Tuesday 19 January 2021

TAIFA STARS KUANZA NA ZAMBIA LEO MICHUANO YA CHAN

...


Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha wa Taifa Stars, Mrundi Etienne Ndayiragije amesema “maandalizi yameenda vizuri, wachezaji wapo sawa. Kuhusu korona wamechekiwa wote wako sawa, tuko vizuri. Tunaendeelea kujiandaa kwenye vile ambavyo tunaamini vitakuwa vya msaada kwetu”.

Kuhusu nafasi ya Stars kwenye mchezo huo, Ndayiragije amesema “ morali na hali ya kujiamini kuko juu kwenye kambi, wachezaji wapo tayari kwa mchezo, nimewaambia tutatcheza ili tushinde maana najua ushindi utainua ari kwenye kikosi na kupelekea tufanye vizuri kwenye michezo inayofuata”.

Etienne amesema ari imeongezeka baada ya kocha msaidizi Selemani Matola kujiunga na kikosi hicho  baada ya kumaliza majukumu ya kuiongoza kikosi cha Simba kwenye michuano ya Mapinduzi viswani Zanzibar na Erasto Nyoni akijiunga na timu baada ya kumaliza matatizo ya kifamilia.

Ushiriki wa Taifa Stars kwenye michuano ya CHAN umekuja baada ya miaka takribani 11 tokea ushiriki wao mwaka 2009 michuano hiyo ulipoanzishwa na ndiyo msimu ambapo Zambia walishiriki kwa mara ya kwanza na kushika nafasi ya 3 ikiwa ndiyo ya juu zaidi kwa upande wao kwenye CHAN.

Huu utakuwa mchezo wa 18 wawili hao kukutana, kwenye michezo 8 ya mwisho ambayo Stars imekutana na Zambia kwenye michuano tofauti kukiwa na mchanganyiko wa wachezaji wao wakigeni kwenye vikosi vyao, Zambia imeshinda mara 4, sare 3 wakati Stars imeshinda mara 1 pekee.

Ili Taifa Stars iweke hai matumaini ya kufuzu hatua inayofuata ya robo fainali, inahitaji ipate ushindi michezo yote mitatu ya makundi watakayocheza au kuwa na matokeo yatakayomfany awe na alama nyingi kuliko wote kwenye kundi D au alama nyingi zitakazomfanya ashike wapili kwenye kundi.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger