Thursday, 10 January 2019

JPM ASOMA SMS ZA WATEULE WAKE " ENDELEENI KUGOMBANA TU...MTAGOMBANIA VIJIJINI SIKU MOJA'


Rais John Magufuli jana alieleza jinsi alivyosoma meseji za watendaji wake serikalini na kubaini baadhi yao wanagombana badala ya kufanya kazi kwa ushirikiano katika maeneo yao.

Alisema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam jana baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua.

Alitoa mfano jinsi alivyosoma meseji za majibizano kati ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, (Tamisemi), Zainabu Chaula ambaye jana aliapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya.

“Nilikuwa nazisoma meseji; meseji ya Waziri wa Afya na meseji ya Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi, wanajibizana wee na wote wanatoka Tanga. Huyu mwingine anakaa kimya, huyu mwingine anashindilia maneno, nikaona nani anashindiliwa maneno zaidi, nikasema hawa njia ya kuwakomesha niwaweke wizara moja,” alisema Rais Magufuli.

Alisema wote wawili wanafanya kazi vizuri, hivyo ameona bora wakae wizara moja. Alimpongeza Chaula kwa jitihada zake za kusimamia ujenzi wa hospitali zaidi ya 300 ndani ya miaka mitatu.

Mbali ya viongozi hao, Rais Magufuli pia alisema anafahamu jinsi watendaji katika baadhi ya halmashauri wanavyogombana. Alitolea mfano Halmashauri ya Nyasa ambako alisema mkurugenzi na mkuu wa wilaya hawaivi.

Alitaja mgogoro mwingine kuwa uko Gairo ambako alisema mbunge wa anagombana na mkuu wa wilaya. Mbunge wa Gairo ni Mbunge wa jimbo hilo Ahmed Shabiby (CCM), na Mkuu wa Wilaya ni Siriel Mchembe.

Alisema mbunge amefikia hatua ya kutuma maneno ya kumtukana DC na kusema anashindwa kuelewa kwamba kuna kamati za nidhamu za CCM ambazo zinaweza kumfanya apoteze ubunge. 

“Nimewaangalia tu, I hope (natumai- mbunge) atafika siku moja aombe msamaha kwenye Bunge,” alisema Rais Magufuli na kuongeza:

“Pale Dodoma, mkurugenzi wa Jiji na DC walikuwa wanagombana, nika-send message (nikatuma ujumbe) kwamba ‘endeleeni kugombana tu, mtagombania vijijini siku moja. Wamenyamaza naona yameisha,”

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ni Godwin Kunambi na DC ni Patrobas Katambi.


Na Peter Elias, Mwananchi
Share:

RAIS TRUMP AONDOKA KWA HASIRA KWENYE MKUTANO NA WANADEMOCRATICS

Rais Trump wa Marekani anaelekea katika mpaka na Mexico ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kujenga ukuta,siku moja baada ya kutoka katika mkutano wa majadiliano wakati wapinzani wa ujenzi huo kutoka chama cha Democratic 

Donald Trump alivurumuka na kutoka katika mkutano na viongozi wa mabaraza ya bunge la Marekani " nilisema kwaheri," aliandika katika ukurasa wa Twitter muda mfupi baada ya mkutano huo, wakati juhudi za kumaliza kufungwa kwa sehemu shughuli za serikali, ziliingia katika mparaganyiko mkubwa. 

Mamia kwa maelfu ya wafanmyakazi wa serikali wanakabiliwa sasa na kukosa mishahara hadi kesho Ijumaa.


Wakati atakaposimama kwa muda leo mjini McAllen , Texas , Trump atafanya ziara katika kituo cha mpakani cha doria kwa ajili ya mazungumzo kuhusiana na uhamiaji na usalama wa mpakani, na kupata maelezo kuhusu usalama wa mpaka.

 Lakini Trump ameelezea shaka shaka yake kwamba kujitokeza kwake pamoja na matamshi hayatabadilisha mawazo ya mtu yeyote, wakati akitafuta kupata dola bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa ukuta ambao umekuwa ni ahadi yake kuu tangu alipokuwa akifanya kampeni ya urais.

Mazungumzo hayo yalizusha uvumi zaidi juu ya iwapo Trump atatangaza dharura ya kitaifa na kujaribu kuidhinisha ujenzi wa ukuta huo binafsi iwapo baraza la Congress halitaidhinisha fedha anazotaka.

Chanzo:DW
Share:

RAIS TRUMP AKAZIA UJENZI WA UKUTA, ALITAKA BUNGE KUIDHINISHA DOLA BILIONI 5.7

                     Rais wa Marekani Donald Trump.

 Rais wa Marekani Donald Trump wanawake na watoto ni waathirika wakubwa wa mfumo ulioharibika kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu akisema idara za doria mpakani hazina tena nyumba za kuwapatia hifadhi wahamiaji na haziwezi kuendelea na utaratibu kwa watu wanaotafuta hifadhi.

Trump anasema kuna mzozo wa kibinadamu na usalama unaoendelea kuwa mkubwa kwenye mpaka wa Marekani na Mexico akiueleza kuwa ni mzozo wa moyo na kiroho.

Katika hotuba yake ya kwanza ya kitaifa kutoka chumba cha Oval Office ndani ya White House Rais Trump alifafanua hoja yake ya kujenga ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico lakini hakutangaza hali ya dharura ya kitaifa ambayo itamruhusu kujenga ukuta bila idhini ya bunge.


Alisema wakati wamarekani wanaumizwa kutokana na kile alichokieleza kutodhibitiwa wahamiaji haramu Rais Trump alisema wamarekani wenye asili ya Kiafrika na asili ya Amerika Kusini wanaathirika zaidi kwa sababu fursa za ajira zimechukuliwa na wahamiaji.


Trump alisema wanawake na watoto ni waathirika wakubwa wa mfumo ulioharibika kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu akisema idara za doria mpakani hazina tena nyumba za kuwapatia hifadhi wahamiaji na haziwezi kuendelea na utaratibu wote kwa watu wanaotafuta hifadhi.

Chanzo:Voa


Share:

WENGER KUREJEA KWENYE UKOCHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA 2022

Arsene Wenger.

Meneja wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger anajipanga kurudi katika kazi yake ya ukocha, huku ripoti zikieleza kuwa ataifundisha Timu ya Taifa ya Qatar katika kuelekea michuano ya Kombe la Dunia la 2022.

Wenger amehusishwa na tetesi kadhaa za kufundisha timu mbalimbali zikiwemo PSG, Real Madrid tangu alipoondoka Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita, akisisitiza kuwa anahitaji changamoto mpya na kwamba Qatar inajipanga kuchukua fursa ya hali hiyo na kumvuta mfaransa huyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa France Football, Qatar inajipanga kumnyakuwa kocha huyo kwaajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 ambayo itafanyika nchini humo.

Habari za maslahi ya Qatar hutoka kwa Soka la Ufaransa, ambao wanasema kuwa Qatar ni nia ya kurekebisha timu yao ya kitaifa ya kuweka mbele ya Kombe la Dunia ya 2022.

Kocha huyo alinukuliwa miezi kadhaa iliyopita, akisema kuwa anatamani kurejea katika kazi yake mapema mwaka huu 2019 baada ya kuwa amepumzika kwa kipindi cha kutosha.

Arsene Wenger (69) alihudumu miaka 22 na klabu ya Arsenal, akiiongoza klabu hiyo kushinda mataji matatu ya EPL na mataji saba ya FA.
Share:

MANJI KURUDI KIVINGINE YANGA

Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa klabu ya Yanga, Dr. Jonas Tiboroa amejinasibu kurejesha mfumo wa zamani wa klabu hiyo ambao utaruhusu klabu kuwa na kampuni mbili za kibiashara.


Katika muendelzo wa kampeni zake kuelekea uchaguzi huo, Dr. Tiboroa amesisitiza kuwa klabu ya Yanga itaendelea kuwa ya wanachama huku kukiwa na kampuni mbili, kampuni moja itakuwa inahusika katika uwekezaji na nyingine ambayo itahusika na biashara za klabu.

"Mimi nilipokuwa Katibu Mkuu chini ya Manji tulisema tutahakikisha kuwa Yanga inakuwa klabu ya wanachama na tukaanzisha kampuni mbili, moja inayoshughulikia uwekezaji na nyingine inayoshughulikia biashara za klabu", Alisema Dr. Tiboroa

"Hizi kampunni tulizisajili mwaka 2015, lakini kwa bahati mbaya kizo kampuni zote hazijafanya kazi mpaka sasa, ndiyo maana mimi nimeona kuna haja ya kurudi nikaendeleze yale niliyoyaanza", aliongeza Dr. Tiboroa.

Endapo Dr. Tiboroa atachaguliwa na mpango huo kukamilika, maana yake wawekezaji kama Yusuph Manji na wengine wanaweza kupata nafasi ya nafasi ya kuwekeza katika klabu hiyo bila kuathiri mfumo wake wa uanachama kwakuwa shughuli zote zitaratibiwa chini ya kampuni ya uwekezaji ya klabu.

Uchaguzi wa Yanga unatarajia kufanyika Januari 13, 2019 kwenye ukumbi wa bwalo la maafisa wa polisi Oysterbay Dar es salaa, ambapo nafasi ya Uenyekiti wa klabu inashindaniwa na wagombea wawili, Dr. Jonas Tiboroa na Baraka Igangula.

Chanzo:Eatv
Share:

SAMAKI AUA MTU


Katika mji wa Brooklyn nchini Marekani, kumekumbwa na mkasa wa mama anayedaiwa kupika samaki na harufu iliyotoka, imemuua mwanawe mdogo.

Hadi sasa suala hilo liko katika uchunguzi mikononi mwa mamlaka za kiserikali kupata ukweli wa kifo hicho, kilichoanzia kwa mtoto mhusika mwenye miaka 11 kuugua ghafla, kulegea kwa muda na kupoteza fahamu.

Mtoto Cameron Jean-Pierre, anadaiwa alikuwa na historia ya aleji ya samaki na katika siku ya Mwaka Mpya wiki moja na nusu iliyopita, mama yake alikuwa anaandaa mapishi, harufu ilimfikia mtoto aliyeanguka na kuzimia, mahali hapo anakoishi bibi yake.

Hadi sasa wachunguzi wa kitabibu hawajatoa ufafanuzi kuhusu kilichojiri katika afya ya mtoto huyo ambaye ameshafariki, ingawaje wanafamilia wanakazania chanzo cha kifo hicho ni maradhi ya pumu.

Mama wa mtoto huyo, Jody Pottingr, anasimulia kwamba mwanawe alianza kuugua nyumbani kwa bibi yake, pale binafsi alikuwa alikaanga aina ya samaki hao wa asili.

Mzazi huyo anahisi samaki huyo aliguswa na kitu ambacho kina mtazamo wa sumu kwa samaki wake na ndicho kilicholeta athari inayotajwa na aleji inayotajwa mtoto huyo, iligunduliwa kupitia uchunguzi wa kiafya shuleni, siku moja alivyojisikia vibaya baada ya mlo wa mchana .
Share:

HUYU NDIYE FELIX TSHISEKEDI MSHINDI WA URAIS CONGO

Share:

ANAYEDAIWA KUUA MWALIMU AFIKISHWA MAHAKAMANI


Mtuhumiwa Seif Salimu anayedaiwa kuhusika na mauaji ya mwalimu wa Shule ya Msingi ya Mailisita Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Dinna Lekule, miaka 12 iliyopita amekamatwa na kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Hai.

Mwendesha Mashtaka, Meja Lebulu Mbise aliiambia mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Devota Msofe kuwa mshtakiwa Salimu, maarufu kwa jina la Sharifu, alitenda kosa hilo usiku wa Agosti 21, 2007 nyumbani kwa marehemu Mailisita.

Hata hivyo, mshtakiwa ambaye ni mkazi wa kijiji cha Doma Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, hakutakiwa kujibu lo lote katika kesi hiyo, ambayo aliiahirisha hadi Januari 21, mwaka huu itakapotajwa tena.

Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, mume wa marehemu, Dk Redfan Shao wa Hospitali ya Wilaya ya Hai, alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo.

Alisema kutokana na tukio hilo, alikamatwa na kuwekwa mahabusu kwa miezi 10, akituhumiwa kumuua mkewe.

Alisema, hata hivyo, siku ya tukio hilo alikuwa Handeni katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni kikazi.

Alisema, baada ya tukio hilo alipigiwa simu na kurejea nyumbani Agosti 22 na kujikuta akitiwa mbaroni, akihusishwa na mauaji hayo.

 Dk Shao alisema, baada ya upelelezi Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mahakama, walijiridhisha kuwa hakuhusika na mauaji hayo na kumwachia huru baada ya miezi 10 na sasa anaendelea na kazi katika Hospitali ya Wilaya ya Hai.

Akisimulia kifo cha mkewe, Dk Shao alisema, marehemu alipigwa na kitu chenye ncha kali kichwani, alivunjwa mkono wa kushoto mara mbili na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani.

Alisema, vitu kadhaa viliibiwa katika nyumba yake ikiwamo televisheni moja aina ya Panasonic, redio, vifaa vya kompyuta na pasi ya umeme.

Na Nakajumo James - Habarileo
Share:

SAKATA LA KUDHALILISHA BUNGE : NDUGAI AMPA BARUA YA WITO CAG..MAALIM SEIF NAYE AKOMAA

 Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema ofisi yake tayari imeshaandika barua ya wito kwenda ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ikimtaka kufika mbele ya Kamati ya Maadili, Kinga na Haki ya Bunge ili kuhojiwa.

Hatua hiyo imekuja siku tatu baada ya Spika Ndugai kumtaka CAG, Profesa Mussa Assad kufika mbele ya kamati hiyo kujieleza kuhusu kauli yake kuwa chombo hicho cha kutunga sheria hakitekelezi ipasavyo majukumu yake ya kuisimamia Serikali.

Profesa Assad, ambaye ametakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Januari 21, alitoa kauli hiyo alipohojiwa na idhaa ya Kiswahili ya kituo cha televisheni cha Umoja wa Mataifa (UN), wakati alipokuwa jijini New York, Marekani kuhudhuria mkutano wa jopo la wakaguzi wa nje.

Mbali na CAG, mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee naye ameitwa mbele ya kamati hiyo Januari 22 kwa madai ya kutoa kauli iliyounga mkono kilichosemwa na Profesa Assad.

“Tayari tumeshamwandika barua yaani summons (hati ya wito), maana wito wetu unaenda kama wa kimahakama vile,” alisema Ndugai kwa njia ya simu jana, muda mfupi baada ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa mawaziri wawili na wateule wengine wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wakati Ndugai akisema hayo, katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif amemtaka Ndugai kumuomba radhi Profesa Assad akisema kilichofanywa na CAG ni kutimiza wajibu wake na si kulidhalilisha Bunge.


Na Bakari Kiango, Mwananchi 
Share:

LORI LAGONGA TRENI DODOMA

Na.Alex Sonna,Dodoma
Watu wawili wamenusurika kifo baada ya lori aina ya scania walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kwenda Iringa kuigonga treni ya mizigo katika makutano ya reli na barabara eneo la hazina jijini Dodoma.


Tukio hilo lilitokea jana mchana mara baada ya lori hilo lenye namba za usajili T463 ADW likiwa na tela lenye usajili T483 BLP kuiigonga treni hiyo iliyokuwa ikitoka jijini Dar es salaam kuelekea mikoa ya kanda ya ziwa.


Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa ajali hiyo imechangiwa na mvua zilizokuwa zikinyesha na kumfanya dereva wa lori kutoona kizuizi cha treni mbele yake.


Mmoja wa mashuhuda hao Ramadhani Rashid Mkazi wa Majengo amesema kuwa ajali hiyo ilichangiwa na dereva wa lori kutaka kukatiza kwa mwendo mkali lakini alikuwa kacheleWa hali iliyosababisha kugongwa na treni hiyo ya
mizigo.


“Dereva wa lori alikuwa katika mwendo mkali wakati akikatiza kivuko cha reli hivyo alishindwa kusimama na treni likawa limekaribia na kumgonga tumetoa watu wawili wakiwa wamejeruhiwa vibaya mwingine mmoja utumbo ukiwa nje”alisema


Kaimu kamanda wa polisi mkoani Dodoma ACP William Mkonda, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo ni uzembe wa dereva wa lori ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi na majeruhi wamelazwa katika hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma
Share:

TUME YA UCHAGUZI YAMTANGAZA TSHISEKEDI KUWA MSHINDI WA URAIS CONGO

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Congo (Ceni) imetangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo yanayoonesha mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi ameshinda kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Desemba 30 mwaka uliopita.

Tshisekedi amemshinda mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu, pamoja na mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na serikali ya Rais anayemaliza muda wake, Emmanuel Shadary.


Kwa mujibu wa Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Ceni) Corneille Nangaa, mapema leo Alhamisi amesema kwamba kwamba Bw Tshisekedi amepata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na kumtangaza rasmi kuwa Rais mteule wa nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini na mafuta.


Tshisekedi anatokea katika muungano wa kisiasa na aliyekuwa mgombea wa chama cha UNC (Union for the Congolese Nation), Vital Kamerhe ambaye atakuwa ni Waziri Mkuu wa serikali yao kwa mujibu wa makubaliano yao.


Ripoti zinaeleza kuwa mshindi wa kwanza (Felix Tshisekedi) amepata kura takriban milioni 7, huku mshindi wa pili (Martin Fayulu akipata kura takriban milioni 6.4 milioni na mgombea wa tatu ambaye anaungwa mkono na Rais Joseph Kabila (Emmanuel Ramazani Shadary) akipata takriban kura millioni 4.4.
Share:

Wednesday, 9 January 2019

AZAM FC YATINGA NUSU FAINALI MAPINDUZI..YAITWANGA MALINDI 2 - 1


Azam Fc imefanikiwa kutinga nusu fainali katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Malindi FC mabao 2-1.

Mechi hiyo imepigwa usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Kutokana na ushindi huo Azam FC inatinga nusu fainali na kuikwepa Simba SC.

Mabao ya Azam Fc yamefungwa na Agrey Morris pamoja na
Donald Ngoma huku bao la Malindi FC likifungwa Abdulswamad Kassim
Share:

SIMBA WAONESHA UBISHI

Simba wameonyesha kuwa wao ni wabishi kwenye soka kwa sasa baada ya jana kufanikiwa kuwachapa Mlandege bao 1-0 kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi Kundi A, uliopigwa kwenye Dimba la Amaan.

Simba wamefanikiwa kushinda michezo yao yote ya kundi na hivyo wamemaliza kwa kukusanya pointi tisa kwenye kundi hilo.

Katika mchezo wa jana, Haruna Niyonzima ndiye alikuwa shujaa wa Simba baada ya kuifungia timu hiyo bao pekee kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 20 ya mchezo

Niyonzima alifunga bao hilo baada ya beki wa timu hiyo, Asante Kwasi kuangushwa kwenye eneo la hatari na mwamuzi kuamuru mkwaju wa penalti.

Hata hivyo, kipindi cha pili Mlandege walionekana kuwika zaidi kwenye eneo la kiungo lakini walishindwa kuipenya ngome ya Simba ambayo ilikuwa inaongozwa na Kwasi, Poul Bukaba na Hassan Mlipili ambao walionyesha kiwango cha hali ya juu.

Mbali na Simba timu nyingine ambayo imefuzu kwenda nusu fainali ni KMKM, huku Kundi B, Azam na Malindi nazo zikienda hatua hiyo.

Lakini kuna uwezekano mkubwa Simba ikakutana na kigingi kwenye hatua inayofuata kwa kuwa baada ya mchezo wa jana watabadilisha kikosi na wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza watarejea Dar es Salaam kucheza mchezo wa hatua ya Makundi wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya JS Saoura kwenye Uwanja wa Taifa.

Moja ya timu ambayo Simba wanaomba wasipangwe nayo ni Azam ambayo iliwachapa wapinzani wao Yanga mabao 3-0 kwenye mchezo wa Kundi B.
Share:

YANGA YAMALIZA KOMBE LA MAPINDUZI KWA KUICHAPA JAMHURI 3 - 1

Yanga imemaliza mechi yao ya mwisho ya hatua ya makundi katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kuichapa Jamhuri kwa mabao 3-1.

Mechi hiyo imepigwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, leo na timu zilicheza bila ya presha kubwa.

Yanga iliyoonyesha soka safi ilifanikiwa kushinda kwa mabao hayo ualiyofungwa na Faraji Kilaza, Gustafa Saimon.

Hadi mapumziko, tayari Yanga ilikuwa imepata mabao hayo matatu na Jamhuri moja, na kipindi cha pili kikawa hakina mabao.

Kipindi cha pili kilionekana kuwa cha tahadhari kwa kila timu. Licha ya Jamhuri kutaka kusawazisha mabao hayo mawili lakini ilionekana kujilinda kwa kiasi kikubwa.
Share:

BODI YA FIRAMU YAENDELEA KUMPIGA “PINI” WEMA SEPETU

NA KAROLI VINSENT Katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo amesema msanii wa filamu, Wema Sepetu hajafunguliwa kujihusisha na masuala ya uigizaji kama inavyovumishwa mitandaoni. Bi Fisso ameyasema hayo  leo Jumatano Januari 9 Jijini Dar es Salaam,wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za Bodi hiyo wakati wa kujadili Tasmini ya Tamasha la “KATAA MIHADARATI” lililofanyika katika viwanja vya Mburahati Barafu jijini Dar es Salaam.  Amesema endapo msanii huyo atafunguliwa Baraza hilo litaitisha mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kulieleza jambo hilo na si kama inavyoelezwa…

Source

Share:

WILAYA YA KILOLO KUNG’ARISHWA KWA BARABARA ZA LAMI

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mh. Asia Abdallah amewataka wananchi wa Kilolo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakandarasi ili kufanikisha mradi wa ujenzi wa barabara za lami katika wilaya hiyo unaotokana na juhudi za mbunge wa jimbo la kilolo, Mh. Venance Mwamoto pamoja na serikali ya awamu ya tano utakaondoa changamoto ya usafiri kwa wakina mama wajawazito, wazee na watu wa Kilolo. “kwa hiyo watu watakapo kuja site tuwape ushirikiano wa asilimia 100 barabara itengenezwe na sisi tupate maendeleo kama wenzetu wa kule kaskazini walipofikia, sasa lami inakuja, Mh. Mbunge,…

Source

Share:

CALL FOR STUDENTS TO APPLY FOR HULT PRIZE CHALLENGE UNIVERSITY OF DODOMA 2018-2019

CALL FOR STUDENTS TO APPLY FOR HULT PRIZE CHALLENGE UNIVERSITY OF DODOMA 2018-2019

The University of Dodoma (UDOM) is selected among world’s top Universities to
host local edition of Hult Prize as students answer the United Nations Challenge and
go head-to-head for US$ 1M.

About HULT PRIZE UDOM Challenge
HULT PRIZE UDOM Challenge is a student lead (lead by the official appointed
HULT PRIZE Campus Director) event under the coordination of the UDOM
Innovation Spaces and Incubation Centre (UDOISIC). The HULT PRIZE UDOM
Challenge is a local edition of the world’s largest competition run by HultPrize in
partnership with United Nations, hosting College and University events around the
world in search of the next game changing start up.

About the HultPrize Foundation
Hult Prize is the world’s biggest engine for the launch of for-good, for-profit startups
emerging from University with over 2500 staff and volunteers around the world. In
nearly a decade, the movement has deployed more than $50M of capital into the
sector and mobilized more than one million young people to re-think the future of
business as it continues to breed disruptive innovation on college and University
campuses across 100 plus countries.

The Hult Prize Foundation been called the
“Nobel Prize for Students” and has been featured in a TIME Magazine Cover Story
highlighting the “Top 5 Ideas Changing the World.”
To learn more, visit www.hultprize.org

Objective of the HultPrize UDOM Challenge 2018/19
The Challenge aims at creating the best engine of social entrepreneurs worldwide by
inspiring and motivating youth to engage themselves in social entrepreneurship in
which they can turn social challenges to profitable ventures and be able to earn
income and create jobs for others.
Specifically, this year’s competition aims to have student “create a venture or a
business idea or an idea that can provide 10000 meaningful jobs to youth within
the next decade.
The winner of the intra – campus event will automatically advance to compete in
one of the fifteen regional finals. In our case, the winner will proceed to Nairobi in
April 19th – 20th
. The winning team will then proceed to summer business accelerator
in Ash ridge, United Kingdom in July 2019 for the whole one month and half where
the participants will receive free mentorship, advisory and strategic planning as they
create prototypes and set up to launch their new social business. A final round of
competition will be hosted in New York at United Nation’s headquarters in
September where the winner will be awarded $1,000,000 prize.
“The hultprize is a wonderful example of the creative cooperation needed to build a
world with shared opportunity, shared prosperity, and each year I look forward to
seeing many outstanding ideas the competition produces” (Former US President
Bill Clinton).

HultPrize is now recruiting teams who are interested in registering for the
competition.

Who is Eligible to Apply?
o Must be a team of 3 or 4 students.
o The team must have a name.
o Current student at University of Dodoma (Bachelor, Masters, and PhD).
o UDOM Alumni, Faculty or staff are NOT eligible.

How to Apply?
Applications will be done online by registering your team at
http://bit.ly/2Rf4arc

Application deadline
“It’s not every day that you have an opportunity to change the world. This is your
chance to show the world that you’re dedicated to impact.”
So, make sure you do not miss the application deadline, which is on 15
th January 2019!!!

For more information, contact:
Nominated HultPrize UDOM Campus Director,
Mr. Denice Benedict
+255745356808
+255657933934

For technical support, please contact:
College Innovation Space Coordinators UDOISIC Heads
CBSL: Mr. Mohamed Kaluse (+255717976 265)
E-mail: kaluseone@gmail.com
Dr. Alex F. Mongi
Head, UDOISIC
Technical Support
Phone: +255 755 498 126
E-mail: afmongi@gmail.com
CNMS: Mr. Benatus Mvile (+255 764 860 999)
E-mail: benimvile@yahoo.com
CHSS: Dr. Happyness Nnko (+255 754 816 634)
E-mail: happyjackson.nnko@gmail.com
CIVE: Dr. Mustafa H. Mohsin (+255 676016085)
E-Mail: muky4us@gmail.com
Dr. Lutengano Mwinuka
Head, UDOISIC
Business Support Services
Phone: +255 784 891 291
E-mail:
mwinuka.lutengano@gmail.com
CHS: Dr. David Munisi (+255 762 850 502)
E-mail: massugii@gmail.com
COED: Dr. Pambas Tandika (+255 758 198 170)
E-mail: tpambas@gmail.com
COES: Mr. Desmond Risso (+255 755 870 270)
E-mail: rissodesmond@yahoo.com

The post CALL FOR STUDENTS TO APPLY FOR HULT PRIZE CHALLENGE UNIVERSITY OF DODOMA 2018-2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger