Monday 18 January 2021

BABU WA MIAKA 80 AFARIKI HOTELINI AKIWA NA MPENZI WAKE WA MIAKA 33 DAR

...

 

Picha ya kitanda

Na Mwandishi wa Malunde 1 blog Dar es salaam

Mwanaume aliyejulikana kwa jina la David Makerege Mluli (80) amekutwa amefariki dunia ndani ya Hoteli ya Mbezi Garden iliyopo Mbezi jijini Dar es salaam akiwa na mpenzi wake aliyejitambulisha kwa jina la Neema Kibaya (33).

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni ACP Ramadhan Kingai amesema tukio hilo limetokea Januari 16,2021 majira ya saa 9 alasiri katika eneo la Mbezi Beach ambapo Jeshi la polisi lilipokea taarifa kutoka kwa Meneja wa Hoteli ya Mbezi Beach Garden, Newton Mkonda kuwa katika hoteli hiyo kuna mteja amefariki dunia.

"Baada ya taarifa hiyo kupokelewa, Jeshi la polisi lilifika katika hoteli hiyo chumba namba 22 na kubaini uwepo wa maiti ya mwanaume ambaye baada ya kupekua katika nguo zake vilikutwa vitambulisho vyenye majina ya David Makerege Mluli (80) mkazi wa Goba aliyekuwa amekodi chumba hicho",ameeleza

"Pia katika chumba hicho alikutwa mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Neema Kibaya (33) mkazi wa Goba ambaye katika maelezo yake alieleza kuwa marehemu alikuwa mpenzi wake", ameongeza Kamanda Kingai.

Kamanda Kingai amesema uchunguzi wa awali ulifanyika na kubaini kuwa mwili wa marehemu hauna jeraha lolote na kuchukuliwa na askari polisi kupelekwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi na hifadhi.

Aidha amesema mwanamke huyo aliyekutwa chumbani ambamo mwili wa marehemu ulikuwemo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger