Friday, 17 September 2021

DC ILEMELA: SENSA INA MAANA KUBWA TUKAHESABIWE

...

Wananchi wa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza wametakiwa kujiandaa kwa ajili ya kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika mwakani ili kupata takwimu halisi zitakazoisaidia Serikali katika mipango ya maendeleo.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masalla wakati akizungumza na watendaji wa Manispaa ya Ilemela na viongozi wa ngazi mbalimbali za wilaya hiyo katika ukumbi wa shule ya sekondari Marist iliyopo kata ya Nyakato ikiwa ni hitimisho la ziara yake aliyoifanya Kwa kutembelea kata 18 za wilaya hiyo ikisalia kata ya Nyamanoro ambapo amewaasa viongozi wa mitaa na kata kuhamasisha wananchi kushiriki na kutambua umuhimu wa zoezi hilo kwao binafsi na taifa kwa ujumla.


"Wananchi wetu wajiandae kuhesabiwa, hili ni zoezi la kitaifa na lina maana kubwa sana kwetu, Mipango tunayoipanga ya kimaendeleo haitekelezeki kama hatujui idadi ya watu wetu", alisema.

Aidha Mhe. Masalla akatumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Kwa kumuamini na kumteua kuwa mwakilishi wake katika wilaya ya Ilemela huku akiahidi kushirikiana na viongozi wengine na wananchi katika kuileta maendeleo wilaya hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt. Angeline Mabula mbali na kumpongeza Mkuu huyo wa wilaya kwa jitihada kubwa anazozifanya katika kuwatumikia wananchi amemshukuru Mhe Rais Samia kwa kutoa fedha kiasi cha bilioni moja kila Jimbo kwa ajili ya ujenzi wa barabara.


Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Mhandisi Apolinary Modest akiwasilisha mchanganuo wa miundombinu ya elimu ndani ya wilaya aliwaomba wadau kushirikiana katika kutatua kero na kuweka mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia

Akihitimisha Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela amesema kuwa anaridhishwa na juhudi za Mkuu wa wilaya ya Ilemela katika utatuzi wa kero za wananchi huku akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kuitendea haki Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi,
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger