NA KAROLI VINSENT KUMEKUCHA sasa ndivyo unaweza kusema baada ya kuibuka mnyukano mkubwa kati ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Asaad na Spika wa Bunge Job Ndugai ambapo sasa vita hiyo imefika pabaya baada CAG kuibuka na , “kumvua nguo” Spika huyo. Mtifuano huo ulianza kama mdhaha pale Spika Ndugai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma na kumtuhumu kiongozi huyo, kudhalilisha Bunge. Spika Ndugai alikuwa akirejea kauli ya CAG, aliyoitoa nchini Marekani wiki iliyopita, kwamba mhimili huo wa kutunga sheria, umekuwa dhaifu…
Wednesday, 9 January 2019
SHULE YAFUNGULIWA BILA MWANAFUNZI HATA MMOJA KAHAMA
Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako
Tatizo la ucheleweshaji wa fomu kwa wazazi za kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu limechangia idadi kubwa ya wanafunzi kushindwa kuripoti kwa wakati shuleni kujiunga na masomo yao.
Hali hiyo ilielezwa jana na wazazi wa wanafunzi hao akiwemo Diwani wa Kata ya Busoka katika Halmashauri ya Mji wa Kahama, mkoani Shinyanga Julius Malale,ambaye alisema hali ya kuchelewa kupata kwa muda fomu hizo kumechangia wazazi kushindwa kufanya maandalizi mapema ya watoto wao.
Katika Shule ya Sekondari Nyandekwa juzi,ikiwa siku ya kwanza ya kufungua shule hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyeripoti kuanza shule,kitendo ambacho kinaelezwa kuwa cha kwanza shuleni hapo kutokea tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa Kaimu Ofisa Elimu ya Sekondari katika Halmashauri ya Mji wa Kahama,Neema Lema,alisema hadi jana siku ya Jumanne ni wanafunzi watatu tu ndiyo walioripoti katika shule hiyo ya Sekondari Nyandekwa,ingawa alidai tatizo halikuwa lao bali lilikuwa upande wa wazazi.
Neema alisema hali hiyo imejitokeza kutokana na wazazi wa wanafunzi wanaostahili kuanza kidato cha kwanza,kutozifuata mapema fomu hizo kwenye shule za msingi pale watoto wao walikuwa wakisomea.
Alisema ofisi yake ilirahisisha upatikanaji wa fomu hizo kwa kuzipeleka katika shule za msingi walizosomea wanafunzi hao mapema ,lakini wazazi wenyewe wameshindwa kuzichukua kwa wakati ili vijana wao wahudhurie masomo kwa wakati.
Pamoja na hayo baadhi ya wadau wa elimu mjini Kahama,akiwemo Juma Mapolu,walisema ukata mkubwa wa fedha kwa wazazi ni sababu kubwa iliyochangia hali hiyo.
Mapolu alisema pamoja na elimu bure lakini hiyo haisadii sana kwa wazazi kuwakuwa gharama za maandalizi ili mtoto aweze kuanza kidato cha kwanza ni kubwa zaidi ya ada iliyofutwa ambayo ni Shilingi Elfu Ishirini kwa mwaka wakati maandalizi ni zaidi ya laki mbili.
Na Mwandishi wa Malunde1 blog - Kahama
SPIKA NDUGAI AZIDI “POPOLEWA” CAG AIBUKA NA “KUMVUA NGUO”
NA KAROLI VINSENTKUMEKUCHA sasa ndivyo unaweza kusema baada ya kuibuka mnyukano mkubwa kati ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Asaad na Spika wa Bunge Job Ndugai ambapo sasa vita hiyo imefika pabaya baada CAG kuibuka na , “kumvua nguo” Spika huyo. Mtifuano huo ulianza kama mdhaha pale Spika Ndugai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma na kumtuhumu kiongozi huyo, kudhalilisha Bunge. Spika Ndugai alikuwa akirejea kauli ya CAG, aliyoitoa nchini Marekani wiki iliyopita, kwamba mhimili huo wa kutunga sheria, umekuwa dhaifu mno…
BABU WA MIAKA 80 AZIKWA KICHWA CHINI BAADA YA KUKATWA SEHEMU ZA SIRI NA WASIOJULIKANA KAGERA

Picha haihusiani na habari hapa chini
Mzee Laurian Kakoto (80), mkazi wa kijiji cha Ihunga kata Kishanda wilayani Muleba mkoani Kagera amefariki dunia baada ya kukatwa sehemu zake za siri na wahusika kuondoka nazo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa mzee huyo aliondoka nyumbani Januari 7,2018 kwenda kuhemea lakini hakurudi hadi maiti yake ilipogunduliwa na wananchi ikiwa imezikwa huku nyayo za miguu zikiwa zinaonekana juu ya kaburi, Januari 08 saa moja asubuhi.
Kamanda Malimi amesema baada ya wananchi kugundua tukio hilo walitoa taarifa polisi ambao walifika na kufukua mwili huo uliokuwa umezikwa.
“Baada ya mzee huyu kuuawa,wahusika walichimba shimo na kumzika kwa kutanguliza kichwa chini wakabakiza miguu nje, wakati wananchi wakipita waliona nyayo za miguu ya binadamu zikiwa juu ya kaburi baada ya polisi kufika ukafukuliwa na kukutwa amechinjwa shingo na kitu chenye ncha kali huku sehemu zake za siri zikiwa zimekatwa”,amesema.
Amesema tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina kutokana na mwili huo kukutwa sehemu za siri zimekatwa na wahusika kuondoka nazo.
Kamanda huyo alisema kuwa katika eneo la tukio kulikutwa na kiroba kilichokuwa na mchele na kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini waliohusika na unyama huo.
Na Mwandishi wa Malunde1 blog - Kagera
HARAKATI ZA KUMTAFUTA MRITHI WA MANJI YANGA ZAPAMBA MOTO,TIBOROHA AMWAGA AHADI ZAKE HIZI
NA KAROLI VINSENT.KIPENGA kimeshapulizwa cha kuelekea kwenye uchaguzi wa timu ya Yanga unaofanyika jumapili hii ambapo uchaguzi huo unatajwa kumrithi aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo Bilionea Yusuf Manji. Wakati kampeni zikiwa zimeanza ambapo Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, hatimaye leo amezindua rasmi kampeni zake za kuwania nafasi ya mwenyekiti katika klabu hiyo. Katika uzinduzi huo uliyofanyikia makao makuu ya klabu hiyo amewatambulisha baadhi ya wajumbe wanane atakaoambatana nao, ambao ni Ally Msigwa, Christopher Kashililika, Dominic Francis na Salim Rupia. Wengine ni Arfat Hadji, Said Barala na Peter…
MEYA WA MJI NJOMBE AWAPIGA DONGO WAKAZI WA MJINI KWA KUTOA MICHANGO MIDOGO YA UJENZI
Na Amiri kilagalila Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Edwirn mwanzinga amewataka wananchi wanaoishi mjini kuacha tabia ya kukadilia na kutoa michango midogo isiyoweza kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati hususani ujenzi wa madarasa ya shule kutokana na watoto wengi kushindwa kuanza masomo kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa. Akizungumza na mtandao huu ofisini kwake amesema kuwa licha ya halmashauri yake kujitahidi kuwapeleka watoto wote katika shule mbali mbali hususani katika kata za vijijini kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule zilizopo katika kata za mjini,…
TRA Yakusanya Trilioni 7.9 Katika Kipindi Cha Miezi 6 Ya Mwaka Wa Fedha 2018/19
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 7.9 kwa kipindi cha miezi sita ya Mwaka wa Fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia Julai hadi Desemba, 2018 ikilinganishwa na shilingi trilioni 7.8 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Richard Kayombo amesema makusanyo ya mwezi Desemba, 2018 yaliongezeka kuzidi makusanyo ya miezi yote iliyopita kwa mwaka huu ambapo TRA ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.63. “Mbali…
SERIKALI YASHINDA KESI DHIDI YA WANAHARAKATI KUHUSU KANUNI ZA MAUNDHUI MITANDAONI
Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imehukumu kwamba Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo hakukosea wala kukiuka Katiba kwa kutunga Kanuni za Maudhui Mitandaoni za mwaka 2018. Hayo yamejidhihirisha baada ya Mahakama hiyo kusikiliza na hatimaye kuitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu, Bodi ya Wadhamini wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mtandao wa Watetea Haki za Binadamu Tanzania (Human Rights Defenders Coalition) dhidi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Katika shauri hilo walalamikaji wameshindwa kuthibitisha jinsi…
MAANDAMANO YA BARAZA LA VIJANA(BAVICHA)SERENGETI YAZUIWA NA JESHI LA POLISI
Polisi wilayani Serengeti mkoani Mara imezuia maandamano yaliyopangwa kufanyika leo na Baraza la vijana Chadema(BAVICHA) Barua ya kuzuia maandamano hayo imetolewa na Mkuu wa Polisi wilaya ya Serengeti Mathew Mgema na kusema swala la kusitisha kikokotoo lilifanywa na Rais John Magufuli wakati wa hotuba yake iliyofanyika Disemba 28,2018 Polisi wamesema badala ya kufanya maandamano hayo wameshauriwa kuwasiliana na wananchi wake wa Bunda mjini ili kupanga namna ya kumpongeza Bulaya katika eneo lake hilo la uwakilishi Hata hivyo mkuu huyo wa Polisi alisema hatua kali zitachukuliwa Kwa wale wote watakaokiuka na…
PICHA ZA ALIYEPOTEA ZASAMBAA MTANDAONI AKIWA UCHI KAVAA SHANGA
Matukio ya kutoweka kwa wananchi sasa yanazidi kuibuka baada ya kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Michungwani wilayani Handeni kupotea na siku chache baadaye picha zinazomuonyesha akiwa hana nguo na amevaa shanga, zinasambaa katika mitandao ya kijamii.
Kijana huyo Omari Athumani, ambaye ni dereva wa gari la mfanyabiashara aitwaye Ally Matahika, maarufu zaidi kwa jina la Kanto, alitoweka Novemba 14 mwaka jana baada ya kumuaga mama yake kuwa anakwenda kupakia mzigo wa machungwa, na hadi sasa hajaonekana.
Bado sababu za kutoweka kwake hazijajulikana, lakini mkuu wa kituo cha polisi Michungwani, Mgaza Mnkangara amesema kijana huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa tajiri yake anayeitwa Kanto na kusisitiza kwamba “mwanamke anauma”.
Alipoulizwa na Mwananchi kuhusu tuhuma hizo, Kanto alisema anafahamu kuhusu kutoweka kwa Omary lakini amekataa kuzungumzia suala hilo kwa undani.
“Ni kweli,” alijibu Kanto alipoulizwa kama ana taarifa za kupotea kwa kijana huyo, lakini alipoulizwa kuhusu kudhalilishwa kwa kijana huyo na picha zake kusambaa mitandaoni, alikataa kuzungumzia suala hilo.
“Mimi kwa sasa sitaki kuzungumzia suala hilo,” alisema.
Mkuu wa wilaya, kamanda wa polisi wa wilaya na mwenyekiti wa kijiji, wote wana taarifa za kutoweka kwa Omary, lakini wameshindwa kumuhusisha tajiri wake na kitendo cha kutoweka na kudhalilishwa kwa kijana huyo na kwamba uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
Via Mwananchi
MAHAKAMA YATUPA KESI YA KUPINGA MATUMIZI YA KANUNI ZA MAUDHUI YA MTANDAO
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara imetupilia mbali shauri la kupinga matumizi ya kanuni za maudhui ya kimtandao.
Kesi hiyo namba 25 ya mwaka 2018 ilifunguliwa na Baraza la Babari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Muungano wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu wote kwa pamoja wanapinga kanuni za maudhui ya kimtandao.
Katika kesi hiyo washtakiwa ni Waziri wa Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mwanasheria Mkuu.
Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano Januari 9, 2019 na Jaji Wilfread Ndyansobera.
Katika maamuzi yake Jaji Ndyansobera amesema kwamba maombi ya wapeleka maombi hayana uzito.
Akizungumza baada ya maamuzi hayo, Wakili wa Mahakama Kuu upande wa wapeleka maombi, James Marenga amesema wanaheshimu uamuzi wa mahakama kwa niaba ya wateja wake lakini wataangalia nini cha kufanya.
“Tutazungumza na wateja wetu tuone ni namna gani nyingine tunaweza kufanya kama tutakata rufaa basi tutakwenda kwenye mahakama ya juu lakini tunaheshimu mahakama kwa sababu ndio taratibu za kisheria,” amesema Marenga
Kwa kawaida kanuni hizo zilipaswa kuanza kutumika rasmi Mei 5, 2018 lakini Mei 4, 2018 mwaka huu, Mahakama hiyo iliweka zuio la muda baada ya kuwasilishwa kwa shauri la kupinga.
Na Haika Kimaro, Mwananchi
KESI YA KUONGEA HOVYO HOVYO INAYOMKABILI HALIMA MDEE YAPIGWA KALENDA
Kesi inayomkabili, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee anayekabiliwa na shtaka la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kusikilizwa Februari 7, 2019.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita ameeleza hayo leo Jumatano Januari 9, 2019 mbele ya hakimu mkazi mkuu Salum Ally kuwa kesi hiyo ilipaswa kuendelea na ushahidi lakini hakimu husika yuko likizo.
"Kesi imekuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini kutokana na hakimu husika kuwa likizo, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na ushahidi," amedai Wakili Mwita.
Baada ya kueleza hayo Hakimu Ally aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 7, 2019 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kuendelea na hatua ya ushahidi. Tayari mashahidi wawili wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi katika kesi hiyo.
Katika kesi hiyo, Halima anadaiwa kutenda kosa hilo, Julai 4, 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni.
Mdee anadaiwa kumtukana Rais John Magufuli kwa kusema “anaongea hovyo hovyo , anatakiwa afungwe breki” kitendo hicho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
MAMIA YA WATU WAANDAMANA MASHARIKI MWA MJI WA SUDAN

Mashuhuda wanasema kuwa majeshi ya ulinzi yametumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya kundi la watu, ambao walikuwa wakiimbia wakisema Uhuru, Amani na Mapinduzi kwa Sauti ya Wananchi.
Maandamano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Maprpfesa nchini Sudan, ambayo inamtaka Rais Bashir kujiuzulu.
Akizungumza katika kituo cha jeshi katika mji wa Atbara, kiongozi huyo amelaani kile alichokiita usaliti wa kuchoma mali kwa makusudi na kusababisha madhara.
Wakati huo huo Uingereza, Marekani, Canada na Norway zimetoa taarifa ya pamoja, zikisema kwamba zimeshtushwa na taarifa za vifo na kujeruhiwa kwa watu walioshiriki maandamano hayo ya kudai haki zao.
Chanzo:Bbc
KAMBI YA KABILA YAKANUSHA KUHUSU MIKUTANO YA MAKABIDHIANO YA AMANI YA MADARAKA
Timu ya Kampeni ya mgombea urais nchini Congo Felix Tshisekedi, imesema wawakilishi wa kambi yao wamekutakana na kambi ya rais anaemaliza muda wake Joseph Kabila kuhakikisha makabidhiano ya amani ya madaraka.
Kambi ya Kabila hata hivyo imekanusha kuwepo na mikutano kama hiyo tangu kufanyika kwa uchaguzi wa Desemba 30, ambao matokeo yake ya awali yanatarajiwa kutangazwa baadae wiki hii.
Uchaguzi huo ulinuwia kuleta mabadiliko ya kwanza ya kidemokrasia nchini Congo katika kipindi cha miaka 59 ya uhuru wake, lakini wasiwasi unazidi kuenea huku baadhi ya wanasiasa wa upinzani wakiituhumu serikali kwa kujaribi kuiba kura.
Matokeo mengine yanayobishaniwa huenda yakazusha aina ya vurugu zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2006 na 2011 na kuvuruga tena usalama katika maeneo ya mpakani mwa DRC na Uganda, Rwanda na Burundi, ambako dazeni kadhaa za makundi ya wanamgambo zinaendesha shguhuli zake.
Tshikedi aliwania dhidi ya mgombea alieteuliwa na kabila mwenyewe Emmanuel Ramazani Shadary, na kiongozi mwingine wa upinzani Martin Fayulu, ambaye uchunguzi wa maoni ya wapigakura kabla ya uchaguzi ulimuonyesha akiongoza kinyanganyiro hicho.
Chanzo:DW
RAIS MAGUFULI AMPA TANO IGP KUWASWEKA RUMANDE ASKARI,WATUHUMIWA WA DHAHABU
Rais Magufuli amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania-IGP Simon Sirro kwa kuhakikisha watuhumiwa wote wa Dhahabu ya mamilioni ya pesa iliyokuwa inatoroshwa jijini Mwanza wamekamatwa wakiwemo Askari polisi 8.
Rais Magufuli ametoa pongezi hizo Leo Jumatano January 9, 2019 Ikulu Dar es Salaam wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua jana.
Akisimulia kwa kina kuhusu tukio hilo, Rais Magufuli amesema watuhuhiwa hao walikamatwa January 4 Misungwi, kisha wakarudishwa kituo kikuu cha kati, lakini hawakuwekwa Mahabusu.
"Ile dhahabu, Watuhumiwa wale walishikwa tarehe 4, wakarudishwa Mjini Mwanza na Kikosi cha Polisi nane, wakawapeleka Central wala hawakuwaingiza ndani wakawa wanajadili namna ya kuwapa hela, wakawaambia watawapa Bilioni 1. ",amesema Rais Magufuli.
Amesema, watuhumiwa hao walitoa Rushwa ya milioni 700, ikawa imebaki milioni 300 ambayo polisi hao waliahidiwa kwamba watapewa wakifika Sengerema.
Rais Magufuli ameendelea kusimulia kuwa, usiku huo watuhumiwa waliondolewa Central huku wakisindikizwa na Polisi hao kuelekea Sengerema.
Amesema taarifa za kiintelijensia zikawa zimemfikia, akatoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwamba watu hao wafuatiliwe haraka na wakamatwe.
Rais amesema, Polisi toka Sengerema waliweka kizuizi na kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao pamoja na Polisi waliokuwa wakiwasindikiza. Polisi hao walinyang'anywa silaha zao, wakapigwa pingu na wako mahabusu.
YANGA KUFUNGA KAMBI YA MAPINDUZI LEO NA KUPANDA BOTI

Wachezaji wa Yanga.
Klabu ya Yanga inatarajia kucheza mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Mapinduzi 2019, leo Jumatano dhidi ya Jamhuri ya kisiwani Pemba.
Katika mchezo huo, Yanga itakamilisha ratiba tu na kisha kupanda boti tayari kwa kurejea Jijini Dar es salaam kutokana na kutofuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Yanga ni ya pili toka mkiani katika kundi A kwa pointi zake tatu, ikishindwa kufanya vizuri katika mechi zake tatu za awali, baada ya kushinda mechi moja pekee na kufungwa mechi mbili.
Katika kundi hilo, Azam inaongoza ikiwa na pointi saba sawa na Malindi ambazo zote zimefuzu hatua ya nusu fainali. Jamhuri ina pointi nne, Yanga ina pointi tatu na KVZ inaburuza mkia na pointi moja.
Michuano hiyo ambayo ilianza Januari Mosi mwaka huu, inazishirikisha timu tisa, tatu za Tanzania Bara na sita za Zanzibar na itahitimishwa Januari 13.
Chanzo:Eatv
RAIS MAGUFULI AMPOTEZEA SPIKA NDUGAI OMBI LA MAWAZIRI KUCHOKA WAPEWE LIKIZO
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewaombea likizo mawaziri na manaibu waziri kwa Rais John Magufuli.
Spika Ndugai ametoa maombi hayo kwa Rais Magufuli wakati akitoa salamu katika hafla ya uapisho wa viongozi wa serikali iliyofanyika leo tarehe 9 Januari 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
“Nikiwaangalia mawaziri nawaona mmechoka hivi mnakwenda likizo kweli?, ninawaombea kwa rais likizo hata ya mara moja kwa mwezi,” amesema na kuongeza Spika Ndugai.
“Mawaziri wetu wamekuwa wakifanya kazi kubwa, namalizia kwa kuwahakikishia ushirikiano, bunge letu litakuwa pamoja nanyi na kama mtahitaji msaada wetu kwa jambo lolote lile wakati wowote ofisi ziko wazi.”
Katika hatua nyingine, Spika Ndugai amewapongeza viongozi walioapishwa leo na kuwapa pole kutokana na kasi ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano huku akiwataka kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi hiyo.
Akijibu maombi ya Spika Ndugai, Rais Magufuli amesema mawaziri hawana likizo kwa kuwa wananchi wanaowaongoza hawana likizo, na kuwataka kukubali kuteseka katika kipindi hiki cha miaka mitano ya awamu ya kwanza ya uongozi wake ili kuwaletea maendeleo watanzania.
“Kwa makatibu wakuu na wizara, najua mna majukumu makubwa ndio maana mheshimiwa spika anazungumza hamjachukua likizo lakini na mimi sijachukua likizo, wananchi unaowaongoza hawana likizo watanzania hawa wote milioni 55 hawana likizo katika shughuli zao kwa hiyo wakati mwingine inakuwa vigumu kuchukua likizo sababu tunaowaongoza hawana likizo,” amesema na kuongeza Rais Magufuli.
“Leo sijalala nilikuwa nazungumza na waliokwenda kuchukua ndege ya ‘Air Bus’, kujua kama wamechukua spea na kui ‘test’ ndege (kuijaribu ndege), wakaniambia tumekaa angani masaa manne ndege inazunguka, kwa hiyo tukichukua likizo, angalau hii miaka mitano tuteseke kuwatumikia watanzania.”







