Wednesday, 3 August 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Agosti 3

Share:

Tuesday, 2 August 2016

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SUA FIRST BATCH 2016/2017-POSTGRADUATE

Share:

MPYA:ANGALIA HAPA DEADLINE YA KUOMBA VYUO TCU KWA FORM SIX 2016/2017

Share:

MPYA:TAARIFA KWA WANAFUNZI WALIOKUWA WAMECHAGULIWA MSUMBIJI NA KURUDISHWA NYUMBANI,WANATAKIWA KUAPPLY TENA,HAYA HAPA MAJINA YAO

Share:

MPYA:RATIBA MPYA YA RPL EXAM,DEADLINE IMESOGEZWA HADI TAREHE 5 AGUST 2016

Share:

Magazeti Ya Leo Jumanne ya Agosti 2, 2016

1n
Share:

Monday, 1 August 2016

Rais Magufuli akamilisha ziara yake, atoa onyo kwa walimu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe amekamilisha ziara ya siku nne Singida, Tabora, Shinyanga na Geita ambapo amefanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mnadani na kuwajumuisha wananchi wa Katoro na Buseresere mkoani Geita.
akizungumza katika mkutano huo Rais Magufuli amewaagiza viongozi wote kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Kitongoji hapa nchini kufuatilia matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutoa elimu bila malipo kwa lengo la kudhibiti mianya ya matumizi mabaya ya fedha hizo. 
Katika agizo hilo Dkt. Magufuli amewaonya walimu ambao wameanza kufanya udanganyifu kwa kuandikisha idadi kubwa ya wanafunzi kuliko idadi halisi kwa lengo la kupata mgao mkubwa wa fedha za ruzuku na amesema Serikali itachukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kufanya hivyo.
>>>’Ninafahamu mgao wa fedha hizo hutolewa kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo, wapo baadhi ya walimu ambao wameanza kuandika wanafunzi hewa katika shule zao, ili kusudi aletewe hela nyingi kuliko idadi ya wanafunzi waliopo, wanafunzi kama wapo laki nne yeye anasema shule yangu hii ina wanafunzi laki tano, ili kusudi hela zikija za wanafunzi laki tano, za wanafunzi laki moja wagawane’
>>>’Napenda nitoe wito kwa walimu Tanzania nzima, mnatafuta matatizo, narudia mnatafuta matatizo, msijaribu kula hela ya Serikali’
Share:

Video: James Lembeli akizungumza kuhusu hatma yake kurudi CCM


Wakati jana  Rais Magufuli akiwa  wilayani Kahama  mkoani Shinyanga  alimpa nafasi aliyekuwa Mbunge wa Kahama kwa tiketi ya CCM na baadae kuhamia CHADEMA, James Lembeli ili azungumze.
Lembeli aliongea mambo kadhaa ikiwemo hatma yake kurudi CCM ambapo alisema yupo tayari kurudi iwapo Rais Magufuli atakisafisha chama kwa kuwashughulikia wanafiki na wala rushwa
Share:

Rais Magufuli Asema Hatagawa Chakula cha Bure Kwa Watakaopatwa na Janga la Njaa Bila Sababu za Msingi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali yake haitagawa chakula cha bure kwa wananchi wanaopatwa na tatizo la njaa pasipo kuwa na sababu za msingi na badala yake amewataka watanzania wajikite kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ikiwa ni pamoja na kuzalisha chakula cha kutosha.

Rais Magufuli amesema hayo jana tarehe 31 Julai, 2016 wakati akihutubia mikutano ya hadhara na kuzungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake akiwa njiani kutoka Mkoani Tabora kuelekea Shinyanga na baadaye Geita anakoendelea na ziara yake.

Pamoja na kuwahimiza wananchi kuzalisha chakula cha kutosha ili kuondokana na njaa Rais Magufuli alisema serikali yake itajikita kuhakikisha inashughulikia tatizo la uhaba wa maji, ujenzi wa miundombinu hususani barabara na reli, kuimarisha huduma za matibabu, elimu na kutengeneza ajira.

Akiwa Isaka Mkoani Shinyanga Rais Magufuli alisema serikali haitalipa fidia kwa wananchi waliopatwa na maafa ya mafuriko yaliyobomoa nyumba zao mwezi Machi mwaka 2015 na badala yake itajielekeza kutatua tatizo kubwa la uhaba wa maji katika mji huo ambao una makutano ya reli ya kati ya kutoka Dar es Salaam kwenda nchi za Burundi na Rwanda.

Katika Mji wa Kagongwa Rais Magufuli alipokea kilio cha wananchi dhidi ya vitendo vya ujambazi na ametoa siku tano kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha watu wanaojihusisha na ujambazi wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Mjini Kahama, Dkt. Magufuli aliiagiza Wizara ya Nishati na Madini kushirikiana na Mbunge wa Kahama Mhe. Jumanne Kishimba kukokotoa mahesabu vizuri na kubaini kodi ambayo Serikali inastahili kulipwa baada ya Mbunge huyo kudai kuna kiasi kikubwa cha kodi hakijakusanywa kama ambavyo sheria inaelekeza.

Aidha, Rais Magufuli alisema serikali itahakikisha wawekezaji wanaochimba madini wanaacha kusafirisha mchanga wenye madini kwa lengo la kwenda kuchakata nje ya nchi na badala yake ametaka uchakataji huo ufanyike hapa hapa nchini.

Dkt. Magufuli alizungumza na wananchi vijiji vya Segese na Bukoli na kuwahakikishia kuwa Barabara ya Kahama, Segese, Kakola hadi Geita yenye urefu wa kilometa 146 itajengwa kwa kiwango cha lami kama alivyoahidi.

Mjini Geita, Rais Magufuli alipokea kilio cha wananchi wanaodai kuwekewa zuio la kutumia mawe yenye mabaki ya madini ya dhahabu (Magwangala) kwa lengo la kusaga na kuchenjua ili kupata dhahabu, na ametoa wiki tatu kwa Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathimini na kuwaruhusu wachimbaji wadogo kutumia Magwangala.

Rais Magufuli pia ameiagiza Bodi ya Pamba hapa nchini kuhamisha ofisi zake zilizopo Jijini Dar es salaam na kuzileta katika Mikoa ya kanda ya ziwa ambako uzalishaji wa zao la pamba unafanyika.

Dkt. Magufuli amewaonya viongozi na watendaji wa bodi hiyo dhidi ya vitendo vya usambazaji wa mbegu za pamba zisizoota na amesema ikitokea tena watachukuliwa hatua.

Tarehe 01 Agosti, 2016 Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli anatarajia kukamilisha ziara yake ya siku nne katika Mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Geita

31 Julai, 2016
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULY TAREHE 1.8.2016

Share:

Sunday, 31 July 2016

CHUOKIKUU CHA SYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA CHAKANUSHA KUFUNGIWA UDAHILI

Share:

Mkutano wa Rais Magufuli, Kahama: James Lembeli Atangaza kurejea CCM

Katika hali inayoshangaza wapenzi na mashabiki wengi wa CHADEMA ni pale aliyekuwa mgombea Ubunge kupitia CHADEMA ameonekana katika mkutano wa CCM unaoendelea hapa mjini Kahama.

Wadadisi wa masuala ya kisiasa hapa Kahama wanadai kiongozi huyo aliyejizolea umashuhuri mkubwa enzi za uongozi wake kwa sasa mambo yake yamekwenda mrama hivyo njia nyepesi ni yeye kutubu na kurejea nyumbani kwao waliko mababu zake

image.jpeg
 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger