Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu Rasimu ya Katiba ya Fungamano la Kisiasa la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kuongeza uelewa na kuimarisha ushiriki wao katika hatua za kufikia fungamano hilo.
Zoezi hilo lililoendelea leo, Oktoba 27, 2026, limehusisha wawakilishi wa vyama vya siasa, jumuiya za wafanyabiashara, taasisi za dini, mashirika ya kiraia, makundi maalumu ya kijamii yakiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, pamoja na taasisi za utafiti, uchambuzi wa sera na elimu ya juu.
Zoezi hilo lililozinduliwa rasmi Oktoba 26, 2026, linaongozwa na Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama wa Wizara hiyo, Bi. Mwanamridu Amity Jumaa.
Ushirikishwaji wa wadau hao unalenga kuongeza uelewa kuhusu Rasimu ya Katiba ya Fungamano la Kisiasa la EAC na kutoa fursa kwa makundi mbalimbali kufahamu masuala yanayohusu mchakato huo.






0 comments:
Post a Comment