Wednesday 21 September 2022

AKATWA MKONO NA TITI NA MMEWE AKIMTUHUMU KUFUTA 'MISSED CALL' YA MWANAUME MWINGINE

...

Maria Marwa aliyekatwa mapanga
***

Maria Marwa (36) mkazi wa Kijiji cha Isango, wilayani Rorya mkoani Mara, amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa baada ya kujeruhiwa kwa mapanga na kukatwa mkono wa kushoto na titi la kushoto na mume wake kwa madai ya kukosekana kwa namba ya simu iliyopigwa kwenye simu ya mwanamke huyo.

Akisimulia tukio hilo mwanamke huyo amesema usiku wa kuamkia Septemba 8 mwaka huu baada ya chakula cha usiku mume wake Werema Ibaso, alimuomba ampatie simu yake na kuanza kumhoji juu ya namba ya simu iliyopigwa siku mbili nyuma ambapo mwamke huyo alipoikosa ndipo mwanaume huyo alipochukua panga na kuanza kumkata kata maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Akizungumzia sababu ya kukata mkono na titi Daktari wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara, amesema mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo kwa kuchelewa hivyo majeraha aliyokuwa ameyapata yalianza kuharibika.

EATV ilimtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime, Rorya Geofrey Sarakikya, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema jeshi la polisi linaendelea kumsaka mwanaume huyo ambaye baada ya kufanya tukio hilo na kutoroka kusikojulikana.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger