Tuesday 19 January 2021

SKAUTI MBEYA WATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KATA YA KALOBE

...

 

Muathirika wa mafuriko Bibi, Tamali Mwalukunga Mkazi wa Kata ya Kalobe jijini Mbeya akiwashukuru Vijana  wa Skauti baada ya kumjengea choo kilicho sombwa na mafuriko. Wa pili kushoto ni Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Sadock  Ntole na kulia ni Mratibu wa Majanga wa  chama hicho mkoani humo, Lusajo Exaud Sanga.
Vijana wa Skauti wakizibua mtaro.
Diwani wa Kata ya Kalobe, akiwapongeza vijana wa Skauti kwa kazi hiyo.
Vijana wa Skauti wakiwa katika picha ya pamoja.
Kazi ya uchimbaji choo cha Bibi Tamari Mwalukunga ikiendelea.
Choo cha Bibi Tamari Mwalukunga kikichimbwa.
Kazi ikiendelea.
Kazi ikiendelea..

Na Dotto Mwaibale.

CHAMA cha Skauti Mkoa wa Mbeya kimetoa msaada kwa kuwasaidia waathirika wa mafuriko katika Kata ya Kalobe jijini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Kamishna wa Skauti wa mkoa huo Mratibu wa Majanga wa  chama hicho mkoani humo, Lusajo Sanga alisema eneo lililoathiriwa zaidi na mafuriko hayo ni Mtaa wa Maendeleo A katika kata hiyo.

Alisema mafuriko hayo yalitokea Januari 8 mwaka huu kufuata mvua kubwa iliyonyesha.

" Eneo hilo liliathiriwa zaidi na mafuriko hayo kutokana na mifereji ya maji kuziba hivyo maji ya mvua kukosa muelekeo na kwenda kwenye makazi ya watu" alisema Sanga.

Alisema baada ya kutokea mafuriko hayo walisaidia na Kamishna wa Skauti Mkoa huo, Sadock Ntole, kuratibu namna ya kwenda eneo la tukio kutoa msaada wa kibinadamu kwa waathirika ikiwa ni pamoja na kuchimba vyoo vilivyosombwa na maji, kuzibua mitaro na kuwafariji waathirika kwa kushirikiana na diwani wa kata hiyo na viongozi wengine. 

Sanga alisema mafuriko hayo yaliathiri nyumba tano katika mtaa huo ambapo nyumba ya mkazi mmoja wa eneo hilo  aliyefahamika kwa jina la Mama Muro na Bibi Tamali Mwalukunga ziliathiriwa zaidi  kwani sehemu ya nyumba yake na choo  vilibomoka ambapo walilazimika kumjengea choo kingine cha muda.

Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Sadock  Ntole alisema wao kama skauti wamekuwa wakitoa msaada kwa jamii pale yanapotokea majanga ya namna hiyo hivyo baada ya kutokea mafuriko hayo walienda eneo la tukio kutoa msaada huo. 

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger