Polisi wilayani Serengeti mkoani Mara imezuia maandamano yaliyopangwa kufanyika leo na Baraza la vijana Chadema(BAVICHA) Barua ya kuzuia maandamano hayo imetolewa na Mkuu wa Polisi wilaya ya Serengeti Mathew Mgema na kusema swala la kusitisha kikokotoo lilifanywa na Rais John Magufuli wakati wa hotuba yake iliyofanyika Disemba 28,2018 Polisi wamesema badala ya kufanya maandamano hayo wameshauriwa kuwasiliana na wananchi wake wa Bunda mjini ili kupanga namna ya kumpongeza Bulaya katika eneo lake hilo la uwakilishi Hata hivyo mkuu huyo wa Polisi alisema hatua kali zitachukuliwa Kwa wale wote watakaokiuka na…
Wednesday, 9 January 2019
PICHA ZA ALIYEPOTEA ZASAMBAA MTANDAONI AKIWA UCHI KAVAA SHANGA
Matukio ya kutoweka kwa wananchi sasa yanazidi kuibuka baada ya kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Michungwani wilayani Handeni kupotea na siku chache baadaye picha zinazomuonyesha akiwa hana nguo na amevaa shanga, zinasambaa katika mitandao ya kijamii.
Kijana huyo Omari Athumani, ambaye ni dereva wa gari la mfanyabiashara aitwaye Ally Matahika, maarufu zaidi kwa jina la Kanto, alitoweka Novemba 14 mwaka jana baada ya kumuaga mama yake kuwa anakwenda kupakia mzigo wa machungwa, na hadi sasa hajaonekana.
Bado sababu za kutoweka kwake hazijajulikana, lakini mkuu wa kituo cha polisi Michungwani, Mgaza Mnkangara amesema kijana huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa tajiri yake anayeitwa Kanto na kusisitiza kwamba “mwanamke anauma”.
Alipoulizwa na Mwananchi kuhusu tuhuma hizo, Kanto alisema anafahamu kuhusu kutoweka kwa Omary lakini amekataa kuzungumzia suala hilo kwa undani.
“Ni kweli,” alijibu Kanto alipoulizwa kama ana taarifa za kupotea kwa kijana huyo, lakini alipoulizwa kuhusu kudhalilishwa kwa kijana huyo na picha zake kusambaa mitandaoni, alikataa kuzungumzia suala hilo.
“Mimi kwa sasa sitaki kuzungumzia suala hilo,” alisema.
Mkuu wa wilaya, kamanda wa polisi wa wilaya na mwenyekiti wa kijiji, wote wana taarifa za kutoweka kwa Omary, lakini wameshindwa kumuhusisha tajiri wake na kitendo cha kutoweka na kudhalilishwa kwa kijana huyo na kwamba uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
Via Mwananchi
MAHAKAMA YATUPA KESI YA KUPINGA MATUMIZI YA KANUNI ZA MAUDHUI YA MTANDAO
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara imetupilia mbali shauri la kupinga matumizi ya kanuni za maudhui ya kimtandao.
Kesi hiyo namba 25 ya mwaka 2018 ilifunguliwa na Baraza la Babari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Muungano wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu wote kwa pamoja wanapinga kanuni za maudhui ya kimtandao.
Katika kesi hiyo washtakiwa ni Waziri wa Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mwanasheria Mkuu.
Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano Januari 9, 2019 na Jaji Wilfread Ndyansobera.
Katika maamuzi yake Jaji Ndyansobera amesema kwamba maombi ya wapeleka maombi hayana uzito.
Akizungumza baada ya maamuzi hayo, Wakili wa Mahakama Kuu upande wa wapeleka maombi, James Marenga amesema wanaheshimu uamuzi wa mahakama kwa niaba ya wateja wake lakini wataangalia nini cha kufanya.
