Friday, 24 July 2020

Tanzia : RAIS MSTAAFU TANZANIA BENJAMIN MKAPA AFARIKI DUNIA

...
Mhe. Benjamin William Mkapa 

Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa (1995-2005) ambaye amefariki dunia usiku huu Julai 24,2020 wakati akiendelea kupatiwa matibabu Hospitali Jijini Dar es salaam.

"Kwa Masikitiko Makubwa tumepata msiba mkubwa, Mzee wetu Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu amefariki dunia, amefariki dunia katika hospitali Jijini Dar es salaam ambako alikuwa amelazwa,niwaombe Watanzania tulipokee hili,tumepata msiba mkubwa na tuendelee kumuombea Mzee wetu, Rais Mstaafu Benjamini Mkapa ambaye ametangulia mbele za haki,taarifa zingine zitaendelea kutolewa lakini Mzee Mkapa hatunaye tena", amesema Rais Magufuli katika taarifa yake kwa Taifa.

Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kuwa watulivu na wastahimilivu baada ya kupokea taarifa za kuondokewa na mpendwa wao, Mhe. Benjamin William Mkapa.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger