INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Friday, 11 July 2014
SERIKALI YA TANZANIA YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 1,324
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Sekretarieti
ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia Watanzania wenye sifa
na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,324 ambazo ni kwa ajili
ya waajiri mbalimbali Nchini.
Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi amesema kuwa nafasi 1,334
zimeainishwa bayana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni
www.ajira.go.tz ili kuwawezesha wahitimu wote wenye sifa na uwezo
kutuma maombi kwa ajili ya kujaza nafasi hizo ajira Serikalini.
"Nadhani ni vizuri zaidi kwa kila
muhitimu anayetafuta kazi serikalini kufungua tovuti ya Sekretarieti ya
Ajira kuangalia nafasi za kazi zilizotangazwa na pale anapoiona kazi
inayoendana na sifa alizonazo kutuma maombi yake ili kuweza
kushindanishwa na wengine....maana ajira za Serikali hivi sasa ni za
ushindani hivyo inampasa kila anayetaka kupata kazi serikalini kujiandaa
vyema ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuajiriwa katika
Utumishi wa Umma" alisema Daudi.
Alifafanua
kuwa kwenye tovuti hiyo kuna matangazo mawili tofauti ya kazi ambapo
moja liko katika lugha ya Kingereza likiwa na jumla ya nafasi za kazi
447 na tangazo lingine lipo kwa lugha ya Kiswahili ambalo lina jumla ya
nafasi za kazi 877.
Aidha,
alizitataja baadhi ya nafasi hizo za kazi zilizoko katika tangazo la
kazi kwa lugha ya Kiswahili kuwa ni Mhandisi kilimo (agro–engineers),
Afisa kilimo (agro–officers) Mkufunzi kilimo (aquaculture), Afisa kilimo
msaidizi (agricultural field officers), Daktari wa mifugo (veterinary
officers), Daktari utafiti mifugo (veterinary research officer), Daktari
mifugo mkufunzi (veterinary tutor), Mkufunzi mifugo (animal science),
Afisa mifugo (live stock officer), Afisa utafiti mifugo (livestock
research officer), Afisa Utumishi (human resources officer), Afisa ardhi
msaidizi, Dereva (driver).
AJALI YA BASI: BASI LA AMANI LAPATA AJALI MAENEO YA SALANDA MKOANI TABORA, MTOTO MMOJA AFARIKI DUNIA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Basi la Amani Express likitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam limepata
ajali usku wa kuamkia leo maeneo ya Salanda mkoani Tabora, ambapo mtoto
wa miaka mitatu amepoteza maisha na abiria kadhaa wamepata majeraha.
Mashuhuda wanahisi kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi. Pichani
abiria wakitafuta vitu vyao
MUDA WA NYONGEZA KWA WAOMBAJI MIKOPO AMBAO HAWAKUJAZA FOMU ZA MAOMBI YA MIKOPO KABLA YA JUNI WAONGEZWA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa
mikopo kwa mara ya kwanza na Umma kwa ujumla kwamba muda wa maombi ya
mikopo umeongezwa kwa mwezi mmoja kutoka Julai 1, 2014 hadi Julai 31,
2014.
Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa
mikopo kwa mara ya kwanza na Umma kwa ujumla kwamba muda wa maombi ya
mikopo umeongezwa kwa mwezi mmoja kutoka Julai 1, 2014 hadi Julai 31,
2014.
Bodi ilianza rasmi kupokea maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao kuanzia
Aprili 23, 2014 ambapo tarehe ya mwisho wa kupokea maombi hayo ilikuwa
Juni 30, 2014.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa muda wa nyongeza kwa
waombaji wa mikopo kukamilisha maombi ya mikopo katika kipindi cha siku
30, kupitia mtandao kwa anuani: http://olas.heslb.go.tz.
NYOTA SANCHEZ ATUA ARSENAL, KULAMBA PAUNI 140,000 KWA WIKI
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Nyota mpya wa Arsenal, Alexis Sanchez akiwa ndani ya 'uzi' mpya.
MSHAMBULIAJI mahiri wa Chile na Barcelona, Alexis Sanchez, amejiunga
na Klabu ya Arsenal kwa pauni milioni 30 na mkataba wa miaka miaka
minne.
Nyota mpya wa Arsenal, Alexis Sanchez akiwa ndani ya 'uzi' mpya.WAZIRI MH.MAKALA AWA MBOGO BAADA YA KUAMBIWA KAKWEPA KODI
SERIKALI YA TANZANIA YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 1,100 NYINGINE
MBUNGE MH. SHIBUDA NOMA,AWACHANA LIVE WASUKUMA,AWATAKA KUACHANA NA DHANA YA "NDUHU TABHU" KWA KILA JAMBO,SIKILIZA HAPA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mlezi wa chama cha wakulima wa pamba nchini na msemaji
wa wabunge wanaotoka katika mikoa inayolima zao la pamba nchini,mbunge wa Maswa
Magharibi kupitia Chadema mheshimiwa John Shibuda amewapigia filimbi wasukuma
kwa kuwataka kuamka na kueleza wazi wazi matatizo yanayowakabili badala ya
kukaa kimya na kusema hakuna tatizo(Nduhu Tabhu” wakati kuna tatizo
linawasumbua.
MH RAIS:KILA HALMASHAURI KUPATIWA SH MIL 500 KWA AJILI YA UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Rais Jakaya Kikwete amesema serikali imetenga kwa kila halmashauri ya
wilaya nchini kupatiwa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa
nyumba za walimu ili kuwapunguzia adha na usumbufu walimu wanapopangiwa
kwenda katika vituo vya kazi wanakosa mahali pa kuishi.
Thursday, 10 July 2014
FUMANIZI :JIBABA LADAKWA LAIVU LIKIMLA URODA MWANAFUZNI, TENA NDANI YA GARI LAKE KWEUPE
AOZA MGUU BAADA YA KUPATA AJALI-ANAOMBA MSAADA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
AMA kweli ng’ombe wa maskini hazai, kijana Peter Sitiwati (26), mkazi wa Sinza ya Kwaremmy jijini Dar amejikuta akikatisha ndoto za utafutaji maisha kufuatia kuoza mguu baada ya ajali mbaya ya gari.
Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar juzikati kwa sauti ya kukata tamaa, Peter alisema alipata ajali ya gari mwaka 2013 maeneo ya Sinza-Mori, Dar na kuumia vibaya mguu wa kulia.
kijana Peter Sitiwati akiwa na maumivu makali yaliyosababishwa na kuoza kwa mguu.
’’Baada ya kugongwa na gari niliangukia mtaroni nikachomwa na kijiti
kwenye mguu wa kulia.
AMA kweli ng’ombe wa maskini hazai, kijana Peter Sitiwati (26), mkazi wa Sinza ya Kwaremmy jijini Dar amejikuta akikatisha ndoto za utafutaji maisha kufuatia kuoza mguu baada ya ajali mbaya ya gari.
Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar juzikati kwa sauti ya kukata tamaa, Peter alisema alipata ajali ya gari mwaka 2013 maeneo ya Sinza-Mori, Dar na kuumia vibaya mguu wa kulia.
ROSE NDAUKA:ASEMA KUWA SASA NI KAZI TU,NI BAADA YA KUMALIZA BIFU NA JACK CHUZI
HIZI NDO SABABU ZA MUME KUMCHINJA MKEWE,KUBWA NI KUTOKANA NA "WIVU WA MAPENZI"
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
JESHI
la Polisi Mkoa wa Arusha linamsaka kwa udi na uvumba, muuza nyama
jijini hapa, Lucas Lomayany Molel (37) mkazi wa Ilboru kwa madai ya
kumuua mkewe wa ndoa, Agnes Lucas (24) kwa kumcharanga na sime kwa kile
kinachoelezwa kuwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.
JESHI
la Polisi Mkoa wa Arusha linamsaka kwa udi na uvumba, muuza nyama
jijini hapa, Lucas Lomayany Molel (37) mkazi wa Ilboru kwa madai ya
kumuua mkewe wa ndoa, Agnes Lucas (24) kwa kumcharanga na sime kwa kile
kinachoelezwa kuwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.



