Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji wakisaini makubaliano (MoU) katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.
*************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Jeshi la Polisi ili kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kutekeleza azma ya kuendelea kulinda Maisha ya watanzania kwa kuhakikisha kuwa ukaguzi wa magari wakati yanapotumika hapa nchini unaofanyika kwa mujibu wa Sheria ya Trafiki (yaani Road Traffic Act, Cap 168), unafanyika kwa kutumia mitambo ya kisasa ili kuthibitisha usalama wake.
"Kwa kuzingatia uwezo uliopo,TBS itatumia wataalam wake, viwango pamoja na mitambo ya kisasa katika kukagua na kupima magari yote yatakayoletwa na Jeshi la Polisi, Kitengo cha Trafiki kwa ukaguzi kwa mujibu wa Sheria Usalama Barabarani Sura 168 ambayo inalazimu kufanyika ukaguzi wa vyombo vya moto ili kuhakikisha vinakidhi matakwa ya vigezo vya usalama kwa lengo la kulinda usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara". Amesema
Aidha amelihakikishia jeshi la polisi kwamba TBS ni mshirika sahihi wa Jeshi la Polisi Tanzania, kwani ndiyo inayodhibiti ubora na usalama wa vyombo vya moto vinavyoingia nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji amesema kupitia makubaliano hayo wanatarajia usalama barabarani kuimarika zaidi kwa watumiaji wa barabara.
"Tukiwa na Vyombo vya Moto salama tutakuwa na watumiaji salama wa barabara, tutakuwa na barabara salama na pia shughuli za uokozi zinaweza kuimarishwa na mwisho tutakuwa na tumeimarisha uongozi katika usalama barabarani". Amesema
Amesema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa Maelekezo ya Tume ya Haki Jinai inayosisitiza kushirikiana na wadau mbalimbali katika usimamizi wa sheria za usalama barabarani ili kuzuia uhalifu barabarani.
Pamoja na hayo amewataka wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha wanatimiza wajibu wa kisheria wa kukagua vyombo vyao kama inavyoelekezwa katika sheria kwani jeshi la polisi litakuwa na muhari kwa watakaoshindwa kutii sheria bila shuruti.
Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akibadilishana mikataba na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji mara baada ya kusaini makubaliano (MoU) katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akibadilishana mikataba na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna wa Polisi Awadhi Haji mara baada ya kusaini makubaliano (MoU) katika kushirikiana katika ukaguzi wa Vyombo Vya Moto kwa kutumia Vifaa vya Kisasa vinavyomilikiwa na TBS. Hafla hiyo imefanyika leo Januari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment