Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Vituo vya Taarifa na Maarifa Wilaya ya Kishapu vimefanya Kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambapo vimepongeza hatua kubwa zilizofanywa na Halmashauri hiyo katika utengaji wa bajeti ya mrengo wa kijinsia katika sekta ya elimu, kilimo na afya huku vikionesha kutoridhishwa na bajeti katika sekta ya maji iliyopangiwa bajeti ndogo katika mwaka wa fedha 2023/2024 wakati uhitaji wa maji bado ni mkubwa.
Kikao hicho kilichokutanisha pamoja Viongozi wa Vituo 9 vya taarifa na maarifa wilaya ya Kishapu na Maafisa na Wakuu wa Idara Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kimefanyika leo Ijumaa Desemba 29,2023 Wilayani humo.
Akiwasilisha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu uliofanywa na Vituo vya taarifa na maarifa, Mshauri Mwelekezi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Joseph Abila amesema malengo ya uchambuzi huo ni pamoja na kupongeza juhudi za serikali katika kutatua kero za wananchi kupitia utekelezaji wa bajeti za shughuli za maendeleo.
“Lengo la uchambuzi huu wa bajeti kijinsia pia ni kuishauri serikali kuhusu vipaumbele vya kibajeti vyenye manufaa kwa jinsia zote (mwanamke na mwanaume), kubainisha changamoto za utekelezaji wa bajeti na kushauri serikali kuhusu sera na Program mbalimbali zenye manufaa kwa jinsia zote ndani ya nchi pamoja na kujua ni kundi gani ndani ya jamii linaguswa moja kwa moja na utekelezaji wa bajeti na kushauri serikali kuhusu jinsi ya kuyafikia makundi yaliyoachwa nje”,amesema Abila.
Abila amesema katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, jumla ya shilingi Bilioni 12 (12,997,010,000/=) zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwa ni ongezeko la asilimia 3 kutoka bajeti yam waka 2022/2023 (Shilingi 12,651,769,415.98/=) ambapo 7.3% ya pesa zilizotengwa zimepokelewa hadi Septemba 2023 na 49% ya fedha zilizopokelewa zimetumika hadi Septemba 2023.
“Tunaipongeza sana Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kuongeza bajeti kwenye Sekta za vipaumbele ikiwemo afya imetengewa 22.43%, elimu 56.08%, Kilimo/mifugo 3.69%. Lakini Maji bajeti ni kidogo sana 0.23%”,ameongeza.
Akielezea kuhusu Sekta ya Afya licha ya kwamba bajeti imezingatia mrengo wa kijinsia inayotoa kipaumbele kwa afya za akina mama na watoto wachanga,dawa,vifaa tiba,zahanati,mama na mtoto, watumishi wa afya na miundombinu ya afya kwa kuidhinishiwa shilingi 3,478,048,389.92/=, bado ni ndogo ukilinganisha na mahitaji ya huduma za afya wilayani Kishapu.
“Kwa upande wa vipaumbele vya elimu ikiwemo matundu ya vyoo mashuleni,mabweni na miundombinu Rafiki kwa watoto wenye uhitaji maalumu vipaumbele vya bajeti vinashabihiana na vya TGNP na wadau wa vituo vya taarifa na maarifa. Hapa tunaipongeza serikali kutekeleza bajeti yenye mrengo wa kijinsia jumuishi”,amesema Abila.
Viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa wakiwa kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia.
Hata hivyo amesema mabweni bado ni changamoto katika shule nyingi wilayani Kishapu hali inayohatarisha usalama wa watoto wa kike wanaotembelea umbali mrefu kwenda shuleni, pia baadhi ya wazazi kushindwa gharama za bweni na ukosefu wa madaraja, vivuko vya mito hasa sehemu za Mwadui Luhumbo hali inayosababisha watoto kuacha kwenda shule wakati wa mvua kubwa.
Akielezea kuhusu sekta ya kilimo/ufugaji amesema vipaumbele vimeegemea zaidi kwenye ufugaji badala ya kilimo cha mazao na kwamba ushuru wa mazao unaokatwa haunufaishi wakulima hasa wanawake na mikopo ya zana za kilimo zina gharama kubwa na siyo rafiki kwa mkulima mdogo.
Katika hatua nyingine ameipongeza serikali kwa kuwapa kipaumbele wanawake kumiliki ardhi.
Aidha amesema katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu changamoto ya maji bado ni kubwa kwani yanapatikana kwa umbaili mrefu kwa baadhi ya maeneo mfano kata ya Kiloleli wanatembea umbali wa kilomita 15 kupata maji, Mwadui Luhumbo maji yamepita kwenda Kishapu Mjini wananchi hawana maji na bei kubwa za maji.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ibrahim Sakulia amesema wamezipokea changamoto zilizojitokeza katika mrejesho wa uchambuzi wa bajeti ya kijinsia na kwamba watazifanyia kazi.
Sakulia ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kushiriki katika michakato ya bajeti kwa kushiriki vikao na mikutano mbalimbali inayofanywa katika ngazi ya vijiji ili watoe maoni yao kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Kishapu, Fredina Said amesema wananchi wanataka bajeti inapotengwa iwe na mrengo wa kijinsia ili kuhakikisha hakuna mtu anaachwa nyuma katika jamii.
“Tunatamani kuona bajeti inatengwa ili ikatatue changamoto za jamii. Bajeti inapotengwa ije kwenye jamii, tunaamini mabadiliko yatatokea. Na sisi wana jamii tusisubiri kila kitu kifanywe na serikali mfano tuhamasishane watoto wapate chakula shuleni ili wasome kwa furaha”,amesema Fredina.
“Kishapu ni Halmashauri ambayo imekuwa mfano mzuri katika utengaji wa bajeti ya mrengo wa kijamii kwa ajili ya kutatua changamoto za kijamii. Tunaipongeza sana kwa kuwa na vipaumbele vya mrengo wa kijinsia”,ameongeza.
Aidha ameshauri kuanzishwa kwa jukwaa la wakulima wadogo ili kuwa na sauti ya pamoja ili kilimo kiwe na tija huku akihamasisha matumizi ya mbolea za asili katika kilimo kwani ni salama na upatikanaji wake ni rahisi.
Naye Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, John Mchele amesema wanaendelea kukazia mafunzo kwa wakulima na maafisa ugavi kuhusu matumizi ya mbolea za asili huku akiwahamasisha wakulima kuchangamkia fursa ya kupimiwa udongo ili kujua lishe ya udongo ili wajue wanapozalisha, wanazalisha kwa kiwango gani na zao gani linafaa kwa udongo huo.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mshauri Mwelekezi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Joseph Abila akiwasilisha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu uliofanywa na Vituo 9 vya taarifa na maarifa Wilaya ya Kishapu leo Ijumaa Desemba 29,2023 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mshauri Mwelekezi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Joseph Abila akiwasilisha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu uliofanywa na Vituo 9 vya taarifa na maarifa Wilaya ya Kishapu
Mshauri Mwelekezi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Joseph Abila akiwasilisha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu uliofanywa na Vituo 9 vya taarifa na maarifa Wilaya ya Kishapu
Mshauri Mwelekezi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Joseph Abila akiwasilisha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu uliofanywa na Vituo 9 vya taarifa na maarifa Wilaya ya Kishapu
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Kishapu, Fredina Said akizungumza wakati wa kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Kishapu, Fredina Said akizungumza wakati wa kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Kishapu, Fredina Said akizungumza wakati wa kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ibrahim Sakulia akizungumza wakati wa kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ibrahim Sakulia akizungumza wakati wa kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa wakiwa kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kikiendelea
Maafisa na Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Maafisa na Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, John Mchele akizungumza kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, John Mchele akizungumza kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joyce Mathias akizungumza kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Shoma Richard Sitta akizungumza kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mtwangi Mwipola akizungumza kwenye kikao cha Mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Washiriki wa kikao cha mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakipiga picha ya kumbukumbu
Washiriki wa kikao cha mrejesho wa Uchambuzi wa Bajeti Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakipiga picha ya kumbukumbu.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
0 comments:
Post a Comment