Friday 10 July 2020

Majina Matatu Ya Wagombea Urais Zanzibar Kujadiliwa Leo

...
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi jana ilikutana jijini Dodoma na kufanyia kazi taarifa ya Kamati Kuu Maalum ya Visiwani Zanzibar, kupokea taarifa kutoka Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na taarifa ya Kamati ya Usalama wa Maadili ya CCM Taifa kuhusiana na makada wa Chama hicho wanaoomba kusimamishwa kuwania Urais Zanzibar.

Kamati Kuu imependekeza majina matatu ya wagombea wa urais Zanzibar kwa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).

Hata hivyo, majina hayo yatawekwa wazi leo Julai 10,2020 katika kikao cha NEC kwa wajumbe kwa ajili ya kupiga kura kumchagua mwanachama mmoja kwa nafasi hiyo.

Akitoa taarifa kuhusu kikao hicho leo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, alisema mapendekezo hayatakuwa wazi na kuwataka watu waendelee kuwa wanyenyekevu na watulivu.

“Ukifanya mchezo tu kesho(leo) tunafanya utaratibu mwingine, kwa hiyo kesho(leo) kwenye NEC tutawaambia wajumbe ni wakina nani kamati kuu imewapeleka NEC… wana CCM tuendelee kuwa watulivu,”alisema.

Aidha, Polepole alisema pamoja na mambo mengine kikao hicho kimetoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar kwa kuimarisha uchumi wa Taifa licha ya kupitia katika kipindi kigumu cha ugonjwa wa corona.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger