Wednesday 20 January 2021

BABA MATATANI KWA KUMFINYA AKITUMIA PRAIZI MTOTO KISA HAJUI KUSOMA WALA KUANDIKA

...
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mwanaume aitwaye Shija Abdallah (28), mkazi wa kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga kwa kosa la kumshambulia kwa kumfinya kwa kutumia Praizi mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 8 anayesoma darasa la tatu katika shule ya msingi Kambarage.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo Januari 15, 2021 saa majira ya saa nane kamili mchana. 

“Tunamshikilia Shija Abdallah kwa kosa la shambulio la kudhuru mwili baada ya kumfinya kwa kutumia praizi mwanae wa kiume, (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 08, mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Kambarage sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

“Bibi wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka 70 mkazi wa kata ya Ndala, Manispaa ya Shinyanga alibaini mtoto huyo kufanyiwa ukatili huo na baba yake mzazi huyo kwa kufinywa kwa kutumia praizi sehemu mbalimbali za mwili wake chanzo kikiwa ni kumuadhibu mtoto huyo kwa sababu hajui kusoma wala kuandika na mahudhurio shuleni ni hafifu”,amefafanua Kamanda Magiligimba. 

Amesema madhura amepatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga na hali yake inaendelea vizuri na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika. 

“Natoa wito kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwafanyia ukatili watoto wao na watumie njia sahihi ya kuwaadhibu watoto pindi wakoseapo. 

“Jeshi la polisi mkoani Shinyanga halitamvumilia mzazi au mlezi yeyote atakayebainika kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake na niwatake wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kukomesha vitendo hivi vya ukatili dhidi ya watoto”,amesema.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger