Thursday, 2 July 2020

TAKUKURU wilaya ya Kiteto yasaidia kurejesha Mahindi ya Kijiji.

...
Na John Walter-Manyara
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa  wilaya ya Kiteto mkoa wa  Manyara ,imefanikiwa kurejesha  mahindi gunia 45 katika kijiji cha Loltepes.

Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Kiteto Venance Sangawe amesema mahindi  hayo ni sehemu ya gunia 90 ambazo Takukuru  iliingilia kati kurejesha.

Sangawe amesema  diwani wa kata ya Sunya  aliemaliza muda wake, Musa Brayton na mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi  katika  kata hiyo Abdi  Puputo  walishindwa kutimiza masharti waliyokubaliana na kijiji  ya  kulipa mahindi hayo baada ya kulima shamba la kijiji  ekari tisini.

Ameongeza kuwa makubaliano kati ya watu hao na kijiji ilikuwa ni kulipa  gunia moja kwa kila ekari tangu mwaka 2017  hivyo kwa kushindwa kufanya hivyo Takukuru imeamua kuisaidia kijiji kurejesha mahindi hayo.

Akikabidhi mahindi hayo kwa mwenyekiti wa kijiji cha Loltepes Mkuu wa wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa,  amewataka viongozi wa kijiji na shule kuhakikisha mahindi hayo yanatumika kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wa shule za Loltepes na Loiborsoit zilizopo katika kijiji hicho.

Huo ni mwendelezo wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Manyara katika kurejesha na kukabidhi mali kwa wahusika halali ili  kuondoa  migogoro isiyokuwa ya lazima.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger