Thursday, 25 February 2016

Taarifa Kwa Umma Toka TCU Kuhusu Mgogoro wa Chuo Cha St. Joseph (SJUIT) Kampasa ya Arusha

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

 TAARIFA KWA UMMA
MGOGORO WA CHUO KIKUU CHA MT. YOSEFU TANZANIA(SJUIT) KAMPASI YA ARUSHA

1.  Tunapenda  kuuarifu  umma  kwamba,  Chuo  Kikuu  cha  Mt.  Yosefu  Tanzania (SJUIT) Kampasi ya Arusha ni mojawapo ya vyuo vikuu vilivyosajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ambacho kilianza kudahili wanafunzi kwa mara ya kwanza mwaka wa masomo 2013/2014.

2.  Kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Vyuo Vikuu, Sura ya 346 ya Sheria za Tanzania, Tume ina mamlaka ya kusimamia na kudhibiti ubora na usimamizi wa uendeshaji wa Vyuo Vikuu hapa nchini.

3. Tume  inatambua  kuwa  kwa  nyakati  tofauti  kumekuwapo  na  matukio  ya migogoro baina ya uongozi wa Chuo  Arusha na wanafunzi.
Tume imekuwa ikifuatilia kwa karibu chimbuko la migogoro hiyo na kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo kwa uongozi wa chuo kurekebisha kasoro zinazosababisha migogoro chuoni hapo. 
Katika kutekeleza azma hiyo, hivi karibuni Tume iliunda jopo la wataalam kufanya ukaguzi wa kina katika Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania Kampasi ya Arusha. Ripoti ya ukaguzi huo iliwasilishwa tarehe 22/02/2016.

4.  Kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa kisheria, ripoti hii inatakiwa kuwasilishwa na kujadiliwa na Kamati ya Ithibati ya Tume ya Vyuo Vikuu, ambayo itatoa mapendekezo kwa Tume kuhusu hatua stahiki za maamuzi. Kamati hii itakutana katika kikao cha dharura tarehe 25/02/2016 saa 3:00 asubuhi, na taarifa ya Kamati  hiyo  itawasilishwa  kwenye  Mkutano  wa  dharura  wa  Tume  tarehe hiyohiyo saa 9:00 alasiri.

5. Kwa mantiki hiyo, taarifa rasmi kuhusu maamuzi yaliyofikiwa juu ya hatma ya Kampasi hiyo ya Arusha ya Chuo cha Mt. Yosefu itatolewa siku ya Ijumaa tarehe 26/02/2016.

6.  Kwa taarifa hii, Tume inawaomba wanafunzi wote wa Chuo cha Mt. Yosefu Kampasi ya Arusha kuwa watulivu wakati huu ambapo suala lao linashughulikiwa.

7. Tume inapenda kutumia fursa hii pia kuwaarifu wanafunzi wote wa vilivyokuwa Vyuo Vikuu Vishiriki vya Sayansi za Kilimo na Teknolojia (SJUCAST) na Teknolojia ya Habari (SJUCIT), kuwa orodha ya majina yao na vyuo walivyopangiwa inapatikana  katika   tovuti  ya  Tume  ya   Vyuo   Vikuu.  Hivyo  wanashauriwa kuondoka Chuoni  mara moja na kujiandaa kwa ajili ya kuripoti katika vyuo walivyopangiwa katika muhula wa pili.

Imetolewa na

PROF. YUNUS D. MGAYA

Katibu Mtendaji

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania

24 Februari 2016
Share:

RATIBA YA MTIHANI KIDATO CHA SITA(ACSEE) 2016 ,HII HAPA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 
Share:

TCU Yabani Madudu Vyuo Vikuu Tanzania,maamuzi kutolewa kesho

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya, amesema katika ukaguzi wa vyuo vikuu unaoendelea nchi nzima, wamebaini kasoro mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyuo vyote kutokuwa na walimu wa kutosha huku vingine vingi vikitumia mitala isiyoendana na soko la ajira.
 
Alisema kwa vyuo vingi visivyo vya serikali, kati ya asilimia 60 mpaka 80 ya walimu wake, hawana kiwango cha elimu kinachotakiwa kwa mwalimu wa chuo kikuu (shahada ya uzamivu).
 
Ukaguzi wa TCU kwa vyuo vyote nchini, unafuatia Waziri wa  Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, kuiagiza taasisi hiyo kufanya ukaguzi kwenye vyuo vikuu vyote na vile watakavyobaini vimekiuka kanuni za kutoa elimu ya juu, vipewe adhabu ikiwa ni pamoja na kuvifutia ithibati.
 
“Ukaguzi umebaini Tanzania kwa ujumla wake kuna upungufu wa walimu kwenye vyuo vikuu vyote, hakuna kinachojitosheleza kwa walimu, hata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Muhimbili...lakini tulichokiona kweye vyuo kama cha Dar es Salaam, Muhimbili, St. Augustine na Tumaini, vimekuwa vinawasomesha walimu wake, vina mradi na bajeti za kusomesha ili wapate shahada ya tatu ndani na nje ya nchi,” alisema na kuongeza:
 
“Baadhi ya vyuo vikuu binafsi, wao hawasomeshi, kazi yao ni kuwavizia wenzao wakisomesha ndipo wawachukue, bahati nzuri hawana fedha za kuwalipa, maana hawa wakisomeshwa mishahara yao ni mikubwa hawawezi kuwalipa, wanaishia kuwachukua kwa muda wa ziada,” alisema.
 
Kuhusu viwango vya elimu vya walimu, Profesa Mgaya alisema: “Ukiona chuo kina walimu karibu asilimia 60 hadi 80 ni wa shahada ya pili (shahada ya uzamili) tu, hawana ya tatu (shahada ya uzamivu).
 
Pia tumebaini vyuo vikuu vinavyofundisha sayansi vina upungufu kwenye maabara, hakuna vifaa vya kisasa vya kutosha vinavyoendana na idadi ya wanafunzi. Hii ipo karibu vyuo vikuu vyote binafsi tulivyovikagua angalau vile vya umma vina mpango wa kutekeleza hilo,” alisema Profesa Mgaya.
 
Akielezea kuhusu mitaala alisema baadhi ya vyuo binafsi vimekuwa vikizalisha wahitimu wasioendana na soko.
 
Alisema wanapobaini upungufu kama huo, hurudi chuoni kuwataka waipitie mitaala yao ili iendane na soko.
 
Pia alisema changamoto nyingine waliyoibaini ni ufinyu wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa maktaba.
 
“Lipo tatizo la maktaba siyo kubwa na tatizo la vitabu, mfano UDSM kinaprogramu ya kuongeza ukubwa wa maktaba yake mara tatu ya iliyopo, lakini baadhi ya vyuo vikuu binafsi hawana program yoyote,” alisema.
 
Profesa Mgaya akizungumzia kuhusu ujio wa wanafunzi zaidi ya 100 wa Chuo Kikuu cha Mt. Joseph Tanzania (SJUIT) kampasi ya Arusha waliokuja Dar es Salaam ili kueleza changamoto zinazowakabili, alisema bahati nzuri waliyoyaeleza jopo la wataalam waliotumwa kuchunguza wameshakabidhi ripoti Jumatatu ya wiki hii.
 
Alisema wanafunzi hao walibainisha changamoto zao kuwa ni walimu hawatoshi, wengine hawana viwango, baadhi wakifundisha hawaeleweki kwa sababu lafudhi zao ni za Kihindi.
 
Alisema wataalam wa TCU wameshafanya ukaguzi kwenye chuo hicho na ripoti yake itajadiliwa leo kwenye Kamati ya Ithibati ya Vyuo Vikuu kisha kutoa mapendekezo ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa.
 
Alisema uamuzi wa kitakachoafikiwa yatatolewa kwa umma kesho.
 
Alisema matawi mengine ya chuo hiyo yaliyo Bagamoyo, Luguruni na Boko vya Dar es Salaam, ukaguzi wake umekamilika.
 
Pia alisema wanafunzi hao wamesema wana tatizo la maabara, maktaba, ada ni kubwa na kuzilalamikia sheria za chuo kuwa ni kali.
 
Kuhusu ada alisema serikali haijawa na ada elekezi, lakini Aprili 9, mwaka jana walipeleka mapendekezo yao serikalini.
Alisema kutokana na bajeti wakati huo ilikuwa imeshapita, wanatarajia mwaka huu watafanikiwa. 
 
"Changamoto zao serikali tumeshaunda tume ya uchunguzi juzi Jumatatu jopo lilituletea matokeo, kesho tunaingiza kwenye kamati yetu ya ithibaki," alisema.
CHANZO: NIPASHE
Share:

NEWS:WANAFUNZI WA VYUO VIFUATAVYO WANATAKIWA KUOMBA MKOPO BODI YA MIKOPO KABLA YA TAR.4TH MARCH 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
HESLB LOGO
HESLB has started officially to receive electronic applications for students admitted to pursue HIGHER DIPLOMA IN SCIENCE/MATHEMATICS EDUCATION at Monduli,Korogwe and Kleruu only from 23rd-Feb-2016 at 00:00 Hours through 4th-Mar-2016 at 23:59 Hours. Please read carefully ALL information before filling and submitting your data!
Share:

Niva Aanika Siri za Nay wa Mitego

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Baada ya Nay wa Mitego kumchana staa wa bongo muvi,Niva super mario kuwa ‘hana pa kulala,analala kwenye gari’ kupitia wimbo wake wa shika adabu yako,Niva amejitokeza na kurusha madongo kadhaa kwa msanii huyo anayejiita rais wa manzese.

Kupitia mahojiano yake na kipindi kimoja cha redio Niva ameweka wazi kuwa hajaanza kumfahamu leo Nay na yeye amekuwa akimjua kwa jina la ‘Imma Chogo‘ na amewahi kumsaidia mambo kadhaa ikiwemo kulala kwake na kushangaa anasemaje yeye (Niva) hana pa kulala.

“Nay amewahi kuja kwangu mwaka 2012 ameibiwa kila kitu kwenye gari yake nikamsaidia tuka chill kwangu apoze machungu,kama sina pa kukaa pale alikuja kwa nani?” alihoji Niva na kuongeza “Sio hilo tu wakati wa kampeni Nay alivamiwa kwake,Dar akawa anataka msaada wa pesa nikatoa milioni mbili na nusu,na ndicho kipindi ambacho Shamsa alimpa kibuti kwenye ziara za kampeni,Mwanza kwa sababu hajielewi.” alimaliza Niva.
Share:

Q Chillah Aamua Kwenda Kusaka Soko la Muziki Nigeria

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Msanii wa bongo fleva ,Q Chilla ameweka wazi kuwa siku za hivi karibuni atafunga safari kwenda Nigeria kufanya kazi zake za kimuziki ili kupanua soko.

Hata hivyo Msanii huyo amesema hajajua bado atafanya kazi na msanii gani wa Nigeria ila amejipanga kukabiliana na yeyote atayejitokeza kwani anaamini ni uwoga kupanga kufanya kazi na msanii fulani tuu.

“kuna watuwengi ambao tunawasiliana nao kwa sasa,lakini nimeona niwafate kule kule Nigeria ilikuwa niende tarehe 20 lakini tumeongeza wiki mbili ili kuimarisha bendi kwanza ambayo nimeizindua..nimejiandaa kolabo na yeyote yule,kwa sababu ukisema fulani ina maana una hofu na watu fulani” alifunguka Q Chillah.
Share:

Wadaiwa 16 Waliotorosha Makontena Bandarini Kuanza Kufilisiwa Leo

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Wadaiwa 16 waliokwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), baada ya kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, mali zao zinaanza kukamatwa leo na kufilisiwa.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, iliyopewa kazi ya kufuatilia wadaiwa hao wakiwemo baadhi ambao wamekamilisha malipo, Yono Kevella alisema hayo Dar es Salaam jana.

Kevela alisema kuanzia leo wanakaa na vyombo vya dola, kuanza utaratibu wa kukamata na kufilisi mali za wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Kevela alisema hadi sasa hakuna zuio lililotolewa, linazowazuia kutekeleza wajibu wao katika kukusanya madeni hayo. Hata hivyo alisema, wengi wa wadaiwa baada ya kutolewa kwa muda huo wa siku 14, wameonesha moyo wa kulipa.

Wadaiwa 16 hawajamaliza madeni
Alitaja wadaiwa 16 ambao hawajalipa madeni yao wala kupunguza, ambao watafilisiwa wasipojitokeza kufanya malipo ni Said Ahmed Said Sh 28,249,352.50, Strauss International (45,393,769.95), Farid Abdallah Salum (52,185, 614.97).

Wengine ni Nasir Saleh Mazrui (60,105,873.77), Simbo Yona Kimaro (64,221,009.10), Ally Masoud Dama (102,586,719.22) na Juma Kassem Abdul (130,182,395.12), Salum Link Tyres (233,447,913.31) na Tybat Trading Co.Ltd (448,690,271.90).

Pia wamo IPS Roofing Co.Ltd (966,723,692.10), Tuff Tyres General Co Ltd, (7,435,254,537.03), Swalehe Mohamed Swalehe (34,687,165.00), Rushwheel Tyre General Co Ltd, (1,802,988,679.20), Said Ahmad Hamdan (68,362,558.31), Ahmed Saleh Tawred ( 59,237,578.40) na Farida Abdullah Salem Sh 75,334,871. 85.

Akizungumzia wadaiwa waliolipa ndani ya siku 14 walizopewa na zikaisha juzi, alisema wanane kati ya 24, ndiyo walijitokeza kulipa madeni baada ya kampuni yake kuwafuatilia.

Kevela alisema hadi jana zaidi ya Sh milioni 200 zimelipwa na wadaiwa hao.

Wadaiwa hao 24 walishindwa kulipa kodi kwa wakati kama walivyotakiwa kufanya, ndipo TRA ilimpa dalali huyo kazi ya kuwafilisi. Kampuni hiyo ya udalali ilitoa siku 14, kuanzia Februari 10, mwaka huu wawe wamekamilisha; muda ambao umeisha juzi.

Kevela alisema katika siku hizo 14, kati waliojitokeza kulipa,wanne kati yao wamemaliza madeni na wengine wanne wamepunguza madeni na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki.

Waliomaliza madeni yao
Wadaiwa waliolipa madeni yao yote ni Issa Ali Salim aliyekuwa akidaiwa Sh 94,543,161.96, Libas Fashion (26,593,245.78), Omary Hussein Badawy (21,346,615.40) na Zulea Abas Ali (16,760577.24).

Waliopunguza madeni yao
Waliopunguza madeni yao ni Zuleha Abbas Alli aliyelipa Sh milioni 47 na kubakiwa na deni la Sh 28,508,551, awali alikuwa akidaiwa Sh 75,508,551.88, mwingine ni Ally Awes Hamdani aliyelipa Sh milioni 17.26 awali alikuwa akidaiwa Sh 55,485,904.07).

Wengine waliopunguza kidogo ni Tifo Global Trading Co Ltd waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 1,573,300,644.58, Lotai Steel Tanzania Ltd, waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 5,476,475,738.19.

“Tulikabidhiwa wadaiwa 24 na TRA, waliokwepa kodi kwa kutorosha kontena katika bandari kavu ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, sasa walipewa muda wa kulipa ila walikaidi, tukakabidhiwa tuwafilisi mali zao zote ili kulipia madeni na wamejitokeza hao na kuanza kulipa wengine wamemaliza”, alisema Kevela.

Awali wadaiwa 24, walikwepa kodi ya Sh bilioni 18.95 kwa kutorosha makontena 329 ya bidhaa zao kutoka Kampuni ya SSB ambayo ndiyo mmiliki wa bandari kavu ya (Azam ICD) na kampuni ya Regional Cargo Services.

Mapema Desemba mwaka jana aliyekuwa Kaimu Kamishna wa TRA, Dk Philip Mpango alizungumza na waandishi wa habari na kusema kampuni 15 kati ya 43, zilizokwepa kodi baada ya kutorosha kontena 329 katika ICD ya Azam, wamelipa.

Dk Mpango alisema Desemba 12, mwaka jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho aliyotoa Rais John Magufuli ya siku saba kwa wakwepa kodi hao 43, kulipa wenyewe kwa hiari, vinginevyo sheria zitachukua mkondo wake. Kufuatia kauli hiyo ya Rais Magufuli, wadaiwa 15 walijitokeza na kulipa na waliobaki hawakujitokeza kulipa.
Share:

Kundi la Navy Kenzo Kufanya Show Kubwa Kwa Mara ya Kwanza Maisha Basement Jumapili Hii 28 Feb 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Kwa Mara ya Kwanza Kundi la Navy Kenzo litafungua Kamatia Tour Maisha Basement Club Dar Jumapili hii Tarehe 28 Feb...Njoo Uone Nahreel Anavyomkamatia Baby wake Aika..Pia mtawaona wakiimba Game, Viza, Bokodo na Nyimbo zao nyingine Kali ...
Usikose Kiingilio ni 10,000 mlangoni
Share:

Ndege Ndogo Yapotea ikiwa na Abiria 23

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Ndege ndogo ya shirika la ndege la tara Airlines iliyokuwa na watu 23 wakiwemo watoto imepota ikiwa maeneo ya usawa wa milima Magharibi mwa Nepal.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Pokhara, Magharibi mwa Mji Mkuu Kathmandu, kwenda Jomsom, eneo ambalo watu wengi wanaoenda kukwea milima ya Himalaya huanza safari yao ya kukwea milima hiyo.
Ripoti zinasema mabaki ya ndege hiyo yamepatikana ingawa hakuna taarifa zozote kuhusu vifo au majeruhi.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, Ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na maafisa wa udhibiti wa safari za ndege wa Pokhara dakika 18 baada ya kupaa na kwamba hakuna viwanja vya ndege kati ya maeneo hayo mawili.
Maafisa wanasema ndege hiyo ya shirika la Tara Airlines ilikuwa na marubani watatu na abiria 20, mmoja wao raia wa China na mwingine wa Kuwait. Wawili kati ya abiria waliokuwa wamebebwa na ndege hiyo walikuwa watoto.
Tangu mwaka 1949, kumetokea zaidi ya ajali 70 zilizohusisha ndege za kawaida na helikopta, na vifo vya watu 700
Share:

MSANII LULU ALIPIWA MAHARI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Wakati akikanusha vikali taarifa mbaya za kuzushiwa kifo mwishoni mwa wiki iliyopita na watu ambao alisema hajui lengo lao, habari ya heri ni kwamba, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, (pichani) anaelezwa kuwa kwenye shamrashamra za ndoa baada ya kudaiwa kulipiwa mahari na mfanyabiashara maarufu jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sasa).

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho ni mtu wa karibu wa Lulu, hivi karibuni mrembo huyo alilipiwa mahari hayo kwa siri kwa kuwa mwanaume huyo hakutaka mambo hayo yafike kwenye vyombo vya habari.

“Sasa mimi nawapa habari motomoto kuwa Lulu amelipiwa mahari na mwanaume wake wa sasa lakini ishu nzima ilikuwa kwa siri sana,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Shughuli nzima ilifanyika nyumbani kwa Lulu (Mbezi-Beach, Dar) na sasa kinachoendelea ni taratibu za harusi lakini jamaa (huyo mwanaume) hataki iwe na mbwembwe.


“Ndiyo maana Lulu sasa hivi ametulia siyo kawaida yake. Hata kwenye viwanja vya bata na shughuli za mastaa haonekani kwa sababu anafanya mazoezi ya kukaa nyumbani kama mke wa mtu.”

Habari hizo zilidai kwamba, Lulu ataolewa ‘soon’ kwani maandalizi yamepamba moto kimyakimya chini ya usimamizi wa mama yake, Lucresia Karugila.

Baada ya kunyaka madai hayo, Amani lilizungumza na Lulu ili kumpongeza kwa kuchumbiwa na kulipiwa mahari kisha kusikia neno lake juu ya ishu hiyo ambapo tofauti na matarajio ya mwanahabari wetu, msanii huyo alikasirishwa na habari hizo huku akiweka wazi kuwa mambo mengine katika maisha yake ni ya binafsi na kwamba siyo kila kitu anaweka wazi kwa watu wengine.

“Hayo ni mambo binafsi, kwenye maisha yangu siyo kila kitu cha kuweka wazi kwa watu,” alisema Lulu kisha akakata simu kwa hasira.
Share:

Dk. Tulia Ackson Anusurika Kifo Baada Ya Kupata Ajali

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali jana jioni.
 
Taarifa za awali zimeeleza kuwa Dk. Tulia alipata ajali hiyo baada ya gari dogo kugonga gari alilokuwa akisafiria katika eneo la Kiwira jijini Mbeya.
Share:

Listen/Download | AUDIO: Kimbunga Mchawi – NIMCHANE (Shika Adabu Yako)

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
maxresdefault

DOWNLOAD HAPA
Share:

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARY 25 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:

Chanzo cha Mgomo Chuo Kikuu St. Joseph Hiki Hapa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya

WANAFUNZI 1,548 wa Chuo Kikuu cha St. Joseph tawi la Arusha, wamegoma kuingia darasani kwa siku tatu na kukodi mabasi matatu kwenda Dar es Salaam kumwona Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

Lengo la safari yao hiyo ya Dar ni kujua hatma yao, baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), kufungia chuo hicho tawi la Songea.

Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya, alibainisha kuwa hatma ya chuo hicho, itatolewa rasmi kesho baada ya tume hiyo kupitia mapendekezo ya tume ya wataalamu iliyoundwa mapema kwa ajili ya ukaguzi wa chuo hicho, tawi la Arusha.

Kulikuwa na vurugu miongoni mwa wanafunzi juzi jioni, hali iliyofanya uongozi kufikia uamuzi wa kufunga chuo hicho kwa muda usiojulikana. Wakizungumza jana kabla ya kuanza safari kwenda Dar es Salaam kumwona Waziri Ndalichako, wanafunzi hao walisema mmiliki wa St. Joseph ni mmoja, hivyo kama tawi la Songea lina shida ni wazi matawi yote nchini yana shida.

Waliomba serikali kutoa ufafanuzi, kabla ya kuendelea kupoteza fedha za umma walizopatiwa kama mikopo.

“Pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu kutoa waraka kwenye mtandao kuwa kufungwa kwa chuo cha Songea, hakuhusiani na matawi ya chuo hicho, lakini sisi hatuna hakika tunataka watu hakikishie kama tupo salama,” alisema mwanafunzi Joel Lameck.

Aliendelea kusema, “na tukimaliza masomo yetu, je, tutapata ajira serikalini, yasije yakatukuta ya Chuo cha St. John cha Dodoma ambao hawakupata ajira kwa sababu elimu waliyopata haikuwa na viwango.”

Wanafunzi hao ambao wengi wao hawakutaka majina yao yatajwe gazetini, walisema wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kuwa chuo hicho kina upungufu mwingi, ikiwemo uhaba wa vifaa vya kufundishia.

Pia wanafunzi hao walihoji sababu za serikali, kutowaleta wanafunzi wa tawi la Songea iwapo tawi lao la Arusha lipo salama, badala yake wamepelekwa vyuo vingine, nje ya St Joseph.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Siles Balasingh, aliomba serikali kutoa majibu haraka kwa wanafunzi hao wanaosomea ualimu wa masomo ya Sayansi, waendelee na masomo yao, kwani wamepata wasiwasi baada ya kufungwa tawi la Songea, japo hawana shida na chuo.

Alisema wao kama chuo, wamejitahidi kubandika chuoni hapo tangazo la TCU kwamba tawi hilo halihusiki na matawi mengine, lakini wanafunzi hawaelewi, wamegoma kuingia darasani, pia wameharibu mali za chuo.

“Hawa wanafunzi leo siku tatu hawataki kuingia darasani na wamekodi mabasi matatu wanaelekea Dar es Salaam kumwona waziri, lakini wamewapiga baadhi ya wanafunzi wenzao kwa kuwakataza kufanya mitihani mpaka wapate uhakika wa masomo tunayowapatia kama tumekidhi vigezo vya mitaala ya elimu,” alisema.

Alisema walimu wanasikitika kuona vurugu zinatokea kwa sababu hiyo, hivyo ikiwezekana wanamwomba waziri wa elimu afike chuoni hapo, kutoa ufafanuzi ili wanafunzi wao hao wapatao 1,518 waendelee na masomo yao.

Hatma ya chuo kujulikana Ijumaa

Akihojiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dar es Salaam jana, Profesa Mgaya alisema mgogoro wa chuo hicho, ulianza muda mrefu tangu mwaka 2014, hali iliyosababisha tume hiyo kufanya ukaguzi chuoni hapo.

“Tume iliunda timu ya wakaguzi iliyoongozwa na maprofesa wa taaluma mbalimbali, waliokagua mfumo wa ufundishaji, mazingira ya ufundishaji na kuhoji wanafunzi chuoni hapo. Tayari timu hii imewasilisha ripoti yake kwa TCU,” alisisitiza.

Alisema leo tume hiyo inatarajia kukutana na timu hiyo na Kamati ya Ithibati majira ya saa 3 asubuhi, kuijadili ripoti ya ukaguzi wa chuo hicho na saa 9 mchana itaitisha mkutano wa dharura kujadili mapendekezo ya taarifa hiyo na kutoa maamuzi dhidi ya chuo hicho.

“Tutautangazia umma Ijumaa (kesho) majira ya saa nne asubuhi kuhusu hatma ya chuo hiki cha St Joseph tawi la Arusha.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger