Wednesday, 18 December 2019

Viongozi 6 wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Wasimamishwa Masomo kwa Muda Usiojulikana

...
Viongozi sita wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – UDSM, (DARUSO), akiwemo Rais wao, Hamis Musa Hamis wamesimamishwa masomo kwa muda usiyojulikana kufuatia madai ya mikopo iliyochelewesha na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa wanafunzi wa chuo hicho.

Juzi, DARUSO ilitoa saa 72 kwa bodi ya mikopo ( HESLB) kutekeleza maagizo 4 likiwemo kuwawekea fedha za kujikimu wanafunzi ambao hawajapewa tangu Chuo kilipofunguliwa na Kama agizo hilo halitatekelezwa watakusanyika nje ya Ofisi hizo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, jana Jumanne, Desemba 17, 2019, aliupa uongozi wa chuo hicho saa 24 kuwachukulia hatua wanafunzi waliotoa tamko hilo na kusema  lilitolewa kinyume cha utaratibu na ni utovu wa nidhamu.

Viongozi wengine waliosimamishwa masomo kwa muda usiojulikana na uongozi wa chuo hicho ni Waziri wa Mikopo, Waziri wa Habari, Mwenyekiti wa Bunge na Jaji wa Mhimili isipokuwa Makamu wa Rais na inaelezwa kwamba wamepewa muda hasi saa 6 mchana wa leo wasionekane chuoni hapo.



Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger