Wednesday 8 July 2020

Mfumuko wa Bei Mwezi Juni Waendelea kuwa Asilimia 3.2

...
Na   Mwandishi Wetu- MAELEZO
Mfumuko wa bei wa Taifa kwa  mwezi Juni 2020 umeendelea kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa mwezi  Mei, 2020. 
 
Akizungumza leo Julai 8, 2020 Jijini Dodoma,  Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bi. Ruth Minja amesema kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka unaoishia mwezi Juni umebaki kuwa sawa na iliyokuwepo kwa mwezi Mei. 
 
Akifafanua, Bi Minja amesema kuwa baadhi ya bidhaa za vyakula zilipungua bei kwa mwezi Juni 2020 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2019, baadhi ya bidhaa hizo ni pamoja unga wa mahindi kwa asilimia 1.6, matunda kwa asilimia 2.1, viazi mviringo asilimia 0.5 na mihogo asilimia 13.3. 
 
Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula amesema kuwa ziliongezeka bei kwa mwezi Juni, 2020 ikilinganishwa na bei za mwezi Juni 2019, bidhaa hizo ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.7, gesi ya kupikia kwa asilimia 7.8 , mkaa asilimia 11.2, samani asilimia 2.7 na vitabu vya shule kwa asilimia 1.5. 
 
Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2020 umepungua hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka unaoishia mwezi Mei, 2020. 
 
Kwa upande wa nchi ya Kenya Bi Minja amesema kuwa Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2020 umepungua hadi kufikia asilimia 4.59 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2020. Kwa upande wa Uganda, Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2020 umeongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 2.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2020. 
 
…Mwisho…


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger