUMBO..ASEMA ELIMU YA UHIFADHI INAHITAJIKA KWA WANANCHI.
Na Bakari Chijumba, Mtwara Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,Sophia Kizigo amelipongeza Shirika la kimataifa la utunzaji wa mazingira (WWF), kwa elimu ya uhifadhi wanayoendelea kuitoa huku akiwaomba kujikita zaidi kutoa elimu vijijini hasa kwa kuwatumia watendaji wa vijiji ambao watasambaza taarifa kwa haraka. Bi.Kizigo, ametoa kauli hiyo wakati Wafanyakazi wa WWF, walipotembelea ofisi yake kujadili miradi ya pamoja wanayoweza kufanya na wilaya ya Namtumbo katika mwaka huu wa 2019 ili kuboresha uhifadhi. “Mnaweza kuandaa semina ya watendaji wote wa vijiji, mukawapa elimu ya kutosha wakasambaza kwa wanavijiji, mie…
MRADI WA MAJI WAMLAZA NDANI MHANDISI WA MAJI.
Na Allawi Kaboyo-Kagera. Naibu waziri wa maji Jumaa Aweso amemuagiza kamanda wa polisi wilaya ya Muleba kumkamata mhadisi wa maji wilayani humo Boniface Lukoho na kuagiza kutafutwa kwa mkandarasi M/S SAGUCK ENGINEERING baada ya kukagua mradi wa maji Katoke ulioanza kujengwa novemba 2013 na kutakiwa kukamilika mei 2014, wenye thamani ya shilingi milioni 467 na zaidi ya shilingi milioni 400 zikiwa zimeshalipwa huku mradi huo ukiwa hautoi maji. Naibu waziri Jumaa Aweso akiwa katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Kagera, amefika wilayani Muleba katika mradi wa maji Katoke na kuwakuta…
VYAMA VYA SIASA VYAALIKWA KUTOA MAONI MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA.
Na,Mwandishi wetu. Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria inatarajia kukutana na wawakilishi wa vyama vya siasa Januari 19 na 20, 2019 kuwasikiliza na kupokea maoni yao kuhusu muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018. Kamati hiyo itapokea maoni yao baada ya kumaliza vikao vyake na wadau wengine vitakavyofanyika Januari 17 na 18, 2019 mjini Dodoma kuhusu muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2018 na kufuatiwa na mkutano wake na wawakilishi wa kila chama cha siasa chenye usajili wa…
AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMPA MIMBA DADA YAKE
Gabriel Nyantori (25) amefikishwa mbele ya mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti mkoani Mara akituhumiwa kwa makosa ya kuzini na dada yake na kumpa mimba.
Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile, mwendesha mashitaka, Faru Mayengela leo Jumatatu Januari 14, 2019 amesema mshitakiwa anakabiliwa na makosa mawili.
Amesema kosa la kwanza ni kuzini na dada yake mwenye umri wa miaka (16) mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Kibeyo na kosa la pili ni kumpa mimba dada yake, makosa ambayo aliyatenda Aprili 30, 2018 nyumbani kwao, Kibeyo.
Na Anthony Mayunga, Mwananchi
POLISI WATOA SABABU ZA TRAFIKI KUMTEMBEZEA KICHAPO DEREVA WA LORI
Jeshi la Polisi mkoani Songwe limeeleza sababu ya askari wa usalama barabarani kumshambulia dereva kwa kumpiga kuwa alitumia lugha ya matusi na kutotii amri ya kumtaka atoe ushirikiano kwa wanausalama hao ambao walikuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana na maofisa toka Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra).
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa Yusuph Sarungi amewaambia waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 14, 2019 kuwa tukio hilo lilitokea juzi Jumamosi Januari 12, 2019 saa 2:30 asubuhi katika eneo la Transforma, halmashauri ya mji wa Tunduma wilayani Momba wakati askari hao wakishirikiana na maofisa toka Sumatra wakiwa kwenye ukaguzi wa magari mbalimbali.
Amesema dereva huyo Mawazo Jairos (29) mkazi wa Mbeya aliyekuwa akiendesha gari aina ya Mistubishi Fuso lenye namba za usajili T842 AAC, baada ya kusimamishwa alianza kutoa lugha za kashifa na matusi kwa askari na maofisa wa Sumatra.
Kamanda huyo amesema Jairos aliliondoa gari bila ya kuruhusiwa kwa kupitia barabara ya vumbi hali iliyolazimu askari hao kumfuatilia na kumkamata tena katika eneo la Makambini ambapo walimzuia tena.
Sarungi amesema dereva huyo aliteremka kwenye gari kwa jazba huku akiendelea kutoa matusi na kumshambulia askari......
Na Stephano Simbeye, Mwananchi
MAKOCHA WAPYA WA SINGIDA UNITED WAANZA KUCHAPA KAZI
Kikosi cha Singida United
Klabu ya soka ya Singida United imethibitisha kuwa makocha wao wapya wamewasili jijini Mwanza na kuungana na timu tayari kuanza kazi ya kusaka alama tatu dhidi ya Mbao FC.
Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga ameiambia www.eatv.tv kuwa benchi lao hilo jipya la ufundi limechukua majukumu tayari kutoka kwa makocha waliokuwa na timu.
''Makocha wetu wameshaungana na timu Mwanza, tayari kwa mchezo dhidi ya Mbao FC siku ya Jumatano, makocha hao ni kocha mkuu Dragan Popadic, kocha msaidizi Dusan Kondic na wataendelea na kocha wa makipa Mirambo'', amesema Sanga.
Makocha wapya wa Singida United.
Aliyekuwa kocha mkuu wa Singida United, Hemed Morocco amepewa majukumu katika timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys. Makocha wengine Jabir Mahamoud na Shadrack Sanjigwa wataendelea na kikosi B cha timu hiyo.
Singida United ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya tano, kwasasa ipo katika nafasi ya 10 wakiwa na alama 24 katika mechi 20 walizocheza.
Via>> EATV
MWANAFUNZI AIBURUZA SHULE MAHAKAMANI KISA NDEVU
Mwanafunzi wa chuo cha St. John nchini Zimbabwe ameupeleka uongozi wa chuo hicho mahakamani, baada ya kuzuiwa kuingia chuoni kwa kosa la kufuga ndevu.
Baba wa mtoto huyo Bw. Mohammed Ismail, amefungua shtaka rasmi kwa niaba ya mtoto wake kwenye Mahakama Kuu ya nchi hiyo, akidai kwamba kitendo hicho ni kuvunja katiba ya nchi na unyanyasaji.
Akiendelea kuelezea tukio hilo, Bw. Mohamed amesema kwamba mtoto wake huyo amekuwa akirudishwa mara kwa mara na uongozi wa chuo, ili anyoe nywele wakidai kuwa anakiuka sheria za chuo.
Baba huyo amesema kwamba suala hilo linaruhusiwa kwa mujibu wa dini yao ya Kiislam na kwamba mtoto wake alikuwa anasoma ili aje kuwa 'Imam', lakini uongozi wa chuo hauruhusu suala hilo, jambo ambalo limekuwa likimpa shida mwanafunzi huyo kwa kurudishwa nyumbani mara kwa mara.
Hata hivyo Mahakama ya nchi hiyo bado haijataja tarehe ya kusikiliza kesi hiyo.
MBOWE,MATIKO WAITWA MAHAKAMA YA RUFAA
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wakiwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam
KESI ya kupinga kurejeshewa dhamana iliyofunguliwa na serikali dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasim na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Mwekahazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (BAWACHA), Esther Matiko, itasikilizwa Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam, tarehe 18 Februari mwaka huu.
Serikali iliwasilisha Mahakama ya Rufaa, maombi ya kuwazuia Mbowe na Matiko kurejeshewa dhamana zao. Ni baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, kutupilia mbali mapingamizi ya serikali yaliyotaka mahakama hiyo kutosikiliza shauri lililofunguliwa na Mbowe na Matiko.
Kwa mujibu wa vyanzo via taarifa kutoka Mahakama ya Rufaa na ambazo zimethibitishwa na Prof. Abdallah Safari, ambaye anaongoza jopo la mawakili katika kesi hiyo, ni kwamba “Mbowe na Matiko, watafika mbele ya majaji wa mahakama ya rufaa, Jumatatu ya tarehe 18 Februari.”
Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai, mkoani Kilimanjaro na Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni, alifutiwa dhamana na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa.
Katika uamuzi wake, mahakama ilisema, maelezo yaliyotolewa na Mbowe, mdhamini wake na wakili wake, yalilenga kuidanganya mahakama.
Naye Matiko ambaye pia ni mbunge wa Tarime Mjini, alifutiwa dhamana na mahakama baada ya kushindwa kufika mahakamani kwa mara mobile mfululizo kwa maelezo kuwa alikuwa nje ya nchi kwa shughuli za Bunge.
Chanzo- Mwanahalisionline
WATAWA,WANAKIJIJI WATAKIWA KUTUMIA BUSARA KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI .
Na.Amiri kilagalila. Wakazi wa Kijiji cha MADOBOLE Kata ya LUPONDE Wilayani NJOMBE pamoja na Shirika la Watawa wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Njombe Wametakiwa kutumia busara kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya Miaka Kumi na Tatu Sasa. Kauli Hiyo Imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka mara baada ya kutembelea eneo lenye mgogoro na kusikiliza pande hizo mbili zinazogombewa eneo lililopo ndani ya eneo linalodaiwa kumilikiwa kisheria na watawa hao. “Tutawatuma wataalamu hapa wachukue ramani ya shamba hilo lote namba 535 waje wapitie mipaka…
MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA ZITTO NA WENZAKE KUPINGA MUSWADA
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeifuta kesi iliyofunguliwa na Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe na wenzake wa vyama vya upinzani waliyokuwa wakiitaka mahakama hiyo kuzuia kusomwa kwa Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wakidai kuwa uko kinyume na katiba ya nchi. Mahakama imetoa uamuzi huo leo Jumatatu, Januari 14, 2018 ambapo walalamikaji, Zitto na wenzake wamekubali maamuzi hayo na kusema sasa nguvu yao ni kwenda kuupinga muswada huo kwenye kamati za bunge. Jaji Benhajo Masoud amesema Mahakama imeliondoa shauri hilo baada ya waombaji kuchanganya…
MAMA ALIYEMFANYIA MTOTO UKATILI AFIKISHWA MAHAKAMANI.
Na,Naomi Milton Serengeti. Mwanamke mmoja aitwaye Penina Petro(20) mkazi wa Kijiji cha Nyamakendo wilayani hapa amefikishwa mbele ya mahakama ya wilaya ya Serengeti kwa kosa la kumfanyia ukatili mtoto mwenye umri wa miaka 6(jina limehifadhiwa). Mwendesha mashtaka wa Jamhuri Faru Mayengela mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile alisema katika shauri la Jinai namba 5/2019 mshitakiwa anakabiliwa na kosa moja la utesaji wa mtoto kinyume na kifungu namba 169 A cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 12…
BIBI ANUSURIKA KUFA AKIPAMBANA NA MAMBA AKIOGA ZIWA VICTORIA
Mkazi wa kitongoji cha Mwibale wilayani Serengeti, Chibona Matoyo (64) akihojiwa na Mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Daniel Makaka (kushoto) baada ya bibi huyo kunusurika kifo kufuatia kushambuliwa na mamba alipokuwa akioga ndani ya Ziwa Victoria, wilayani humo.
Chibona Matoyo (64), mkazi wa Kijiji cha Kanyala Wilaya ya Sengerema, Mara amenusurika kifo baada ya kujeruhiwa na mamba wakati akioga katika Ziwa Victoria.
Katika tukio hilo lilitokea Alhamisi iliyopita, Chibona alivunjika mikono na kujeruhiwa paji la uso na sasa anapatiwa matibabu kwenye Kituo cha Afya Mwangika, Buchosa wilayani humo.
Akizungumza na Mwananchi jana, mama huyo mwenye watoto watano na wajukuu tisa, alisema wavuvi ndio waliookoa maisha yake baada ya kupiga kelele akiomba msaada.
“Walipoona napiga kelele walifika eneo la tukio na kunikuta napambana na mamba, walinisaidia kujinasua, walifanikiwa,” alisema.
Baada ya kupata taarifa za tukio hilo, mume wa Chibona, Ernest Majula (81) aliangua kilioakisema mkewe amepata kilema na kuiomba Serikali kuchukua hatua kuwadhibiti wanyama hao.
Mtoto wa mama huyo, Agnes Majula alisema wamekuwa na mazoea ya kwenda kuoga ziwani wakiamini kuwa kufanya hivyo ni vizuri zaidi kuliko majumbani mwao.
Daniel Makaka - Mwananchi