Wednesday, 16 June 2021

MASHEIKH WA UAMSHO WAACHIWA HURU

...

Masheikh wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), waliokuwa gerezani nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka saba wameachiwa huru, bada ya mashtaka dhidi yao kufutwa.

Kuachiwa kwao kunakuja siku chache baada ya viongozi mbalimbali wa dini akiwemo Mufti mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir kutaka mamlaka za Tanzania kutenda haki katika kesi dhidi yao.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mashitaka (DPP, Sylvester Mwakitalu) aliyenukuliwa na Chombo Mwananchi Digital nchini Tanzania, mashekh wote hao wamefutiwa mashitaka yote na kuachiwa huru na kilichobaki sasa ni taratibu za kutoka gerezani.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger