Thursday, 5 November 2020

MAGUFULI AAPISHWA KUWA RAIS WA TANZANIA ...MITANO TENA

...


Dk. John Pombe Magufuli ameapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mhula wa pili.

Dk. Magufuli ameapishwa leo Alhamis Novemba 5, 2020 katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma katika tukio lililoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Baada ya kula kiapo na kusaini hati ya utii alikabidhiwa katiba na mkuki na ngao ambapo pia Makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan naye alikula kiapo.

Rais Magufuli ametetea nafasi yake baada ya kushinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28.10.2020.

Magufuli alishinda kwa kupata kura 12,516,252 ambayo ni asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa. Tundu Lissu kutoka chama cha upinzani cha Chadema ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,933,271 ya kura zote ziizopigwa.

Jumla ya watu 15,91950 walipiga kura hizo wakati waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 29,754,699 kwa mujibu wa Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC).

Hii ni awamu ya pili kwa rais Magufuli kuongoza Tanzania, yeye ndiye alikuwa rais wa tano kuiongoza Tanzania kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020 na sasa anatarajia kuongoza mpaka mwaka 2025.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger