STAA wa filamu Bongo, Coletha Raymond
‘Koleta’ amewashukia waigizaji wenzake ambao ni wake za watu na kudai
kuwa wanaichafua sanaa hiyo kwa kujirahisisha kwenye ngono na wanaume
wengine.
Akizungumza kwa sharti la kutowataja
majina, Koleta alisema anawatambua wasanii wengi ambao ni wake za watu
na hufanya mchezo huo wakiwa eneo la kutengenezea muvi (lokesheni).
“Wananikera, wamezidi kujirahisisha na
kufanya uchafu. Kuna baadhi ya wake za watu hawajitambui wakiwa
lokesheni nakuishia kufanya umalaya,” alisema.