Tuesday 9 January 2024

MHANDISI MAHUNDI AMKALIA KOONI MKANDARASI MIRADI YA MAJI FUNTA NA WANGA LUSHOTO

...
-ASEMA HATAPEWA MUDA WA NYONGEZA

-WANANCHI 7121 KUNUFAIKA NA MAJI BAADA YA KUKAMILIKA

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuagiza Mkandarasi anayetekeleza Miradi ya Maji ya Funta na Mradi wa Maji wa Wanga iliyopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga kuwa miradi hiyo iweze kukamilika kabla ya Aprili 30, 2024 huku akisema itakapofika muda huo hatapewa muda wa nyongeza.

Kukamilika kwa miradi hiyo kunatarajia kunufaisha wananchi elfu 7121 wa Wilaya ya Lushoto katika kupata huduma ya maji safi na salama.

Mhandisi Mahundi ametoa agizo hilo leo Januari 8 2024 alipotembelea na kukagua utekelezaji wa miradi hiyo miwili kwenye Jimbo la uchaguzi Bumbuli lililopo Wilayani Lushoto

"Utekelezaji wa Mradi wa Maji Funta ulianza rasmi Agosti 18 2022 na ulipaswa kukamilika ndani ya siku 270 lakini mpaka sasa haujakamilika naomba nisisitize itakapofika April 30 hakutakuwa na kuda wa nyongeza tunahitaji wananchi 4782 wa maeneo ya Funta na Manga, na wananchi wa kijiji cha Manga na Kwemkole 2339 waweze kupata huduma" amesema Mhandisi Mahundi

Sambamba na hayo Mhandisi Mahundi amewataka wananchi kuendelee kutunza miundombinu ya maji pamoja na vyanzo vyake ili miradi inayotekelezwa iwe endelevu.

Naye Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mheshimiwa Kalist Lazaro ameahidi kumsimia kwa karibu Mkandarasi huyo ili miradi hiyo itekelezwe kwa wakati na wananchi waweze kupata huduma ya maji

Hata hivyo ikumbukwe kuwa Mradi huo unagharimu jumla ya Shilingi za Kitanzania Milioni 832.6 na baada ya kukamilika unaenda kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.





Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger