Wednesday, 13 January 2021

Mawaziri Wawili Wafariki Kwa Corona Nchini Malawi

...


Rais Lazarus Chakwera wa Malawi ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia vifo vya Mawaziri mawili, ambao wamefariki dunia baada ya kuugua Corona.

Mawaziri hao ni wa wizara ya Uchukuzi Sidik Mia na Lingson Belekanyama ambaye ni Waziri wa Serikali za Mitaa.

Hivi karibuni Rais Chakwera alilihutubia Taifa kupitia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Serikali na kuwataka Raia wa Malawi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Alisema kuwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini Malawi kwa sasa yako juu, hivyo ni lazima tahadhari ikachukuliwa.

Watu 50 wamethibitika kufariki dunia baada ya kuugua Corona nchini Malawi, katika kipindi cha kuanzia mwezi huu hadi sasa.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger