Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Saalam iliyo chini ya mheshimiwa Paul
Makonda imeratibu tukio maalum litakalofanyika siku ya tarehe
24-25/09/2015 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja. Ambapo wananchi
watakaojitokeza kwenye tukio hilo maalum watapatiwa matibabu bure.
Taarifa iliyotolewa na mkuu wa mkoa kupitia akaunti yake ya Instagram
imeeleza kwamba wananchi watapata fursa ya kupimwa magonjwa zaidi ya
kumi (10) na kupatiwa matibabu bure.
Hivyo wananchi wote wanaombwa kujitokeza kwa wingi.
Kama kawaida yetu MASWAYETU BLOG
katika nusanusa yetu tumefanikiwa kunasa hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa
na watu wengi,ni kuhusu majina ya wanafunzi waliochaguliwa na TCU
2016/2017 kujiunga vyuo vikuu mbalimbali 2016/2017. wale wote mlioomba vyuo kama,
Tume ya
Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeongeza muda wa udahili wa wanafunzi
wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu mwaka wa masomo 2016/2017 ili kuwapa
fursa waombaji ambao wana sifa lakini hawakupata vyuo kutokana na
ushindani wa vyuo na kozi walizozichagua.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Eleuther Mwageni
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mwenendo mzima wa
udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017, leo Jijini, Dar es Salaam.
“ Tume
imekamilisha awamu ya kwanza ya udahili kwa waombaji wenye sifa ya
kidato cha 6, ambapo jumla ya waombaji wote ilikuwa 55,347, waombaji
wenye sifa ni 47,203 sawa na asilimia 85.3 ya waombaji wote. Katika
waombaji hao wenye sifa waliopata vyuo ni 30,731 sawa na asilimia 65 na
waombaji 16,472 ambao wana sifa sawa na asilimia 35 hawajapata vyuo hadi
sasa, waombaji waliokosa sifa ni 8,144,” alifafanua Prof. Mwageni.
Amesema
kuwa Tume imeamua kuongeza muda wa udahili kuanzia Septemba 12 mpaka
Septemba 23, 2016 ili kuwapa nafasi waombaji wenye sifa, fursa ya kuomba
tena vyuo na kozi zenye nafasi kutokana na wengi wao kuomba vyuo na
kozi za aina moja.
Prof.
Mwageni alivitaja vyuo ambavyo vimeombwa na waombaji wengi na tayari
vimeshajaa kuwa ni Chuo cha Ardhi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo
Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi Shirikishi, Chuo Kikuu cha
Kikristo cha Tiba Kilimanjaro(KCMUCo) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili.
Pia
alizitaja kozi ambazo zimechaguliwa na waombaji wengi kuliko nafasi
zilizopo kuwa ni kozi ya Ualimu, Udaktari wa Binadamu, Ufamasia,
Uhandisi, Sayansi ya Uthamini wa Ardhi na Sheria. Alitoa mfano wa kozi
ya Ualimu Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Dar es Salaam ilikuwa na
waombaji 15,803 wakati nafasi ni 1,000.
Hivyo
amewashauri waombaji waliokosa nafasi kuomba vyuo na kozi zisizo na
ushindani ili waweze kupata nafasi kwa awamu hii ya pili.
Aidha
Tume hiyo imepunguza viwango vya udahili kwa waombaji wenye sifa ya
stashahada kutoka GPA 3.5 mpaka 3.0. Hivyo wamewataka waombaji wenye
vigezo hivyo kuomba vyuo na kwa wale waliomba awamu ya kwanza
hawatatakiwa kuomba tena bali kusubiri matokeo ya waombaji wenye sifa ya
stashahada
Mkutano
wa Nne wa Bunge umemalizika huku ukiacha sintofahamu baada ya Ukawa
kushindwa kukutana na Spika wa Bunge, Job Ndugai kujadili mgogoro kati
yao na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.
Kikao cha Bunge cha Mei, Ukawa walisusia vikao vyote vilivyoongozwa na Naibu Spika wakidai alikuwa akiminya demokrasia.
Hali
hiyo, ilitokea wakati Spika Ndugai alipokuwa nje ya nchi kwa matibabu
na aliporejea aliahidi kufanya maridhiano kati ya Ukawa na Dk Tulia
kwenye Bunge lililomalizika jana.
Jana, Kiongozi wa Kambi ya
Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema maridhiano yaliyokuwa yafanywe
na Ndugai kati ya Ukawa na Dk Tulia hayakufanyika, kwa kuwa aliyeahidi
hakuitisha kikao chochote.
Alisema kurejea kwao bungeni kulitokana na nasaha za viongozi wa dini waliokutana nao kabla ya vikao vya Bunge.
“Tukarudi bungeni na kufanya shughuli zetu katika mazingira hayohayo magumu,”alisema Mbowe.
List of Selected Candidates to Pursue Various Certificate and Diploma Programmes for 2016/2017
The following candidates have been selected to join various
Certificate and Diploma Programmes offered by the Institute of Finance
Management for the 2016/2017 academic year....Read More
WABUNGE wote wa Chama cha Wananchi (CUF) wametangaza rasmi
kutomtambua aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim
Lipumba. Wamemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi
kutomkumbatia mwanasiasa huyo aliyebobea katika uchumi, ikielezwa kwa
sasa hana sifa za kuwa mwenyekiti wa chama hicho, labda aanze upya
mchakato. Wameeleza msimamo huo jana mjini Dodoma na Mbunge wa Viti Maalumu,
Riziki Mngwali ambaye pia ni Kiongozi wa Wabunge wa CUF katika mkutano
baina ya waandishi wa habari za Bunge na wabunge wa CUF isipokuwa Mbunge
wa Jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya aliyesimamishwa uanachama, ingawa
anaendelea kutimiza majukumu yake bungeni. Mngwali alisema Profesa Lipumba amekuwa akijaribu kukiyumbisha chama
na hivi karibuni kudai amekaririwa akisema anasubiri barua ya Msajili wa
Vyama vya Siasa ya kuthibitishiwa kuendelea na uenyekiti wake. “Wakati anajiuzulu uenyekiti Agosti 5, mwaka jana aliutangazia umma
na kudai anakwenda Rwanda kwa kazi aliyodai ya utafiti ili aje kuisaidia
serikali, lakini inashangaza sasa anataka kujirejeshea uenyekiti. Hilo
hatukubali kwa kuwa chama kina taratibu zake,” alisema. Aliongeza kuwa, alikiacha chama katika wakati mgumu kuelekea Uchaguzi
Mkuu, lakini kikaimarika zaidi kwa kupata wabunge 43, madiwani 287,
kuongoza manispaa mbili na halmashauri za wilaya tatu, hivyo
wanashangazwa kuona akitaka kurejea, tena kwa kutumia nguvu. “Tunataka ifahamike kwa dhati kuwa, sisi wabunge, hatumtambui tena
Profesa Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF,” alisema Mngwali na kumtaka
Msajili kutomuidhinisha Lipumba, kitendo alichodai kitachochea mgogoro
ndani ya chama. Aliongeza kuwa badala ya kutumia mabavu kutaka kurejea madarakani, ni
vyema akabaki na heshima yake, kwani amekitendea mambo mengi chama
hicho na kwamba wanamheshimu, hivyo afuate taratibu za kichama kutaka
kuwania tena uenyekiti. Mngwali alisema wamekubaliana na uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi wa
CUF wa kuwasimamisha uanachama Lipumba na wenzake tangu Agosti 28, 2016
kutokana na kile kinachodaiwa kukiuka Katiba ya chama hicho. Miongoni
mwa tuhuma zao ni kusababisha vurugu wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa
Uchaguzi Agosti 21, mwaka huu jijini Dar es Salaam uliokuwa unalenga
kumthibitisha Juma Duni Haji kuwa Mwenyekiti mpya. Hata hivyo, kutokana na vurugu zilizoibuka, mkutano huo ulivunjika.
Mbali ya Lipumba na Sakaya, wengine waliositishiwa uanachama ni Abdul
Kambaya ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho,
Ashura Mustapha, Omar Mhina, Thomas Malima, Kapasha M. Kapasha, Mohamed
Habib Mnyaa, Haroub Shamis na Mussa Haji Kombo. Ashura ni mjumbe wa Baraza Kuu na aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa
Habari na Mawasiliano ya Umma CUF wakati Mnyaa na Kombo, walikuwa
wabunge kipindi cha 2010/2015, Mnyaa akiwakilisha Jimbo la Mkanyageni na
Kombo Jimbo la Chake Chake, kisiwani Pemba. Kutokana na kusimamishwa kwa viongozi hao, Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alimtangaza Julius Mtatiro aliyewahi kuwa
Naibu Katibu Mkuu Bara kuwa kiongozi wa Kamati ya Uongozi wa muda
inayowajumuisha pia wabunge Katani Ahmed Katani na Savelina Mwijage
ambao ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.