“Tutazungumza na wateja wetu tuone ni namna gani nyingine tunaweza kufanya kama tutakata rufaa basi tutakwenda kwenye mahakama ya juu lakini tunaheshimu mahakama kwa sababu ndio taratibu za kisheria,” amesema Marenga
Kwa kawaida kanuni hizo zilipaswa kuanza kutumika rasmi Mei 5, 2018 lakini Mei 4, 2018 mwaka huu, Mahakama hiyo iliweka zuio la muda baada ya kuwasilishwa kwa shauri la kupinga.
Na Haika Kimaro, Mwananchi
KESI YA KUONGEA HOVYO HOVYO INAYOMKABILI HALIMA MDEE YAPIGWA KALENDA
Kesi inayomkabili, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee anayekabiliwa na shtaka la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kusikilizwa Februari 7, 2019.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita ameeleza hayo leo Jumatano Januari 9, 2019 mbele ya hakimu mkazi mkuu Salum Ally kuwa kesi hiyo ilipaswa kuendelea na ushahidi lakini hakimu husika yuko likizo.
"Kesi imekuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini kutokana na hakimu husika kuwa likizo, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na ushahidi," amedai Wakili Mwita.
Baada ya kueleza hayo Hakimu Ally aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 7, 2019 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kuendelea na hatua ya ushahidi. Tayari mashahidi wawili wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi katika kesi hiyo.
Katika kesi hiyo, Halima anadaiwa kutenda kosa hilo, Julai 4, 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni.
Mdee anadaiwa kumtukana Rais John Magufuli kwa kusema “anaongea hovyo hovyo , anatakiwa afungwe breki” kitendo hicho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
MAMIA YA WATU WAANDAMANA MASHARIKI MWA MJI WA SUDAN
Mashuhuda wanasema kuwa majeshi ya ulinzi yametumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya kundi la watu, ambao walikuwa wakiimbia wakisema Uhuru, Amani na Mapinduzi kwa Sauti ya Wananchi.
Maandamano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Maprpfesa nchini Sudan, ambayo inamtaka Rais Bashir kujiuzulu.
Akizungumza katika kituo cha jeshi katika mji wa Atbara, kiongozi huyo amelaani kile alichokiita usaliti wa kuchoma mali kwa makusudi na kusababisha madhara.
Wakati huo huo Uingereza, Marekani, Canada na Norway zimetoa taarifa ya pamoja, zikisema kwamba zimeshtushwa na taarifa za vifo na kujeruhiwa kwa watu walioshiriki maandamano hayo ya kudai haki zao.
Chanzo:Bbc
KAMBI YA KABILA YAKANUSHA KUHUSU MIKUTANO YA MAKABIDHIANO YA AMANI YA MADARAKA
Timu ya Kampeni ya mgombea urais nchini Congo Felix Tshisekedi, imesema wawakilishi wa kambi yao wamekutakana na kambi ya rais anaemaliza muda wake Joseph Kabila kuhakikisha makabidhiano ya amani ya madaraka.
Kambi ya Kabila hata hivyo imekanusha kuwepo na mikutano kama hiyo tangu kufanyika kwa uchaguzi wa Desemba 30, ambao matokeo yake ya awali yanatarajiwa kutangazwa baadae wiki hii.
Uchaguzi huo ulinuwia kuleta mabadiliko ya kwanza ya kidemokrasia nchini Congo katika kipindi cha miaka 59 ya uhuru wake, lakini wasiwasi unazidi kuenea huku baadhi ya wanasiasa wa upinzani wakiituhumu serikali kwa kujaribi kuiba kura.
Matokeo mengine yanayobishaniwa huenda yakazusha aina ya vurugu zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2006 na 2011 na kuvuruga tena usalama katika maeneo ya mpakani mwa DRC na Uganda, Rwanda na Burundi, ambako dazeni kadhaa za makundi ya wanamgambo zinaendesha shguhuli zake.
Tshikedi aliwania dhidi ya mgombea alieteuliwa na kabila mwenyewe Emmanuel Ramazani Shadary, na kiongozi mwingine wa upinzani Martin Fayulu, ambaye uchunguzi wa maoni ya wapigakura kabla ya uchaguzi ulimuonyesha akiongoza kinyanganyiro hicho.
Chanzo:DW
RAIS MAGUFULI AMPA TANO IGP KUWASWEKA RUMANDE ASKARI,WATUHUMIWA WA DHAHABU
Rais Magufuli amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania-IGP Simon Sirro kwa kuhakikisha watuhumiwa wote wa Dhahabu ya mamilioni ya pesa iliyokuwa inatoroshwa jijini Mwanza wamekamatwa wakiwemo Askari polisi 8.
Rais Magufuli ametoa pongezi hizo Leo Jumatano January 9, 2019 Ikulu Dar es Salaam wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua jana.
Akisimulia kwa kina kuhusu tukio hilo, Rais Magufuli amesema watuhuhiwa hao walikamatwa January 4 Misungwi, kisha wakarudishwa kituo kikuu cha kati, lakini hawakuwekwa Mahabusu.
"Ile dhahabu, Watuhumiwa wale walishikwa tarehe 4, wakarudishwa Mjini Mwanza na Kikosi cha Polisi nane, wakawapeleka Central wala hawakuwaingiza ndani wakawa wanajadili namna ya kuwapa hela, wakawaambia watawapa Bilioni 1. ",amesema Rais Magufuli.
Amesema, watuhumiwa hao walitoa Rushwa ya milioni 700, ikawa imebaki milioni 300 ambayo polisi hao waliahidiwa kwamba watapewa wakifika Sengerema.
Rais Magufuli ameendelea kusimulia kuwa, usiku huo watuhumiwa waliondolewa Central huku wakisindikizwa na Polisi hao kuelekea Sengerema.
Amesema taarifa za kiintelijensia zikawa zimemfikia, akatoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwamba watu hao wafuatiliwe haraka na wakamatwe.
Rais amesema, Polisi toka Sengerema waliweka kizuizi na kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao pamoja na Polisi waliokuwa wakiwasindikiza. Polisi hao walinyang'anywa silaha zao, wakapigwa pingu na wako mahabusu.
YANGA KUFUNGA KAMBI YA MAPINDUZI LEO NA KUPANDA BOTI
Wachezaji wa Yanga.
Klabu ya Yanga inatarajia kucheza mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Mapinduzi 2019, leo Jumatano dhidi ya Jamhuri ya kisiwani Pemba.
Katika mchezo huo, Yanga itakamilisha ratiba tu na kisha kupanda boti tayari kwa kurejea Jijini Dar es salaam kutokana na kutofuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Yanga ni ya pili toka mkiani katika kundi A kwa pointi zake tatu, ikishindwa kufanya vizuri katika mechi zake tatu za awali, baada ya kushinda mechi moja pekee na kufungwa mechi mbili.
Katika kundi hilo, Azam inaongoza ikiwa na pointi saba sawa na Malindi ambazo zote zimefuzu hatua ya nusu fainali. Jamhuri ina pointi nne, Yanga ina pointi tatu na KVZ inaburuza mkia na pointi moja.
Michuano hiyo ambayo ilianza Januari Mosi mwaka huu, inazishirikisha timu tisa, tatu za Tanzania Bara na sita za Zanzibar na itahitimishwa Januari 13.
Chanzo:Eatv
RAIS MAGUFULI AMPOTEZEA SPIKA NDUGAI OMBI LA MAWAZIRI KUCHOKA WAPEWE LIKIZO
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewaombea likizo mawaziri na manaibu waziri kwa Rais John Magufuli.
Spika Ndugai ametoa maombi hayo kwa Rais Magufuli wakati akitoa salamu katika hafla ya uapisho wa viongozi wa serikali iliyofanyika leo tarehe 9 Januari 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
“Nikiwaangalia mawaziri nawaona mmechoka hivi mnakwenda likizo kweli?, ninawaombea kwa rais likizo hata ya mara moja kwa mwezi,” amesema na kuongeza Spika Ndugai.
“Mawaziri wetu wamekuwa wakifanya kazi kubwa, namalizia kwa kuwahakikishia ushirikiano, bunge letu litakuwa pamoja nanyi na kama mtahitaji msaada wetu kwa jambo lolote lile wakati wowote ofisi ziko wazi.”
Katika hatua nyingine, Spika Ndugai amewapongeza viongozi walioapishwa leo na kuwapa pole kutokana na kasi ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano huku akiwataka kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi hiyo.
Akijibu maombi ya Spika Ndugai, Rais Magufuli amesema mawaziri hawana likizo kwa kuwa wananchi wanaowaongoza hawana likizo, na kuwataka kukubali kuteseka katika kipindi hiki cha miaka mitano ya awamu ya kwanza ya uongozi wake ili kuwaletea maendeleo watanzania.
“Kwa makatibu wakuu na wizara, najua mna majukumu makubwa ndio maana mheshimiwa spika anazungumza hamjachukua likizo lakini na mimi sijachukua likizo, wananchi unaowaongoza hawana likizo watanzania hawa wote milioni 55 hawana likizo katika shughuli zao kwa hiyo wakati mwingine inakuwa vigumu kuchukua likizo sababu tunaowaongoza hawana likizo,” amesema na kuongeza Rais Magufuli.
“Leo sijalala nilikuwa nazungumza na waliokwenda kuchukua ndege ya ‘Air Bus’, kujua kama wamechukua spea na kui ‘test’ ndege (kuijaribu ndege), wakaniambia tumekaa angani masaa manne ndege inazunguka, kwa hiyo tukichukua likizo, angalau hii miaka mitano tuteseke kuwatumikia watanzania.”
POLEPOLE : HAKUNA MWINGINE ATAKAYEPEWA RIDHAA YA KUGOMBEA URAIS CCM ZAIDI YA JPM
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa alichokifanya Rais Magufuli kwa kipindi hiki kifupi alichokaa madarakani, ni dhahiri kuwa hakuna mwingine atakayepewa ridhaa na chama zaidi yake kugombea 2020.
Polepole ametoa kauli hiyo leo katika kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio ambapo amesema CCM haina sababu ya kupitisha mgombea mwingine ikiwa Rais Magufuli amefanya vitu vikubwa na bado uwezo na nguvu ya kulitumikia taifa bado anao.
"Mwaka 2020 hatuna shaka katika nafasi ya Urais mgombea wetu ni Rais Magufuli hatuna wasiwasi kabisa na kiongozi wetu kwa aliyofanya kwa kipindi hiki njia ni nyeupe, lakini hatujakataza wengine kuchukua fomu wao wachukue tu", amesema Polepole.
Akizungumzia kupunguzwa kwa wanachama wanaotakiwa kupiga kura za maoni amesema kuwa, "Sisi hatuukatai ubaya ambao ulikuwepo zamani, tunakiri na kufuta kwa kufanya mema, CCM tuna kadi za kielektroniki hivyo huwezi kupiga kura ya maoni, kama huna kadi ile na sio kwamba tumewapunguza bali ni mabadiliko ya teknolojia hivyo wahakikishe wanakubaliana na mabadiliko na hakuna aliyefukuzwa".
Aidha Polepole amesema kuwa chama chake, hakipokei tena watu wanaotoka upinzani wao wabaki hukohuko usajili umeshafungwa, na kudai kuwa waliobaki hawana vigezo na wajiandae kuachia majimbo 2020.
MO SALAH ATAWAZWA MCHEZAJI BORA WA MWAKA AFRIKA
Mohamed Salah alikabidhiwa tuzo hiyo na rais wa Caf Ahmad Ahmad (kushoto) na rais wa Liberia George Weah (kulia)
Mshambuliaji wa Misri na klabu ya Liverpool ya England Mohamed Salah ndiye Mchezaji Bora wa Mwaka wa Shirikisho la Soka Barani Afrika kwa mwaka 2018 - hii ikiwa ni mara yake ya pili kushinda tuzo hiyo.
Salah, 26, alimshinda mwenzake wa Liverpool Sadio Mane kutoka Senegal na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.
Alikabidhiwa tuzo hiyo katika sherehe iliyofanyika nchini Senegal Jumanne januari 8,2019.
"Nimekuwa na ndoto ya kushinda tuzo hii tangu nilipokuwa mdogo na sasa nimefanya hivyo mara mbili mtawalia," Salah alisema.
Salah amefunga mabao 16 katika mechi 29 alizoichezea Liverpool mashindano yote msimu huu.
Salah, Mane na Aubameyang wamo kwenye Kikosi Bora cha Mwaka Afrika pamoja na beki wa Manchester United Eric Bailly, kiungo wa kati wa Manchester City Riyad Mahrez, kiungo wa kati wa Liverpool Naby Keita na beki wa kushoto wa Tottenham Serge Aurier.
Chanzo:Bbc
KATIBU MKUU WA CCM AMUONYA DIALLO NA MECK SADICK KUENDELEZA MGOGORO
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amemwonya aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mwanza, Said Meck Sadiki kuacha kuendeleza fitina na badala yake ashirikiane na mshindi halali wa kiti hicho, Anthony Diallo kujenga chama.
Onyo hilo alilitoa jana wakati akizungumza na wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, Mkoa wa Mwanza ambacho kiliwahusisha pia watendaji wa serikali ngazi ya mkoa, wilaya na halmashauri kuangalia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi.
Baada ya hotuba yake hiyo, Dk. Bashiru aliwaita Diallo na Sadick mbele ya wanachama na kuwataka kupeana mikono ya heri na kukumbatiana ikiwa ni ishara ya kuondoa tofauti zao na kuwa kitu kimoja ili mkoa uweze kuwa imara na kushinda uchaguzi ujao.
Dk Bashiru alisema, Sadick alifikisha malalamiko ya kumpinga Dk Diallo ambapo kila mmoja alisikilizwa na uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM iliamuru aliyeshinda uchaguzi wa mwaka jana awaongoze.
Alisema viongozi hao walielezwa kuwaunganisha wanachama kukiimarisha chama na kukinadi kwa wananchi wazidi kukiunga mkono lakini Meck Sadiki ameendeleza fitina za chini chini, jambao ambalo ni hatari kwa ustawi wa chama hicho.
Alisema anatambua Meck Sadik na Dk Dialo ni marafiki lakini wanagawanywa na wanachama na makada ambao dhamira yao washindwe kushirikiana na viongozi kusimamia maendeleo ya wananchi, hivyo aliwaonya kwa pamoja kuachana na tofauti hizo.
“Tukiendekeza migogoro na makundi ya watu hatutafika salama maana tutatoa mwanya kwa watu kufanya ubinafsi kwa maslahi yao.
“Kwanza kinachoendelea kati ya Dk Diallo na Sadick ni sawa na kukidhalilisha chama na wananchi, hali ambayo husababisha kukichukia na kukiadhibu kwenye baadhi ya maeneo,” alisisitiza katibu mkuu huyo.
Aidha Dk Bashiru aliwataka viongozi wa chama ngazi ya mkoa na wilaya kutowapokea na kuungana nao kwenye ziara zao mawaziri ambao hawapiti na kujitambulisha kwenye ofisi za chama hicho na pengine hata kuelezwa kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Awali Dk Bashiru alitembelea na kukagua shamba la ekari 29.23 la CCM lililopo Kijiji na Kata ya Katunguru Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza ambapo alipendekeza kijengwe chuo cha uongozi cha chama ili kusaidia kuelimisha viongozi wa CCM wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Kwa upande wake, Dk Diallo alisema kwamba wamepokea kwa mikono miwili ushauri na maelekezo ya katibu mkuu huyo na watayafanyia kazi ili chama kiwe imara.
UPINZANI WAONYA MATOKEO YA UCHAGUZI NCHINI DRC
Mgombea wa urais wa upinzani nchini Congo DRC Martin Fayulu amewaonya maafisa wa uchaguzi dhidi ya ''kuficha ukweli'' huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda baada ya matokeo ya uchaguzi kucheleweshwa.
Bwana Fayulu amesema watu wa Congo tayari wanajua matokeo ya uchaguzi uliyofanyika Desemba 30 kuahirishwa kwa wiki moja.
Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yalitarajiwa kutangazwa siku ya Jumapili ya Januari 6 lakini yakaahirishwa.
Uchaguzi huo ulikuwa wa kumtafuta mrithi wa rais Joseph Kabila, ambaye anaachia madaraka baada ya kuongoza nchi hiyo ya maziwa makuu kwa miaka 18.
Kabila ameahidi kwamba uchaguzi huo ambao ulikuwa umepangwa ufanyike miaka miwili uliyopita utakuwa wa kwanza wa kupokezana madaraka kwa njia ya kidemokrasia nchini DR Congo tangu taifa hilo lilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1960.
Mrithi wake anayempendelea ambaye pia ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Shadary,anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wagombea wa upinzani Martin Fayulu,tajiri mkubwa wa mafuta na Felix Tshisekedi, mwana wa kiume wa kigogo wa upinzani.
Chanzo:Bbc
Good News : Pakua Upya App ya Malunde 1 blog ...Imeboreshwa Kukupa Raha zaidi ...Bonyeza HAPA SASA
Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.
Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.
Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
KUZIONA SIMBA NA JS SOUARA LAKI MOJA
Klabu ya soka ya Simba imetangaza viingilio vya mchezo wao wa klabu bingwa Afrika Jumamosi hii dhidi ya JS Souara kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam.
Simba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara imesema kiingilio cha chini ni shilingi 5,000 huku cha juu kikiwa ni laki moja.
''Viingilio vya mchezo mzunguko ni 5,000 huku VIP B ikiwa ni 10,000 lakini tutakuwa na tiketi za Platinums ambayo ni 100,000 itajumuisha kuchukuliwa na 'Luxury bus' kutoka Serena Hotel na kusindikizwa na polisi, jezi mpya ya Simba, 'Bites na soft drinks' muda wote utakaokuwa uwanjani pamoja na kurejeshwa Serena'', - Manara.
''Tunawasihi sana wanasimba na washabiki wote tujae kama kawaida yetu Jumamosi, na tuje kuhanikiza, tuje tukijua ujaji wetu ndio silaha yetu'', ameongeza Manara.
MAHAKAMA YAAMURU MWILI WA MAREHEMU UFUKULIWE ILI UCHUNGUZWE
Na Stephen Noel Mpwapwa . Mahakama ya Hakimu mkazi wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imeamuru kufukufukuliwa kwa mwili wa marehemu Cosmas Msote aliye fariki miezi mitano ili ufanyiwe uchunguzi wa chanzo cha kifo chake. Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kuwapo na ubishani Kati ya taarifa zilizo andikwa na Mganga wa hospital ya wilaya ya Mpwapwa juu chanzo cha kifo cha bwana Cosmas Msote aliye fariki dunia tarehe 5 October 2018. Kwa mujibu wa Hakimu mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Mpwapwa bwana Pascal Mayumba amesema aliamua kutoa…
HALMASHAURI ZA WILAYA KOTE NCHINI ZIMEAGIZWA KUTENGA FEDHA KUTOKA MAPATO YA NDANI,KWA KUSHIRIKIANA NA WANAINCHI KUJENGA NYUMBA ZA WATUMISHI WA JESHI LA POLISI.
MULEBA, KAGERA. Na Mwandishi wetu. Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola ametoa agizo hilo jana Januari 8,2019 kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika uwanja wa Fatuma Muleba mjini mkoani Kagera na kwamba nyumba hizo zijengwe palipo na kituo cha polisi Lugola amesema askari wanatakiwa kuishi kambini kwenye makazi ya pamoja na kulinda maadiliyao ya kiutendaji wakiwa na familia zao badala ya kuishi mitaani na kukiuka misingi ya utumishi wa Umma na wengine kushawishiwa na rushwa Amesema halmashauri nyingi nchini kwa kutumia kamati za ulinzi na usalama zikijipanga zitaweza kuanzisha maboma…