Friday, 4 January 2019

WANAFUNZI 463 WAKOSA NAFASI KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI NJOMBE,UHABA WA MADARASA WACHANGIA

Na Amiri kilagalila-Njombe Halmashauri ya wilaya ya Njombe imefanikiwa kutafuta muarobaini wa wanafunzi zaidi ya 400 waliokosa nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza kutokana na ukosefu wa vyumba vya madarasa kwa kuchukua hatua za haraka katika ujenzi wa vyumba vilivyokuwa pungufu katika halmashauri hiyo. Kwa mujibu wa afisa elimu taaluma sekondari Christopher haule katika halmashauri hiyo amesema licha ya wanafunzi 1953 kufaulu vyema mtihani wa darasa la saba lakini wanafunzi 1230 ambapo wavulana wakiwa 710 na wasichana 983 pekee huku wanafunzi 463 wakikosa nafasi kutokana na upunfungufu wa vyumba tisa…

Source

Share:

WAWILI WAONGEZEKA KATIKA SHAURI LA JINAI LINALOHUSISHA UPOKAJI NA UBAKAJI SERENGETI

Na,Naomi Milton Serengeti Watu wawili wamefikishwa mbele ya mahakama ya wilaya ya Serengeti kujibu mashtaka yanayowakabili katika shauri la jinai namba 325/2018 ambalo lilikuwa na mshitakiwa mmoja hivyo wameongezwa wawili na kufanya idadi ya washitakiwa katika shauri hilo kufikia watatu Mwendesha mashtaka wa Jamhuri Faru Mayengela mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile alitoa maombi ya kuongeza washitakiwa wawili baada ya mshitakiwa wa kwanza kusomewa mashtaka Disemba 28/2018 Akisoma upya hati ya mashtaka Faru aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Mwita Marwa(24) Chacha Mwita(34) na Moshi Mayenga(42) wakazi wa…

Source

Share:

MENO 10 YA TEMBO NA BUNDUKI YA AINA YA SMG YAWAPELEKA WAWILI JELA MIAKA 25.

  Na, Naomi Milton Serengeti Jummane Azori(43) mkazi wa Songambele Kigoma na Pala Yoram(29) mkazi wa Uvinza Kigoma wamehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kila mmoja katika kesi mbili tofauti moja ni kuhujumu uchumi na ya pili ni kupatikana na silaha ambayo ni Bunduki aina ya SMG. Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile katika mahakama ya wilaya ya Serengeti baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa kwa upande wa mashtaka dhidi ya washtakiwa hao. Kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo mwendesha mashtaka wa Jamhuri Emmanuel…

Source

Share:

WAKILI FATUMA KARUME AWAUMBUA WAKINA MUSIBA NA WENZAKE,

AMEWAUMBUA ndivyo naweza kusema baada ya Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume, kuibuka na kusema hana mpango wowote kwa sasa wa kumiliki kadi ya chama cha siasa nchini badala yake amedai ataendelea kutoa maoni juu ya masuala mbalimbali nchini kupitia taaluma yake ya sheria. Kauli hii ya Wakili Karume inakuja ikiwa ni teyari watu mbali mbali akiwemo Anayejiita Mwanaharakati Mzalendo,Cyprian Musiba kumtuhumu kuwa ni mwanachama wa vyama vya upinzani na anatumiwa kuikwamisha serikali. Wakili huyo anayesifika kwa kutetea haki za binadamu amebainishwa kuwa “sijwahi kumiliki na wala…

Source

Share:

NECTA IMETANGAZA MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA NNE NA KIDATO CHA PILI.

DODOMA. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) leo Ijumaa Januari 4, 2019 limetangaza matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 2018, kueleza kuwa ufaulu umeongezeka ikilinganishwa na matokeo ya 2017. Akizungumza leo mjini Dodoma katibu mtendaji wa baraza hilo, Dk, Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa 1,302,461 wa darasa la nne waliofanya mtihani huo sawa na asilimia 95.58, waliofaulu kwa kupata daraja A, B, C, na D ni 1,213,132 sawa na asilimia 93.16. Amesema wanafunzi 89,093 sawa na asilimia 6.84 wamepata alama…

Source

Share:

MTETEZI HUYU WA HAKI ZA BINADAMU AWACHANA WANAOMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWENYE SAKATA LA WASTAAFU,

NA KAROLI VINSENT WAKATI kukiwa na Maandamano kila mahala  ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa hatua yake kuzuia ukokotoaji mpya kwenye mifuko ya jamii, Maandamazo hayo yamepingwa vikali na Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)Dkt Hellen Kijo Bisimba,ambapo amesema Rais Magufuli hastahili kupewa pongezi kwa madai kuwa yeye na serikali yake ndio chanzo cha Matatizo hayo kwa wafanyakazi. Akizungumza na DarMpya.com Dkt Bisimba amesema hatua ya Rais Magufuli kutoa zuio kwa vikokotoaji huo ni ya kisiasa. “Ujue hapa kuna siasa mtu anatengeneza tatizo halafu anakuja…

Source

Share:

AJIBU KURITHI MIKOBA YA KELVIN YONDANI

  Na. Jovine Sosthenes. Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameamua kumvua kitambaa cha unahodha beki wa timu hiyo, Kelvin Yondani ‘Vidic’ baada ya kutohudhuria mazoezini pasipo kutoa taarifa. Zahera raia wa Congo amemkabidhi kitambaa hicho nyota wake Ibrahim Ajibu kufuatia kitendo cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na Yondani. Beki huyo mwenye historia kubwa na Yanga kutokana na kudumu kwenye kikosi hicho kwa muda mrefu, mwanzoni mwa msimu huu alitangazwa rasmi kuwa nahodha wa timu hiyo akirithi mikoba ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye pia alikuwa akiitumikia nafasi kama hiyo awapo uwanjani. Taarifa…

Source

Share:

MITIHANI KIDATO CHA PILI ILIYOFUTWA KUFANYIKA WIKI IJAYO


Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema mitihani ya kidato cha pili iliyofutwa mwishoni mwa mwaka jana, sasa itafanyika tena wiki ijayo katika shule zote za Unguja na Pemba.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali anayeshughulikia Taaluma, Madina Mjaka Mwinyi alisema mitihani hiyo itafanyika Januari 14 hadi 22 kwa wanafunzi wa shule za Serikali na binafsi.

 Aliwataka walimu wakuu wote kukamilisha maandalizi ya mitihani hiyo ili kuhakikisha hakuna dosari zinazoweza kujitokeza. 

“Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali inatangaza rasmi kwamba mitihani ya kidato cha pili iliyofutwa Desemba 3 mwaka jana itafanyika tena wiki ijayo tarehe 14 hadi 22 nchini kote” alisema.

Akifafanua, alisema mitihani hiyo imetungwa tena baada ya kufanyika kwa udanganyifu mkubwa na kusababisha wizara kufuta mitihani ya awali. Mjaka aliwakumbusha wasimamizi wa mitihani hiyo, kufuata maadili na kanuni za mitihani, ikiwemo kuepuka aina zote za udanganyifu. 

Alisema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali haitasita kumchukulia hatua za kinidhamu mtendaji atakayebainika kujishughulisha na udanganyifu, ikiwemo kumsaidia mwanafunzi kupata majibu ya mitihani.

“Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali inawataka wasimamizi wa mitihani kuhakikisha kwamba wanafuata maadili na kanuni za masharti ya mitihani ikiwemo kuepuka udanganyifu,” alisema. 

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juman (pichani) aliitangaza rasmi kufutwa kwa mitihani ya kidato cha pili, siku moja baada ya wanafunzi kuanza mitihani hiyo kutokana na kuvuja kwa mitihani hiyo na matokeo yake.

SOMA PIA

Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa ya Kidato cha Pili (FTNA) 2018 Na Darasa la nne (SFNA) 2018 yametangazwa..Yaangalie hapa na pia mpangilio wa ufaulu ngazi ya mikoa na halmashauri.

Share:

ZFA YATANGAZA MAPUMZIKO YA LIGI KWA MWEZI MZIMA

Chama cha mpira wa miguu Zanzibar kimetangaza mapumziko ya ligi kupisha mashindano ya Mapinduzi Cup ili yachezwe kwa ufanisi zaidi. Mapumziko hayo ni ya mwezi mzima kuazia 01/01/2019 hadi 05/02/2019 wakati huo wa mapumziko pia ZFA utautumia muda huo kwa mujibu wa kalenda kufanya uhamisho na usajili wa dirisha dogo kuazia 01/01/2019 hadi 25/01/2019 baada ya hapo zfa itaendelea na utaratibu wa kuhakiki na kupitisha uhamisho, usajili na kutoa block ya usajili wa dirisha dogo. Ligi Kuu Zanzibar inakwenda mapumziko huku timu zote zikiwa zimecheza nusu ya mechi zao yaani…

Source

Share:

Breaking : MATOKEO YA MTIHANI KIDATO CHA PILI 2018,DARASA LA NNE 2018, MPANGILIO WA MIKOA,HALMASHAURI KWA UBORA WA UFAULU

Share:

AY KUJA NA KAMPUNI YAKE ALIYOIPA JINA LA MTOTO WAKE WA KWANZA.

Na. Jovine Sosthenes. Msanii wa mziki Bongo, Ambwene Allen Yessayah alimaarufu kama AY , ameonyesha nia ya kutumia jina la mtoto wake wa kwanza katika kutengeneza fedha zaidi kama wanavyofanya wasanii wakubwa na watu maarufu dunia. Msanii AY Ameweka Kwenye Page yake ya Instagram Ujio wa Kampuni ambayo Ameipa Jina la Mtoto wake wa Kwanza Aviel na Kuandika Kuwa Hii Itakuja Hivi Karibuni Ujumbe aliouandika kwenye Ukurasa wake wa Instagram ulikuwa unasema “COMING SOON #AvieSafaris #Safari #Tanzania” Utakumbuka AY na mkewe, Remy walifunga ndoa February 24, 2018 na sherehe hiyo ilifanyika katika…

Source

Share:

BREAKING NEWS:HAYA HAPA MATOKEO KIDATO CHA PILI 2018

Necta imetangaza matokeo kidato cha pili na darasa la nne 2018
Kama kawaida yetu Maswayetu blog ni kukupa kitu roho inapenda

Tunaangalizia matokeo ya form 2 na darasa la 2 kwa gharama ya tshs 3000 tu kwa kila mwanafunzi
Ili uangaliziwe Fanya yafuatayo;
1.Tuma jina la mwanafunzi mf.Jumanne temba ,taja shule,wilaya,na mkoa kwenda no.0621082183
2.weka mbele MF.form 2 au darasa la NNE
3.tuma pesa yako kwenda namba 0768260834
4.utajibiwa ndani ya dk 1 tu
Kuangalia matokeo hayo
Darasa la NNE >>> http://41.59.85.99/results/2018/sfna/sfna.htm
Share:

MTOTO ANAYEDAIWA KUFUNGIWA KABATINI HATOI SAUTI


 Wakati vyombo vya dola vikiendelea na uchunguzi wa hali ya mtoto anayedaiwa kufungiwa kabatini kwa miezi mitano, madaktari wametaja tatizo jingine walilolibaini kwa mtoto huyo kuwa hatoi sauti.

Mtoto huyo aliyelazwa wodi ya watoto wenye utapiamlo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, amegundulika kuwa na tatizo la kutotoa sauti hata anapolia, hivyo kuwafanya madaktari kuanza kutafuta sababu.

Akizungumza na Mwananchi hospitalini hapo jana, Ofisa Muuguzi, Dina Msesa alisema hali ya mtoto huyo inaendelea kuimarika baada ya kumwanzishia lishe ya vyakula vya kuboresha afya yake, lakini tatizo lipo kwenye utoaji wa sauti.

“Mtoto huyu hatoi sauti yoyote wala halii, ila ametulia jambo linalofanya wataalamu waanze kukuna vichwa kutafuta tatizo,” alisema Msesa.

Kuhusu mama wa mtoto huyo ambaye alikuwa mtumishi wa ndani, alisema afya yake imeimarika na mkono uliokuwa umeumia umepona ambapo sasa anaweza kuunyayua tofauti na awali.

Share:

WAZIRI AMPA SIKU 7 MKUU WA UPELELEZI ,SAKATA LA MWANAMKE KUCHOMEWA NYUMBA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ametoa siku saba kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Kagera (RCO), Obassy Nguvillan, kupeleleza upya kesi ya mama aliyechomewa nyumba katika eneo la Kyakailabwa Kata ya Nyanga, Manispaa ya Bukoba.

Lugola alitoa agizo hilo jana kutokana na watuhumiwa kukamatwa kisha kuachiwa na baadaye jalada kufungwa na Mwanasheria wa Serikali.

Kabla ya agizo hilo, mama huyo, Sauda Amir, alilalamika kwa Waziri Lugola katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Uhuru Manispaa ya Bukoba na baadaye RCO alikiri kuwa inawezekana Jeshi la Polisi lilipeleleza kesi hiyo kwa udhaifu.

Lugola alisema kuwa haiwezekani mwanamke huyo achomewe nyumba, watuhumiwa anawafahamu halafu kesi iishe katika mazingira ambayo yana utata na kulazimika kumwita RCO kujibu.

“RCO natoa muda wa wiki moja ufanye kazi hii wewe mwenyewe, uchunguze kesi hii upya na unipe majibu,” alisema.

Akizungumzia tukio hilo, Sauda anayedai alifiwa na mumewe, alisema kuwa nyumba yake ilichomwa moto Juni 11, mwaka jana na kuwa kutokana na tukio hilo, kwa sasa hana mahala pa kuishi.

“Mheshimiwa Waziri, naomba unisaidie suala langu lipatiwe ufumbuzi, nahangaika na watoto, sina pa kuishi, kwa sasa mimi na watoto wangu saba tumepewa hifadhi na mama mmoja katika eneo la Kyakailabwa,” Alisema mama huyo

Share:

MHE. MABULA AFANYA ZIARA KUKAGUA UJENZI WA BARABARA 9 PAMOJA NA UJENZI WA DAMPO ZINAZOGHARIMU BI 15.9

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ameendelea na ziara yake ukaguzi wa miradi ya maendeleo, ambapo amepata fursa kukagua Miradi 10 yenye thamani ya shingi 15,912,434,395.00 iliyochini ya Mpango Kabambe wa uboreshaji Miji na Majiji, Tanzania Strategic Cities Plan inayohusisha kukarabati na ujenzi wa barabara tisa zilizopo Mitaa ya mjini katika Halmashauri ya Jiji Mwanza sanjari na ujenzi wa dampo la Taka. Mhe. Mabula amempongeza Mhe. Dkt. Magufuli kupitia wizara ya Tamisemi Tawala ya Mikoa na Serikali ya Mitaa kwa ushirikiano wake mwema wa wadau wa maendeleo Bank ya…

Source

Share:

SERIKALI KUMTUMIA SAMATTA KUTANGAZA UTALII UBELGIJI,FLAVIANA MATATA ATEULIWA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, amebainisha kwamba ili kukuza utalii tayari ameanza mazungumzo na klabu ya KRC Genk anakocheza mtanzania Mbwana Ally Samatta ili kuweza kutangaza utalii nchini Ubelgiji.

Waziri Kigwangalla amesema kwamba wakati huu wapo kwenye kuandaa mkakati mahsusi, kwa ajili ya kujitangaza kwenye nchi hiyo.

"Tayari pia tumeanza mazungumzo na mcheza soka wa kulipwa, Ndg. Mbwana Samatta, ili tutumie jina lake kufungua soko jipya la Utalii nchini Belgium. Tunaandaa mkakati mahsusi kwa ajili ya kujitangaza kwenye nchi hii"!

Mbali na kuweka mipango juu ya Samatta, Waziri huyo amemuomba Mwanamitindo wa kimataifa, Flaviana Matata kukubali uteuzi wake wa kuwa balozi wa hiari wa Utalii nchini.

"Tunakushukuru na kukupongeza Ndg. Flaviana Matata kwa uzalendo wako. Tutakupa hati ya shukrani na pia tunakupa Safari ya siku 5 kwenye maeneo ya vivutio siku yoyote utakayokuwa tayari. Pia tutaomba ukubali uteuzi wangu wa kuwa Balozi wa hiari wa utalii"

Pamoja na hayo Waziri amesema kwamba tayari amekwisha kamilisha kazi ya kubuni kauli mbiu ya #TanzaniaUnforgettable ambayo itaitambulisha nchi kwenye masoko ya utalii.

Share:

YANGA WAMJIBU MANARA SAKATA LA KULIPA KODI TRA

Klabu ya soka ya Yanga imetoa jibu kwa msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, aliyehoji juu ya utaratibu wa kuchangisha fedha kwa wanachama wake kama ni halali na unakatwa malipo ya kodi kwa serikali.


Kupitia ripoti yake ya michango ya fedha za mashabiki kwa miezi miwili ya Novemba na Desemba Yanga imeweka wazi kuingiza kiasi cha shilingi 5,165,009 kwa mwezi Desemba na 563,737 kwa mwezi Novemba.

Katika ripoti hiyo Yanga imeeleza michango hiyo imefanyika kwa njia ya simu kupitia Selcom Wallet hivyo lazima kodi zote sitahiki zitakuwa zimelipwa.


Manara alihoji juu ya suala hilo hivi karibuni baada ya kusambaa video mtandaoni ikiwaonesha wachezaji wa Yanga wakipewa fedha na mashabiki baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City uliopigwa jijini Mbeya.

Chanzo:Eatv
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger