Wednesday, 2 January 2019
Picha: MAKAMU WA RAIS BUNGE LA AFRIKA AWAPONGEZA WALIOSHIRIKI MICHUANO YA UVCCM CUP SHINYANGA
Chama cha mapinduzi CCM kata ya Kambarage Mjini Shinyanga kimefanya sherehe ya kuzipongeza timu za vijana za mpira wa miguu, zilizoshiriki katika mashindano ya ya Kombe la Vijana (UVCCM CUP) Wilaya ya Shinyanga
Sherehe hiyo imefanyika Jumanne , Januari 1, 2019 katika ukumbi wa Shy Villa uliopo kambarage Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika na Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Mh.Stephen Masele.
Akizungumza wakati wa sherehe hizo Mh. Masele amewapongeza vijana walioshiriki katika michuano ya kombe la Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) huku akiwataka kuongeza bidii zaidi katika soka ili waweze kuonekana na vilabu vikubwa .
‘Endeleeni kushirikiana maana mpira wa miguu ni kama siasa ni kazi ya kitimu kwenye siasa huwezi fanikiwa peke yako lazima uende na wenzako, kwa hiyo mkijitahidi hata timu yetu ya stand lazima iweke jicho lake kuangalia wachezaji wa nyumbani’alisema Masele.
Katika hatua nyingine Mh. Masele amewakumbusha UVCCM kupuuzia maneno ya watu yenye lengo la kuwakatisha tamaa na badala yake waongeze ushirikaiano zaidi katika kufanya kazi .
‘Msiwe na wasiwasi maneno haya yapo tu siku zote kwa hiyo fanyeni kazi simamie misingi ya chama , ukisikia maneno na ukaendelea kufanya kazi ndio kukomaa huko’ alisema Masele.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kambarage Hasan Mwendapole amesema kuwa lengo la kufanya sherehe hiyo ni kuwakutanisha vijana wote walioshiriki katika mashindano hayo ili kujenga umoja na mshikamano ambao utakuwa chachu ya maendeleo katika wilaya ya Shinyanga.
‘Haya mashindano yamechezwa karibu wiki tatu , kila siku vijana walikuwa wanakutana kwa hiyo unakuwa umewaweka pamoja hata muda wa kutembea hovyo haukuwepo’ alisema Mwendapole
Mashindano ya kombe la umoja wa vijana wa CCM (UVCCM CUP) yalijumuisha kata zote za Wilaya ya Shinyanga na aliyeibuka kidedea ni timu ya Kata ya Kambarage na kukabidhiwa Ngao, cheti pamoja na Ng’ombe.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Abubakary Mkadam (kushoto) akiteta jambo na Mh. Stephen Masele
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Abubakary Mkadam (kushoto) akiteta jambo na Mh. Stephen Masele
Diwani wa Kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akisisitiza jambo wakati wa sherehe hizo ambapo amewataka vijana kuendeleza ushirikiano katika michezo ili kuwa chachu ya mendeleo .
Mwenyekiti wa mashindano hayo BI. Jackline Chacha Amesema lengo la mashindano hayo ni kutekeleza ilani ya chama ,huku akiweka wazi kuwa wameunda timu ya wilaya itakayowahusisha vijana kutoka katika timu zilizoshiriki.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Comrade Egobano akisisitiza jambo katika Sherehe hiyo
Andrew Manyonyi Kampteni wa timu ya Kata ya Kambarage amewaomba wadau wa soka mkoani Shinyanga kujitokeza kusapoti timu za vijana kwani wanakumbana na changamoto mbalimbali hasa upande wa vifaa vya michezo.
Mbunge wa Shinyanga Mjini Mh. Masele akipokea hati ya pongezi kutokana na mchango wake ndani ya Chama CCM Wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geoffrey Mwangulumbi akipokea hati ya pongezi kutoka kwa mgeni rasmi Mh. Masele
Mh. Stephen Masele akimkabidhi Comrade Egobano (kushoto) cheti cha pongezi kutokana na mchango wake kwa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Wilaya ya Shinyanga.
Mh.Stephen Masele akikata Keki katika Sherehe hiyo, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Abubakary Mkadam na kushoto ni Mwenyekiti CCM kata ya Kambarage Rehema Nhamanilo.
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Kambarage wakiwa eneo la Sherehe wakifuatilia yanayojiri.
Wadau wa michezo pamoja na wanachama wa CCM wakifuatilia kwa makini kinachoendelea katika Sherehe hizo.
Sherehe inaendelea
.
Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika na Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa michuano ya UVCCM CUP Wilaya ya Shinyanga timu kutoka Kata ya Kambarage Mjini Shinyanga.
Picha na Steve Kanyefu- Malunde1 blog
MHE. MABULA AKAGUA MIRADI YA MAJI YENYE THAMANI YA BI 46.81
Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula afanya ziara ya kikazi MWAUWASA “Mwanza Urban Water Supply and Sanitation Authority” *Mamlaka ya maji safi na Maji taka Jijini Mwanza* kukagua miradi saba ya maji inayotekelezwa katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza yenye thamani ya shilingi 46,810,000,000.00. Mhe. Mabula akiwa MWAUWASA amepokelewa na mwenyeji wake Kaimu Mkurugenzi Mhandisi. Magayane ambaye alipata fursa ya kutoa taarifa ya miradi yote inayotekelezwa na taasis hiyo matharani iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikiwemo Ujenzi wa Tank la maji Nyegezi pamoja na ulazaji wake wa…
JAMII YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUIBUA MATUKIO YA UKATILI DHIDI YA WATOTO.
Dodoma. Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,imewataka wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia ulinzi wa mtoto ili kutekeleza lengo la la kupunguza matukio ya ukatili kwa silimia 50 ifikapo mwaka 2021!2022. Aidha,wizara hiyo imeitaka jamii kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuepuka kutuma picha za watoto ambao ni wahanga wa ukatili na kuziweka wazi kinyume cha sheria ya mtoto ya mwaka 2009. Taarifa ya wizara imetolewa leo,baada ya kuwepo kwa taarifa mapema wiki hii juu ya mwalimu mmoja wa shule ya msingi jijini Dodoma,kumfungia mtoto…
RAIS AL BASHIR ABANWA VIKALI NA WASUDANI, WAAMUA KUANDAMANA KWA MAMIA MJINI KHARTOUM
Khartoum, SUDAN. Maandamano makubwa yamefanyika mwisho wa mwaka 2018 katika mji mkuu wa Sudan Khartoum yakiitikia wito wa baadhi ya vyama vya upinzani na jumuiya za kiraia kwa ajili ya kulalamikia ughali wa maisha na hali mbaya ya uchumi wa nchi hiyo. Waandamanaji hao walikuwa wakielekea katika Ikulu ya Rais mjini Khartoum wakati walipokabiliwa na vyombo vya usalama vilivyolazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wakipiga kelele dhidi ya serikali ya Rais Omar Hassan al-Bashir. Waandamanaji wengi walikuwa wamebeba mabango na maberamu yenye maandishi yasemayo ‘Irhal’ yaani…
DRC:HUDUMA YA INTANETI NA KUTUMA SMS YAKATWA GHAFLA MPAKA MATOKEO YA UCHAGUZI YATAKAPOTANGAZWA.
Kinshasa, DRC. Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imekata huduma ya intaneti na ujumbe wa mfupi wa simu za mkononi (SMS) kote nchini humo kwa siku ya tatu mfululizo hii leo wakati nchi hiyo ikisubiri kwa hamu kubwa matokeo ya kwanza ya uchaguzi wa Rais. Hali hii imetokea kuanzia juzi Desemba 31 kufuatia uchaguzi wa Rais nchini humo, uliofanyika Jumapili iliyopita, huku baadhi ya mikoa ikigubikwa na ghasia na machafuko. Pande mbili za upinzani na muungano wa chama tawala hapo juzi (Desemba 31) zilieleza kuwa, zinaelekea kuibuka na…
WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUJUMU UCHUMI
Na, Naomi Milton Serengeti Mongatoni Sururu(49) na Mashaka Machemba(33) wakazi wa Kijiji cha Mihale wilayani Bunda Mkoani Mara wamefikishwa mbele ya mahakama ya wilaya ya Serengeti kujibu mashtaka yao katika kesi ya Uhujumu Uchumi namba 1/2019 Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu mkazi Felix Ginene mwendesha mashtaka wa Jamhuri Faru Mayengela alisema washitakiwa hao wanashitakiwa kwa makosa mawili kosa la kwanza ni kuingia ndani ya pori la Akiba kinyume na kifungu 15(1)(2)cha sheria ya wanyamapori namba 5/2009 Kosa la pili ni kupatikana na silaha ndani ya hifadhi kinyume na kifungu 17(1)(2)…
RAIS ESSEBSI ATOA SALAMU ZA MWAKA 2019 KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Tunis, TUNISIA. Rais wa Tunisia, Beji Caid Essebsi, amezungumzia uchaguzi ujao wa rais na bunge nchini humo na kusema kuwa mwaka 2019 utakuwa mwaka muhimu kwa nchi hiyo. katika ujumbe wake mwaka mpya wa 2019, Rais Essebsi ameeleza kuwa jitihada kubwa zinapaswa kufanyika kuandaa mazingira bora ya kufanyika uchaguzi wa wazi, huru na wa kidemokrasia katika mwaka huu wa 2019. Aidha, Kiongozi huyo amewataka wananchi wa nchi hiyo kutumia haki yao ya kikatiba na kushiriki kwenye chaguzi hizo, ambapo amewataka Watunisia kuwachagua watu wanaofaa kwa ajili ya kushika nyadhifa za…
IRENE UWOYA AMWAGA MACHOZI USIKU WA MWAKA MPYA
Rasmi ni mwaka 2019 ikiwa ni siku ya kwanza sehemu mbalimbali ulimwenguni sherehe zinaendelea huku kila mtu akiwa na matumaini yake katika maisha. Kutoka kiwanda cha filamu Bongo wasanii mbalimbali wameupokea mwaka mpya (2019) kwa hisia tofauti tofauti.Wengine wameupokea kawaida huku wengine wakiupokea kwa matumaini mengi wakiamini kwamba inaweza kuwa nafasi ya wao kurekebisha ama kusonga mbele zaidi katika mihanagaiko yao Msanii mrembo na mwenye mvuto wakutosha Irene Uwoya yeye ameupokea kitofauti kabisa mwaka mpya usiku wakuamkia leo.Tofauti na matarajio ya wengi ambao walimuona na kuamini kwamba Irene alikuwa na…
MSIOMBE RUSHWA WANAOTAKA VITAMBULISHO VYA MAGUFULI
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Dk Halfany Haule amewataka watumishi na wenye viti wa serikali za mitaa Manispaa ya Sumbawanga, wajiepushe na visa vya kuomba rushwa wanapopitisha barua za wajasiriamali, wanaoomba vitambulisho maalumu vilivyotolewa na Rais John Magufuli.
Aidha, amewataka wajasiriamali wadogo wakiwemo machinga waliopewa na watakaopewa vitambulisho hivyo maalumu, wasivitumie kama tiketi ya kuvunja sheria na kukiuka maelekezo ya serikali.
Hayo yamebainishwa na Dk Haule wakati wa kuwagawia wajasiriamali wadogo wa manispaa hiyo vitambulisho maalumu.
Alisema miongoni mwa watakaopewa ni machinga na waganga wa tiba asili waliosajiliwa. Wilaya ya Sumbawanga kiutawala ina halmashauri mbili za wilaya ya Sumbawanga na manispaa ya Sumbawanga, ambapo kila moja imepewa vitambulisho 6,250.
“Wenyeviti wa serikali za mitaa msijihusishe kuomba rushwa ili kupitisha barua za wajasiriamali wadogo za utambulisho ambao wana sifa ya kupewa... wanapofika kwenye ofisi hizo wasiombwe rushwa na wapitishiwe barua zao za utambulisho bila kutoa hata senti tano watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kinidhamu na kihalifu,” alionya.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga, Jacob Mtalitinya alitaja sifa za wajasiriamali ambao watapewa vitambulisho hivyo kuwa ni kuwa na mtaji wa biashara usiozidi Sh milioni nne, wasiwe wamesajiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na pia watalipa Sh 20,000, ikiwa ni gharama ya kitambulisho.
“Niwahakikishie kila mwananchi mwenye sifa atapata kitambulisho... nawaasa wawe waaminifu katika kutoa taarifa zao waepuke kudanganya kwa kuwa ni kosa pia,” alibainisha.
Aliwataka wajasiriamali wadogo watakaopewa vitambulisho hivyo, wahakikishe wanavivaa ili wasibughudhiwe.
Petro Makasa ambaye ni baba lishe aliyepatiwa kitambulisho chake, alimshukuru Rais Magufuli kwa nia yake njema kufanya jambo hilo kubwa huku akisisitiza azidi kubarikiwa.
“Niwaombe wajasiriamali wadogo wenye sifa wasipoteze nafasi hii wala wasipuuzie wajitokeze kwa wingi kuviomba,” alieleza Makasa.
Christina Mtawa anayemiliki saluni ya kike alisema, “Hatua hii ya serikali ya awamu ya tano ni ya kupongezwa sana hakika sasa tutapumzika na usumbufu wa maofisa wa TRA,” alisema Makasa.
Peti Siyame, Sumbawanga
Chanzo - Habarileo
CHELSEA YAMSAJILI MSHAMBULIAJI KINDA WA DORTMUND
Klabu ya Chelsea imemsaini mshambuliaji wa Borussia Dortmund Christian Pulisic kwa dau la Yuro 64m lakini itamtoa kwa mkopo kwa klabu hiyo ya Ujerumani hadi mwisho wa msimu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 raia wa Marekani , ambaye alikuwa amehusishwa na vilabu vya Liverpool na Arsenal , alijiunga na Dortumund akiwa mchezaji mchanga 2015.
Pulisic amefunga magoli tisa katika mechi 23 akiichezea Marekani.
''Ilikuwa ndoto ya Christian kujiunga na ligi ya Uingereza'' , alisema mkurugenzi wa klabu ya Dortmund Michaek Zorc.
Hiyo ni kutokana na mizizi yake ya Marekani na kutokana na hilo tulishindwa kuongeza mkataba wake.
''Kutokana na hali hiyo tumekubali ombi zuri la Chelsea''.
Kandarasi ya Pulisic katika klabu ya Dortmund ilitarajiwa kukamilika kufikia 2020.
KATIBU MKUU AWATAKA WATANZANIA KUJIANDAA KUIPOKEA SERIKALI MPYA YA CHADEMA 2020
Katibu Mkuu wa Chama cha Deokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vicent Mashinji amewataka watanzania pamoja na dunia kujiandaa kuipokea serikali mpya chini ya chama anachokiongoza.
Dkt. Mashinji ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter, akisisitiza wananchi kuielewa na kuipokea sera mbadala ya chama hicho.
"Pokeeni Sera Mbadala na jiandaeni kuipokea Serikali mpya inayoongozwa na CHADEMA baada ya October 25, 2020," amesema Dkt. Mashinji.
Aidha kiongozi huyo ametoa ujumbe kwa watu wasiopenda siasa kwa kuwakumbusha kwamba siasa ni utaratibu mzima wa kufanya maaamuzi katika jamii hivyo waipende na wasiichukie.
"Wasiopenda siasa, waambieni hivi “siasa ni utaratibu mzima wa kufanya maamzi katika jamii au kundi fulani la watu ikiwemo familia, na pili, ni matumizi ya mamlaka katika kutekeleza maamzi hayo. Tafadhari Watanzania wenzangu tuipende, tuifanye na tuiishi Siasa" Dkt. Mashinji.
RAIS MAGUFULI AWAUMBUA VIONGOZI WANAOSINGIZIA 'NI MAAGIZO KUTOKA JUU'
Rais John Magufuli juzi usiku alitoa salamu za mwaka mpya wa 2019 kwa kuhoji tabia ya watumishi wa umma kutojiamini katika utendaji wao wa kazi kiasi cha kila jambo wanalolifanya kudai kuwa “ni maagizo kutoka juu”, akisema neno hilo sasa limekuwa kama ugonjwa.
Kauli hiyo ya Rais imekuja kipindi ambacho watendaji mbalimbali serikalini wamekuwa wakitumia neno hilo katika utekelezaji wa majukumu yao, hasa masuala yanayowahusu wananchi.
Akizungumza dakika chache kabla ya kufika saa 6:00 usiku juzi, Rais Magufuli alisema, “Na mara nyingi maagizo yanakuwa hayapo, bali ni utekelezaji wa wajibu wa sheria, wajiamini na wasiwaonee watu lakini watimize wajibu wao.”
Mbali na kuwataka watendaji serikalini kujiamini, Rais Magufuli alisema mwaka huu utakuwa wa mafanikio zaidi kiuchumi na kuwataka Watanzania kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano.
“Ujumbe wangu kwa watumishi wa umma, ni kama nilivyotoa ujumbe kwa Watanzania wengine, wachape kazi, wajiamini,” alisema Rais Magufuli na kuongeza:
“Waachane na utamaduni wa kila kitu wanachokifanya kudai ni maagizo kutoka juu, huo ni ugonjwa ambao umeanza kuwapata watumishi wa umma ambapo kila wanalolifanya hata kama ni kwa mujibu wa sheria hawataki kujiamini, na wanasema hili ni maagizo kutoka juu.”
Via Mwananchi
TETESI ZA SOKA ULAYA , INTER MILAN WAMTAMANI ASHLEY YOUNG
Inter Milan wanamnyatia beki kamili wa Manchester United Ashley Young, 33, na wanatumai kwamba wataweza kumchukua bila kulipa ada yoyote mwisho wa msimu baada ya mkataba wake kumalizika. (Mirror)
Meneja Unai Emery amesema Arsenal bado hawajazungumzia uwezekano wa kumnunua beki wa kati wa Chelsea Gary Cahill, 33, Januari. (Football.London)
Lakini meneja wa Fulham Claudio Ranieri amekuwa wakimtaka Cahill akitumai kumtumia kuimarisha safu yake ya ulinzi Craven Cottage. Anamtaka kwa mkopo wa miezi sita. (The Sun)
Emery amefahamishwa kwamba Arsenal hawataunga mkono mpango wake wa kutaka kuwarejesha Calum Chambers, 23, na Reiss Nelson, 19, mwezi huu. Wawili hao wako nje kwa mkopo. (Metro)Gary Cahill
Chelsea wanakariiba sana kukamilisha usajili wa kiungo wa kati Mmarekani Christian Pulisic, 20, kwa £45m kutoka Borussia Dortmund. (Express)
AUAWA KWA KUKATWA PANGA NA RAFIKI YAKE KISA KAMTANIA KWA KUMUITA 'ALBINO'
Mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya sekondari Naisinyai wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara Godfrey Otieno (16) amefariki dunia kwa kukatwa panga kichwani na rafiki yake baada ya kumtania kwa kumuita albino.
Watoto hao ambao ni marafiki na majirani walikuwa pamoja wakisubiria kushangilia mwaka mpya wa 2019 ambao uligeuka kuwa kilio.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Agostino Senga akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Januari 2, 2019 amesema tukio hilo limetokea Desemba 31, 2018 saa tatu usiku katika kitongoji cha Songambele kata ya Mirerani wilayani Simanjiro.
Amemtaja anayedaiwa kufanya mauaji hayo ni George Damas (15) mwanafunzi aliyemaliza shule ya msingi hivi karibuni na kufaulu, alikuwa akisubiri kupangiwa shule ya sekondari.
Ametaja chanzo cha kifo hicho ni utani kwani Otieno alimtania mwenzake kwa kumwita albino ndipo akakasirika na kuchukua panga na kumkata kichwani.
"Baada ya Otieno kukatwa na panga alikimbizwa kwenye kituo cha afya Mirerani lakini alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu," amesema kamanda Senga.
Amesema wanamshikilia Damas huku wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani.
Na Joseph Lyimo, Mwananchi
RAIS MAGUFULI ASHIKA NAFASI YA PILI ORODHA YA VIONGOZI BORA AFRIKA
Rais John Magufuli ameshika nafasi ya pili kati ya marais watano bora Afrika kwa mwaka 2018 kutokana na kazi aliyoifanya ndani ya miaka mitatu ya utawala wake, jarida la mtandaoni la Africa54 limebainisha.
Jarida hilo lilifanya utafiti wake kwa kuuliza wasomaji wake nani ni Rais bora kwa mwaka wa 2018, kiongozi ambaye hafanani na viongozi wengine wa Afrika; ufanisi wake katika kazi, msimamo, ujasiri na uongozi na matokeo makubwa.
Africa54 limebainisha kwamba, Rais Magufuli amefanya maajabu katika muda wa miaka mitatu ambao amekaa madarakani kuliko kiongozi mwingine. Ameweza kutoa elimu bure, amefufua shirika la ndege na kununua ndege saba, ameanza kujenga reli ya kisasa (SGR) na ameongeza upatikanaji wa huduma za afya. Pia anafahamika kwa kupiga vita rushwa na ufisadi.
Nafasi ya kwanza kwa mujibu wa utafiti huo imechukuliwa na Rais wa Botswana, Ian Khama. Jarida hilo limeandika Rais Khama ni kiongozi mtulivu ambaye ameleta mabadiliko makubwa ya kijamii na kiuchumi ikiwamo kuboresha miundombinu, upatikanaji wa huduma za jamii na upatikanaji wa ajira nchini kwake.
Limesema licha ya kuwa kiongozi huyo amestaafu Aprili mwaka huu, bado Waafrika wengi wanamuona kama kiongozi bora ambaye hana mfano barani Afrika.
Nafasi ya tatu imekwenda kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ambaye aliingia madarakani Aprili mwaka huu inaonyesha kuwa alipendwa ghafla na wananchi wengi nchini humo.
Africa54 limesema kiongozi huyo amefanikiwa kuibadilisha Ethiopia kuwa nchi ya kidemokrasia zaidi na jamii iliyo huru.
Ghulib-Fakim wa Mauritius anachukua nafasi ya nne miongoni mwa marais bora wa Afrika. Jarida hilo linabainisha licha ya kuondolewa madarakani kwa kashfa ya kadi ya malipo, alisimamia haki na maendeleo ya watu katika nchi yake.
Nafasi ya tano inakwenda kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda. Limesema licha ya kiongozi huyo kuminya demokrasia, Waafrika wengi wanampenda kwa sababu amefanikiwa kulibadilisha Taifa lake kuwa kitovu cha uchumi Afrika Mashariki.
ORODHA YA SIMU AMBAZO HAZIKAMATI TENA WHATSAPP, NA ZINAZOKARIBIA KUFUNGIWA
Wamiliki wa simu zinazotumia programu endeshi ya simu aina ya Series 40 wamekuwa hawawezi tena kutumia mtandao wa WhatsApp kwenye simu zao.
Hiyo imetokana na uamuzi wa kampuni ya Facebook inayomiliki mtandao wa kijamii wa WhatsApp wa kuacha kutengeneza app yake kwa njia ambayo inaweza kutumiwa katika simu hizo.
Wengi zaidi wataathirika katika kipindi cha mwaka ujao, 1 Februari, 2020 ambapo simu nyingi zikiwemo baadhi ya iPhone zitapoteza uwezo wa kutumia WhatsApp.
Hata kabla ya wakati huo kufika, Facebook wameonya kwamba "kwa sababu hatutakuwa tukitengeneza na kuboresha app yetu tukizizingatia, huenda baadhi ya uwezo wake ukaathirika wakati wowote."
Zitakazoathirika mwaka ujao ni za Android zinazotumia Android 2.3.7 na miundo ya awali, pamoja na iPhone zinazotumia iPhone iOS 7 kwenda nyuma. Kwa sasa, mfumo wa Android umefikia 9.0. [Unaweza kuangalia mfumo unaotumiwa na simu yako kwenye 'Settings', kisha sehemu ya 'Software/Software Info]
Wanaotumia Android 2.3.7 kwenda nyuma hawawezi kufungua akaunti mpya za WhatsApp.
Ndipo uweze kutumia mtandao huo kwa sasa unahitajika kuwa unatumia Android 2.3.3 kwenda juu na Windows Phone 8.1 kwenda juu.
Kwa sasa, walioathirika zaidi ni wanaotumia baadhi ya simu za Nokia zinazotumia mfumo endeshi wa Series 40 ambao wakati mwingine huitwa S40 OS. Miongoni mwa simu maarufu zilizoathirika ni Nokia 6300.
Simu ya mwisho kutengenezwa ambayo ilikuwa inatumia S40 ilikuwa Nokia 515 ambayo ilizinduliwa mwaka 2013.
Ingawa baadhi ya simu hizi ni za bei nafuu na hutumiwa na watu wa kipato cha wastani au cha chini, kuna wanaotumia simu aina ya pia simu za Vertu Signature S ambazo zilikuwa ghali sana na ambazo hutumia programu hiyo endeshi pia.
Wakati wa kuanza kuuzwa kwa simu hizo zilikuwa zinauzwa takriban £8000 (Tshs23m; Kshs1m), ingawa hiyo ilikuwa miaka kumi iliyopita na huenda wengi wao wamenunua simu nyingine au wana uwezo wa kununua simu nyingine kwa urahisi.
Simu zilizoathirika kwa sasa
- Nokia 206 Single SIM na dual SIM
- Nokia 208
- Nokia 301 Single SIM na dual SIM Chat Edition
- Nokia 515 zinazouzwa zikiwa na WhatsApp
- Nokia Asha 201
- Nokia Asha 205 Chat Edition
- Nokia Asha 210
- Nokia Asha 230 Single SIM na dual SIM
- Nokia Asha 300, 302, 303, 305, 306, 308, 309, 310, 311
- Nokia Asha 500, 501, 502, 503
- Nokia C3-00
- Nokia C3-01
- Nokia X2-00
- Nokia X2-01
- Nokia X3-02
- Nokia X3-02.5
Simu ambazo haziwezi kutumia WhatsApp na tarehe ya kuacha kutumia
- Nokia Symbian S60 baada ya Juni 30, 2017
- BlackBerry OS na BlackBerry 10 baada ya Desemba 31, 2017
- Windows Phone 8.0 na miundo ya awali Desemba 31, 2017
- Nokia S40 baada ya Desemba 31, 2018
- Android 2.3.7 na miundo ya awali baada ya Februari 1, 2020
- iPhone iOS 7 na miundo ya awali baada ya Februari 1, 2020
Simu nyingine zisizotumia WhatsApp
Kufikia Juni mwaka 2017, huduma ya WhatsApp pia ilikuwa imeacha kutumika tena katika aina kadha za simu za zamani zikiwemo zile zilizotumia mfumo wa Windows Phone 7.1, Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6.
Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo ilisema wakati huo kwamba inataka kuangazia kustawisha "huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi."
Kampuni hiyo ilikuwa imeorodhesha simu za BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60 kuwa miongoni mwa simu ambazo zingekatiwa huduma mwishoni mwa mwaka 2016 lakini ikabadilisha uamuzi wake na kuongeza muda hadi Juni 30, 2017.
Simu zilizotumia Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6 hata hivyo zilifungiwa mwishoni mwa 2016.
Hatua hiyo ilikuwa imetangazwa na Facebook mapema mwezi Februari mwaka 2016.
Kampuni hiyo ilijitetea na kusema kwamba haikusudii kuwatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
"Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo," kampuni hiyo ilisema.WhatsApp hutumiwa na watu bilioni moja duniani
Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawawezi kutumia WhatsApp:
- Android 2.1 na Android 2.2
- Windows Phone 7
- iPhone 3GS/iOS 6
- BlackBerry OS and BlackBerry 10
- Nokia S40
- Nokia Symbian S60
Wanaotumia simu zilizofungiwa wameshauriwa kununua simu za kisasa zaidi.
Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia.Simu ya Blackberry
Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.
Chanzo- BBC