Monday, 13 September 2021

MLINZI AUAWA KWA KUCHOMWA KISU AKIMZUIA JAMAA KUFANYA MAPENZI NA MHUDUMU WA GESTI KAHAMA

...

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mlinzi Kampuni ya Ulinzi ya Mast Holding aitwaye Steven Felician Samandari (25) ameuawa kwa kuchomwa kisu tumboni na mtu aliyekuwa amemkamata baada ya kuruka uzio akifuatilia wahudumu wa Bar/Guest house kwa ajili ya mapenzi Mjini Kahama.

Kwa Mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando kwa vyombo vya habari, tukio hilo limetokea Septemba 11,2021 majira ya saa nane usiku katika mtaa wa Nyahanga kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama.

 "Mlinzi huyo aliuawa kwa kuchomwa kisu tumboni na mtu aliyekuwa amemkamata baada ya kuruka uzio akifuatilia wahudumu wa bar/guest kwa ajili ya mapenzi",amesema.

"Chanzo cha tukio hilo ni kufuatilia wahudumu wa bar/guest kwa ajili ya mapenzi. Eneo la tukio kimeokotwa kisu kikiwa tumboni. Mbinu iliyotumika ni kuchoma kisu tumboni",amesema Kamanda Kyando.

Kamanda Kyando amesema Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamke aitwaye Fatuma Juma Charles (22), mhudumu wa bar kwa uchunguzi.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger