Wednesday 8 July 2020

FBI Yadai China ni Tishio kwa Marekani.....Ni Baada ya Kuituhumu Kuanza Kampeni Ya Kuwa Taifa Lenye Nguvu Kubwa Duniani

...
MKURUGENZI wa shirika la FBI nchini Marekani amesema kwamba vitendo vya upelelezi na wizi unaotekelezwa na serikali ya China ni tishio la muda mrefu kwa Marekani. Akizungumza katika Taasisi ya Hudson mjini Washington, Christopher Wray alielezea kampeni ya usumbufu iliyokithiri.

Alisema kwamba China imeanza kuwalenga raia wa China wanaoishi ughaibuni, ikiwashurutisha kurudi nyumbani na kwamba ilikuwa inajaribu kuingilia utafiti wa corona wa Marekani.

”China imeanza juhudi za kuhakikisha kuwa ndio taifa la pekee litakalokuwa na uwezo mkubwa zaidi duniani kwa hali na mali”, aliongezea.

Mkurugenzi wa FBI alielezea jinsi China inavyoingilia masuala ya Marekani kupitia kampeni kubwa ya upelelezi wa uchumi wa Marekani, wizi wa data na fedha kwa lengo la kushawishi sera za Marekani. Tumefikia wakati ambapo FBI sasa imeanza kufungua kitengo cha kukabiliana na visa vya Ujasusi wa China kila baada ya saa 10”, Wray alisema.

”Kati ya visa 5000 vya kukabiliana na ujasusi vinavyoendelea kote nchini , karibia nusu yake vinahusishwa na China.”

Mkurugenzi huyo wa shirika la ujasusi nchini Marekani alisema kwamba rais wa China Xi Jinping alianzisha mpango kwa jina ‘Fox Hunt’, unaowalenga raia wa China ughaibuni wanaoonekana kuwa tishio kwa serikali ya China.

”Tunazungumzia kuhusu wapinzani wa kisiasa, watoro na wakosoaji walio na lengo la kufichua ukiukaji wa haki za kibinadamu unaotekelezwa na China”, alisema.

”Serikali ya China inataka kuwalazimisha kurudi nyumbani na mbinu zinazotumiwa na china kufanikisha mpango huo inashtua.”

Aliendelea: inaposhindwa kumpata mtu inayemtafuta, serikali ya China hutuma mjumbe kutembelea familia ya mtu huyo nchini Marekani. Ujumbe unaotolewa ni : Rudi China haraka ama jiue.

Credit: BBC


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger