Tuesday 1 June 2021

ASKARI POLISI AMUUA KWA KUMPIGA RISASI JAMAA WAKIGOMBANIA MWANAMKE

...
Maafisa wa polisi kaunti ya Nairobi nchini Kenya wanachunguza kisa kimoja ambapo afisa wa polisi anadaiwa kumuua jamaa wa umri wa makamo kwa kumpiga risasi baada ya wawili hao kugombana kuhusu mwanamke.

Afisa huyo Titus Kipchirchiri Kirui anasemekana kumpiga risasi Charles Karugu Kikuyu mwenye umri wa miaka 32 kwa madai kwamba alikuwa akimnyemelea mpenzi wake.

 Kulingana na ripoti ya polisi, Maafisa wenzake wa polisi kutoka Embakasi waliofika katika eneo la tukio waliupata mwili wa Kikuyu ukielea kwenye damu sakafuni katika buchari moja mtaani Embakasi. 

Kikuyu alikimbizwa katika hospitali ya Mama Lucy lakini alifariki dunia kabla ya kuhudumiwa, upasuaji wa maiti unatarajiwa kufanywa wakati wowote. Kirui alikamatwa baadaye na yuko kizuizini huku uchunguzi zaidi ukiendelea. 

Maafisa wa polisi walipata risasi moja ambayo itatumika kama ushahidi katika kesi dhidi ya Kirui. 

 Chanzo - Tuko news


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger