Saturday, 16 December 2023

MHANDISI LUHEMEJA: TUFANYE KAZI KWA USHIRIKIANO NA KUTANGAZA MAFANIKIO YETU

...
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amefanya kikao kazi na watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji.

Kikao kazi hicho kilifanyika katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma, na kimehudhuriwa na Menejimenti ya Ofisi za Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu pamoja na Taasisi zilizo chini yake : NSSF, PSSSF, WCF, CMA, OSHA, Idara ya Maendeleo ya Vijana na Idara ya Kazi. Miongoni mwa wadau wengine walioshiriki kikao kazi hiki ni Kampuni ya Mkulazi Holding Company wamiliki wa kiwanda cha kutengeza sukari, Kilimanjaro International Leather Industries Co. Limited, wamiliki wa kiwanda cha kutengeza viatu na bidhaa zinazotokana na ngozi.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhandisi Luhemeja aliwataka watendaji wote wa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zilizo chini yake kufanyakazi kwa ushirikiano, kuwa wabunifu, kuongeza juhudi ya kazi, kutatua kero za wananchi pamoja na kutangaza mafanikio makubwa ambayo Ofisi hiyo na Idara zilizo chini yake imeyafanya.


Aidha, amewakumbusha watendaji wote juu ya umuhimu wa kuendelea kuthamini watu wote, kuhakikisha watu wote ambao tunahudumia wanapata haki zao kama ambavyo wanatakiwa wazipate na katika wasilisho lake ameonyesho ni kwa jinsi gani Wizra anayoongoza inavyohusika na asilimia kubwa ya watanzania wote ukiachilia mbali waajiri na waajiriwa wa nchi hii.

“Unapozungumzia kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu unazungumzia asilimia karibia yote ya wananchi wa taifa hili wanaangukia humu, ni jukumu letu kuona jamii yote hii inahudumia na mwisho wa siku hata tutapokuwa tumemaliza utumishi wetu tubakize historia ya yale mambo mazuri tuliyowafanyia watanzania”, Alisema Luhemeja.

Pamoja na mambo mengine Mhandisi Luhemeja amesema mambo mazuri yaliyofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Idara zilizo chini yake yanapaswa kutangazwa ili wananchi waweze kuyafahamu na hiyo ndio dira ya Serikali.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger