Saturday 11 June 2022

COASTER ILIYOPELEKA MSIBA YAPINDUKA NA KUUA WATU WATANO KUJERUHI 9 TANGA

...


Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine tisa wamejeruhiwa baada ya basi dogo aina Coaster waliyokuwa wamepanda kuacha njia na kupinduka.

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Kalisti Lazaro amesema ajali hiyo imetokea jana Ijumaa Juni katika Kijiji cha Mbaramo Tarafa ya Umba wilayani humo.

Lazaro amesema gari hilo lilikuwa linarejea Dar es Salaam kutoka Kijiji cha Mbaramo kupeleka msiba.

Inadaiwa kuwa dereva wa gari hilo alishindwa kulimudu kwenye kona hali iliyosababisha gari hilo kupinduka.

Via Mwananchi

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger