Friday, 24 July 2020

Viongozi Mbalimbali Waomboleza Kifo cha Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

...
Kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Benjamin William Mkapa ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Julai 24, 2020, viongozi mbalimbali wametoa salam za pole.

“Nimesikitishwa na kifo cha Mzee wetu Benjamin Mkapa (Rais Mstaafu wa Awamu ya 3). Nitamkumbuka kwa mapenzi yake makubwa kwa Taifa, ucha Mungu, uchapakazi na utendaji wake katika kujenga uchumi. Hakika Taifa limepoteza nguzo imara. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.” – Rais Dkt. Magufuli.

“Nimepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa. Hakika kifo hiki ni pigo kubwa kwa taifa letu.” –  Samia Suluhu, Makamu wa Rais wa Tanzania.

“What a loss!!!! Nakumbuka sana Upendo, Malezi na Busara zako nikiwa Mkuu wa Wilaya Masasi! Aaah, mwamba mwenye sifa halisi za kusini, what a loss!! Pumzika baba!” – Nape Nnauye.

“Nimepokea kwa mshtuko taarifa ya Msiba wa Mzee wetu Mzee Benjamin William Mkapa Rais wa Awamu ya Tatu Huu ni msiba Mzito kwa Taifa letu kama ambavyo Mh Rais John Pombe Magufuli alivisema wakati akitutanganzia Watanzania.” – Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji.

“Nimepokea taarifa za msiba wa Mzee Benjamin William Mkapa (Rais wa Tanzania 1995 – 2005) kwa masikitiko makubwa sana. Natuma salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wenzangu wote. Pumzika kwa amani baba yetu!” – Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa  Maliasili na Utalii.

“Ni majonzi makubwa kwa Tanzania! Tumuombee Mzee wetu Mhe. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa apumzike kwa Amani. Natoa pole kwa mke wa marehemu Mama Anna Mkapa, watoto, familia, ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wote. Bwana ametoa, bwana ametwaa.” – Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya.

“Nimepokea taarifa za kifo cha Mzee wetu Rais wa Awamu ya Tatu Ndg. Benjamin William Mkapa kwa masikitiko makubwa sana, salamu zangu za pole ziende kwa Watanzania wote, Mzee Mkapa alikuwa ni Baba, Mwalimu, Mlezi na wengi tulimtazama kama kioo.”- JokateMwegelo, Mkuu waWilaya ya Kisarawe.

“Nimeshtushwa sana na msiba wa Mzee Mkapa ambaye ukiachilia mbali uongozi wake ulioacha alama alikuwa pia kichocheo kwangu kupenda kuwatumikia wananchi kupitia siasa. Alikuwa mwepesi wa kusikiliza na kutoa ushauri muda wowote, na kipekee ni ucheshi wake muda wote.” –  Innocent Bashungwa.

” I mourn former President Benjamin Mkapa, a great friend of the Kenyan people, a pan-Africanist, a true believer in South-South Cooperation and a global statesman. Mkapa believed in Regional Integration and championed the revival of the East Africa Community. In his death, Africa has lost a giant. My thoughts and prayers are with his family, President John Pombe Magufuli and the people of the United Republic of Tanzania.”- Kiongozi wa Chama cha ODM Kenya, Raila Odinga.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger