Saturday, 11 September 2021

MFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB ANUSURIKA KUFA KWA KUPIGWA,KUKATWA MKONO SHINYANGA

...
Picha haihusiani na habari hapa chini

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB Debora Rwekwama (34) mkazi wa Bushushu Mjini Shinyanga amenusurika kufa baada kushambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kukatwa mkono wa kushoto kwa kisu na mme wake aitwaye Jacobo Mwajenga (35) kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea Septemba 9,2021 usiku katika mtaa wa Bushushu, Manispaa ya Shinyanga.

“Debora Rwekwama (34) Banker - CRDB, mkazi wa Bushushu Manispaa ya Shinyanga alishambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na baada ya kupoteza fahamu alikatwa mkono wa kushoto kwa kisu na mme wake aitwaye Jacobo Mwajenga (35)mkazi wa Bushushu”,amesema Kamanda Kyando.

Ameeleza kuwa hali ya majeruhi ni mbaya na amelazwa katika hospitali ya wilaya Kahama.

Amesema chanzo cha tukio ni wivu wa mapenzi na kwamba tayari Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa wa tukio hilo.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger