
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mhe.David Kihenzile wakitazama namna ya uhifadhi maji taka katika kiwanda cha kutengeneza nguo EPZA mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea mamlaka hiyo leo Septemba 28,2022 Jijini Dar es Salaam.












(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
************************
KAMATI ya Bunge Viwanda Biashara na Mazingira imeishauri Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kuhakikisha uchafu ulipo katika dampo kuufanya fursa na kuibua miradi mbalimbali itokanayo na uchafu ili kupunguza mlundikano wa uchafu katika eneo hilo.
Pia imeutaka uongozi wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji(EPZA) kuboresha miundombinu ya kimazingira katika eneo hilo ili kuweza kuwavutia na kuwashawishi wawekezaji.
Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyotembelea Dampo hilo na baadae Mamlaka ya Ukanda Maalumu ya Uwekezaji(EPZA) Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda Biashara na Mazingira David Kihenzile kimsingi alisema hatua hizo zote ni muhimu na zaidi zimelenga kuhakikisha afya wananchi zinalindwa.
Akiwa na Kamati hiyo katika dampo la Pugu Kinyamwezi, Kihenzile alisomewa ripoti ya utendaji kazi wa Dampo na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Amani Mafuru aliyebainisha kuzidiwa kwa dampo hilo kutokana na uwingi wa taka zinazozalishwa katika Jiji la Dar es Salaam.
"Tumejionea changamoto lukuki ambazo zinalikabili dampo hili, kimsingi sisi kama kamati tumeona kuna kila sababu ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kuweka mkono wake mahali hapa na kulisaidia Jiji la Dar es Salaam ambalo linaoekana wazi kuwa limezidiwa nguvu" alisema Kihenzile
Alisema kwa kufanya hivyo pamoja na mambo mengine kwa kiasi kikubwa kutasadia kuokoa maisha ya wananchi waliopo jirani na dampo hilo kutokana na athari zitokanazo na dampo ikiwemo hewa chafu.
Kuhusu EPZA Kihenzile mbali na kutaka Viwanda vingine nchini kuiga njia bora ya utunzaji wa mazingira katika eneo hilo, aliutaka Uongozi unaousimamia ukanda huo wa uwekezaji kuhakikisha miundombinu yake ya kimazingira hasa mfumo wa majitaka ya viwanda yanakuwa bora zaidi ili kuendelea kuwavutia wawekezaji.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo akiwemo Hawa Mchafu na Deo Mwanyika, mbali na kuunga mkono hoja ya Ofisi ya Makamu Raise Muungano na Mazingira kuungana na Jiji la Dar es Salaam katika kutafuta suluhu ya dampo hilo,walisema kuna haja eneo linalolizunguka dampo kujengewa ukuta
Pamoja na ukuta, pia walishauri kuona namna gani afya za wananchi waliopo karibu na dampo hilo zinatazamwa lakini pia wafanyakazi wanaotoa huduma katika dampo hilo .
0 comments:
Post a Comment