Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Mwalu Charles (45) mkazi wa kijiji cha Shilabela kata ya Ulewe wilayani Kahama mkoani Shinyanga amefariki dunia baada ya kukatwa na kitu chenye makali sehemu za mgongoni, kichwani na mkono wa kulia na watu au mtu wanaotafutwa akituhumiwa kuwa mchawi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea Septemba 9,2021 majira ya saa mbili usiku katika kijiji cha Shilabela, kata ya Ulewe, tarafa ya Mweli ,wilaya ya kipolisi Ushetu, wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga.
“Mwalu Charles (45) mkazi wa kijiji cha Shilabela, alikufa kwa kukatwa na kitu chenye makali sehemu za mgongoni, kichwani na mkono wa kulia na watu au mtu wanaotafutwa”,amesema.
Amesema kiini cha tukio ni mgogoro wa kifamilia unaochochewa na imani za kishirikina ambapo marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa mchawi.
Amesema tayari watuhumiwa watatu wamekamatwa.
0 comments:
Post a Comment