Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndg Daniel Chongolo akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya na chama akikata Utepe kuashiria kuzindua Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo Chuo cha Mafunzo Ihemi Iringa.










Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndg Daniel Chongolo akipanda Mti wa Kumbukumbu Katika eneo la Chuo cha Mafunzo Ihemi Iringa,leo tarehe 19 June 2021


....................................................................................
Katibu mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo leo amezindua ukumbi wa Benjamini Mkapa katika chuo cha mafuzo cha umoja wa vijana CCM Ihemi mkoani Iringa pamoja na kufungua mafunzo ya wenyeviti wa wilaya wa umoja wa vijana.
Ndg. Chongolo amewataka Viongozi hao kuendelea kulinda taswira ya chama cha mapinduzi na viongozi wake kwani hilo ndio jukumu kubwa la kiundwa kwa jumuiya hiyoo.
"Chama hiki akina mtu wa kukilinda isipokuwa Vijana, tuna wajibu na tumehapa kulinda Heshima ya Viongozi wetu, tunao wajibu mkubwa wa kulinda Mhe. Rais wetu na mwenyekiti wa chama chetu Samia Suluhu Hassan", amesema.
Aidha Ndg. Katibu mkuu Chongolo ametoa maelekezo kwa Viongozi hao kuendelea kukaa na kutafakari namna ambavyo watachochea nguvu na maarifa yao kwa chama mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Pamoja na hayo Ndg. Chongolo ameeleza kuwa nafasi ya vijana katika taifa lolote duniani ni kubwa hivyo wanategemewa katika ujenzi wa uchumi na Maendeleo ya Taifa.
Pamoja na Mambo mengine Ndugu Chongolo ameshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na imani kubwa kwa vijana na kumteua yeye katika nafasi hiyo kubwa kutoka kwenye kundi la vijana.
Katika tukio hilo Ndugu Katibu Mkuu aliambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka H. Shaka
0 comments:
Post a Comment