Sunday, 3 December 2023

DIT-MWANZA YAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

...

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)-Kampasi ya Mwanza, imeadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kutoa semina elekezi kwa wanafunzi.

Semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo wanafunzi juu ya masuala mbalimbali yahusuyo ukatili wa  kijinsia na namna ya kupinga vitendo hivyo.

Awali mwenyekiti wa dawati la njisia DIT-Mwanza, Bi,Consolata Ndimba ambaye pia ni mkufunzi chuoni hapo ameeleza  kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kujenga uwezo, uelewa na ushiriki wa kila mwanajamii katika kupinga ukatili wa kijinsia.

"Sisi viongozi wa dawati la njisia hapa DIT -Mwanza tumeona ni vyema tutumie fursa hii ya maadhimisho ya siku 16 kwa kutafuta wawezeshaji wa masuala mbali mbali ya kijinsia ili wawapatie mafunzo na stadi za maisha zitakazowasaidia kutimiza malengo yao wakiwa chuoni na hata baada ya kumalizia masomo yao, ilikusudi kila mwanafunzi aweze kujua nini chakufanya pindi anapokutana na kadhia hizi.'"amesema Bi,Ndimba.

Wakizungumza baadhi ya wanafunzi waliohudhuria mafunzo hayo, Grace Semule na Samwel Joshua  wamesema mafunzo yote yaliyotolewa yatawawezesha kujitambua pamoja na kuweka malengo yao ya masomo mbele zaidi na kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kukatisha ndoto zao.

Meshack Samwel ni moja wa wawezeshaji  katika maadhimisho hayo na daktari bingwa wa magojwa ya afya ya akili kutoka hospitali ya rufaa sekou Toure Jijini Mwanza amewahimiza wanafunzi kujitambua ili kuepukana  na madhara yanayoweza kuhatarisha maisha yao.

Naye mhadhiri na mwakilishi wa Mkurugenzi wa DIT  Kampasi , Bwana,Shija Mbitila amesema "Taasisi ya DIT Mwanza  inaungana na taasisi nyingine kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kutoa mafunzo elekezi, tukijua  madhara yanayotokana na ukosefu wa utambuzi kuhusu masuala hayo ni makubwa.

aidha Mbitila ameongeza kuwa "wanafunzi wetu kupitia mafunzo waliyopata yatawasaidia  kujitambua zaidi na kushiriki kupinga vitendo hivyo".

Taasisi ya DIT Kampasi ya Mwanza inaadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na kutoa semina hiyo ikiwa na lengo la kuwawezesha wanafunzi kutimiza ndoto zao za kitaaluma bila vikwazo vitokanavyonna vitendo vya kikatili.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger