KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
(NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa
mfumo wa Udahili wa pamoja yani OnlineCentral Admission System (CAS), umefunguliwa rasmi tarehe 4 Machi, 2016, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi kwa mwaombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada, Stashahada na Shahada kwa mwaka wa masomo 2016/17. Mfumo utajumuisha kozi zifuatazo;
1. Astashahada na Stashahada
2. Shahada za Elimu ya Juu
Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo;
1. Biashara na Utalii, mfano; Uhasibu, Meneja rasilimali watu, Wanyama pori, Mipango.
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Kafariki jana usiku ikiwa ni masaa machache tu yamebaki Majaliwa amtembelee akiwa ziarani Simiyu.
Sababu kubwa ni pressure ,wakati anakimbizwa bugando akafariki dunia. R I P MKUU ,innocent the blogger boy naheshimu mchango wako ktk wilaya yangu ya MASWA.
MASWAYETU BLOG TEAM TUPO PAMOJA NANYI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dkt.
Carina Wangwe akifafanua jambo kwa wajumbe wa bodi wa shirika hilo
(hawapo pichani ) kabla ya uteuzi huo kutenguliwa.
Masaa
kadhaa baada ya uteuzi huo, Waziri mhagama alitangaza kutengua
uteuzi huo kwa madai kwamba kuna baadhi ya taratibu hazijamilika
Kamishina wa Polisi Operesheni na
Mafunzo, Nsato Marijani akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati
wa mkutano makao makuu Jeshi ya Jeshi la Polisi.
Wanasheria waaswa kutumia taaluma kulinda maslahi waajiri wao
Mkuu wa wilaya ya Nzega Bi. Jackline Liana amewataka Wanasheria
wanapokuwa wakisimamia mashauri mbalimbali kutumia taaluma zao na
kuweka weledi wa kutosha ili kulinda maslahi ya waajiri wao.
Akifungua kikao kazi cha Wanasheria wa Mamlaka za Serikali za Mitaa
kilichofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Walimu Nzega tarehe 18
Februari,2016, Bi. Liana aliwaasa Wanasheria kuacha kuuza kesi kwani
alisema kufanya hivyo ni kuwaumiza wananchi.
Bi. Liana aliwataka wanasheria kuwa wazalendo zaidi kwa kujitoa na
kujitolea wakati wanaposimamia mashauri mahakamani pamoja na kusimamia
ipasavyo mikataba na kujiepusha na rushwa.
Aidha, Mkuu wa Wilaya aliwataka wanasheria kujiepusha na migongano ya
kisheria kwakuwa wengi wao ni mawakili wa kujitegemea na kutambua kuwa
wana wajibu mkubwa wa kulinda maslahi ya waajiri wao.
Mafunzo hayo yalihudhuriwa na Wanasheria kutoka Halmashauri za
Mji/Wilaya za Urambo,Tabora,Nzega,Uyui,Mkoa wa Tabora, Nzega, Sikonge,
Igunga na Kaliua.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenister Mhagama ametengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dkt. Carina Wangwe uliotangazwa leo Dar es salaam. Taarifa iliyotolewa usiku huu imeeleza
kuwa uteuzi huo umetenguliwa kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya
taratibu, uteuzi mpya kwa mujibu wa mamlaka na sheria utakapofanyika
taarifa zitatolewa kwa wananchi
Udanganyifu katika udahili wa wanafunzi kwenye vyuo ambayo
havijasajiliwa kuanza kudhibitiwa, baada ya Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (Nacte) kuzindua mfumo wa udahili wa pamoja (CAS) kwa mwaka wa
masomo 2016/17.
Hayo yameelezwa leo na Kaimu Katibu Mtendaji wa Nacte, Dk Adolf Rutayuga
na kusema mfumo huo utaanza kutumika kesho saa 6.00 mchana.
Dk Rutayuga amesema mfumo huo utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na
mafunzo ya astashahada, stashahada na shahada ya kwanza kwa kozi zote
zinazotolewa na vyuo vikuu na taasisi zote za elimu nchini, tofauti na
ilivyokuwa awali.
Amebainisha kuwa Serikali imeamua maombi yote ya udahili kwa ajili ya mafunzo ya ngazi hizo yafanywe kupitia mfumo huo.
Kaimu Katibu huyo alisema mfumo huo wa i utafanyika kwa utaratibu unaotambulika.
“Mfumo huu utatumika kudhibiti udanganyifu katika udahili na kugundua baadhi ya waombaji wanaotumia vyeti vya bandia,” amesema.
Amesema mfumo huo utaiwezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi za
waombaji kwa ajili ya kufanikisha mipango ya elimu nchini na waombaji
kujiunga na mafunzo kwenye taasisi zinazotambuliwa na Serikali peke
yake.
Vilevile, Dk Rutayuga amesema mfumo wa CAS utawapunguzia waombaji
gharama za kuomba udahili katika vyuo mbalimbali, kuondoa uwezekano wa
mtu mmoja kudahiliwa zaidi ya mara moja, hivyo kuwanyima wenzake nafasi.
Ofisa Mafunzo ya Kompyuta wa Nacte, Daud Mabena amesema waombaji
wanatakiwa kutembelea tovuti ya baraza ambayo ni www.nacte.go.tz na
kufuata maelekezo ya udahili.
Gharama ya kutuma maombi kwa kozi moja ni Sh20,000 na zaidi ya moja Sh30,000.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dk. Adolf
Rutayuga, (Kulia) akisisitiza jambo wakati alipokuwa ikitangaza wa
kuzindua Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa
mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu
huo, utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada
(Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)
Katikati ni Mkurugenzi Udhibiti Ubora Rasmalimali watu , Edmund Kinwasi
na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufuatiliaji Tathimini na Uthibiti wa
baraza hilo , Christina Kumwenda. Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar
es Salaam.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dk .Adolf
Rutayuga, akipofya kitufe cha komputa kuashiria Uzinduzi rasmi wa
Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo
yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo,
utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti),
Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)
wanaoshuhudia kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufuatiliaji
,Tathimini na Uthibiti ,Christina Kumwenda, Mkurugenzi udhibiti ubora
rasmalimali watu Edmund Kinwas, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Vyuo
ushauri na Mipango Alfred Kilasi,Mkurugenzi Mafunzo na Upimaji Bakari
Issa (kushoto) na Afisa Mifumo ya Kompyuta wa baraza hilo , Daud
Mabena.Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf
Rutayuga(Kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini
Dar es Salaam ( hawapo pichani) kuhusiana na Uzinduzi wa Mfumo wa
Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo
yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo
utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti),
Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree) wapili
kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Udahili Seremani Majindo, Mkurugenzi wa
Mfumo na Upimaji,Bakari Issa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya vyuo na
ushauri na Mipango.Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam
BARAZA
la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), limetangaza ufunguzi rasmi wa
Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo
yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo,
utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti),
Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree”).
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maelekezo na
Msaada kwa Taasisi wa NACTE, Dk. Adolf Rutayuga amesema kuwa, kwa
mwaka wa masomo wa 2015/16, Baraza liliratibu udahili wa wanafunzi
katika vyuo mbali mbali kwa kozi za astashahada (Cheti) na stashahada
(Diploma) kwa mafunzo ya afya na ualimu yaliyoidhinishwa na Baraza. ameongeza
kuwa, Baraza pia lilishirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania,
kuratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo mbali mbali kwa kozi za
shahada ya kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission
System (CAS)).
“Mifumo
hii miwili ilifanyika kwa ufanisi mkubwa na uliwawezesha waombaji
kudahiliwa. Mifumo hii ya udahili imekuwa na mafanikio yafuatayo:
Kudhibiti udanganyifu katika udahili uliotokana na baadhi ya waombaji
kutumia vyeti vya bandia, kuwapunguzia waombaji gharama za kuomba
udahili katika vyuo mbalimbali, kuondoa uwezekano wa mwombaji udahili
mmoja kudahiliwa zaidi ya mara moja na kuwanyima waombaji wengine
nafasi, kuiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi za waombaji udahili
kwa ajili ya kufanikisha mipango ya elimu nchini, na kuwawezesha
waombaji udahili kujiunga na mafunzo kwenye taasisi zinazotambuliwa na
Serikali,” alieleza.
Dk
Rutayuga alieleza kuwa, kwa kutambua mafanikio ya udahili wa pamoja
yaliyopatikana, Serikali ya kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, imeamua kuwa maombi yote ya udahili kwa
ajili ya mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na
Shahada ya kwanza (Bachelor Degree) yafanywe kupitia kwenye Mfumo wa
Pamoja wa Udahili (CAS).
Amefafanua
kwamba. Baraza linautangazia umma kuwa, kuanzia mwaka wa masomo
2016/2017 udahili wa kozi zote nchini utafanywa kupitia Mfumo wa Udahili
wa Pamoja (CAS) unaosimamiwa na NACTE, Vyuo Vikuu na taasisi za Elimu
zote nchini Tanzania zinazotoa mafunzo ya Cheti na Diploma kutodahili
wanafunzi nje ya mfumo wa udahili wa Pamoja kuanzia mwaka wa masomo
2016/17.
“Tunapenda
kutoa taarifa pia kuwa, maombi ya kujiunga na kozi za Cheti na Diploma
yataanza kupokelewa rasmi kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia
tarehe 4 Machi 2016, saa sita mchana. Baraza pia litaanza kupokea rasmi
maombi ya kujiunga na kozi za Shahada (Degree) kwa wahitimu wenye
Diploma kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia tarehe 4 Machi 2016,
saa sita mchana,”
Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kuomba mafunzo kwa kutumia Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS), alisema Baraza linashauri waombaji watembelee tovuti ya Baraza ambayo ni www.nacte.go.tz
Habari zenu, Kwanza kabisa nipende kuwapongeza wadau wa blog hii pendwa ya MASWAYETU BLOG kwa kuendelea kuwa pamoja katika kuendeleza upatikanaji wa habari mbalimbali.
Hadi sasa Maswayetu blog idadi ya FOLLOWERS wapatao MIL 4300000. Ina pageviewers hadi 40000 kwa siku moja.
Tunakuomba ewe mdau wetu kutangaza biashara yako kwenye blog yetu,tuna uhakika utafanikiwa kwani blog yetu inafikiwa na watu wengi zaidi.
Kama unatangazo lolote lile,tafadhali wasiliana na uongozi wa MASWAYETU BLOG kwa kupiga simu namba
Hatimaye aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi.
Wawili
hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa moja, lakini
habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri
kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Ndoa
hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu za Dr Slaa ambaye mwaka 2010
aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani akidai bado
anamtambua Josephine kuwa ni mke wake wake halali.
Mume
huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama impatie
haki yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa.
Misukosuko
ya wawili hao iliendelea ambapo mwaka 2012 aliyekuwa mke wake, Rose
Kamili alifungua kesi kupinga ndoa hiyo huku akitaka alipwe milioni 50.
Dr
Slaa na Mushumbusi wanaishi kwa takribani miaka sita sasa na waliwahi
kuanza maandalizi ya kufunga ndoa wakiwa hapa nchini lakini wakashindwa
kutokana na mapingamizi hayo.