Thursday, 19 December 2019

Tanzania mbioni Kupata Cheti cha Nchi zenye Vigezo vya Kudhibiti Rasilimali Kutotumika kuendeleza Machafuko

...
Na Nuru Mwasampeta, DSM
Imeelezwa kwamba ndani ya Miaka miwili ijayo Tanzania
inatarajiwa  kupata Cheti Maalumu kitakachoitambulisha kuwa ni nchi iliyokidhi Vigezo vya nchi! zinazotumia rasilimali zinazopatikana nchini kuepusha machafuko kwa nchi wanachama.

Cheti hicho kitaiwezesha nchi kutathmini na kuruhusu Madini ya Bati (tin), dhahabu kuuzwa nje ya nchi yakiwa yametambuliwa na kuthaminiwa.

Hayo yamebainishwa wakati wa kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo  tarehe 18 Desemba,  2019 jijini Dar es Salaam,  kilicholenga  kupokea ripoti juu ya tathmini iliyofanywa kwa lengo la kujiridhisha endapo Tanzania inakidhi vigezo vya kupewa cheti cha nchi wanachama zilizokidhi matakwa ya kutunza rasilimali za nchi ili zisitumike katika kusababisha na
kuendeleza machafuko kwa nchi wananchama.

Ripoti hiyo iliwasilishwa na wajumbe kutoka kwa viongozi wa sekretariati ya Jumuiya ya Nchi zilizo kwenye Maziwa Makuu wenye nchi wanachama 12 ulioundwa kwa lengo la kulinda rasilimali zinazopatikana katika nchi zao ili zisitumike katika kusababisha na kuendeleza machafuko katika nchi wanachama.

Akizungumza katika kikao hicho,  Naibu Waziri Stanslaus Nyongo alisema anatarajia nchi za Rwanda, Uganda na Kongo zitafanya kazi kwa pamoja ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho.

Nyongo alisema kwa tathmini iliyofanywa na Sekretarieri wakati ilipokuwa  nchini, imewaonesha wazi namna Serikali ya Tanzania inavyoendesha biashara ya Madini na kuomba taarifa hiyo itumike kuharakisha mchakato wa nchi kupewa cheti hicho.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila aliwataka wajumbe kukamilisha kazi hiyo kabla ya Mwaka kuisha ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho.

Akizungumza mchakato huo, Gerard Nayuburundi mmoja Kati ya wajumbe wakiokuwa wakifanya tathmini nchini kutoka Burundi alisema wako tayari kuandaa kikao ili kuwasilisha na kujadili matokeo waliyoyapata ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho.

Aliongeza kuwa, wamejiridhisha na namna Tanzania inavyolinda na kuwasaidia wawekezaji ili kile  walichowekeza nchini kiwe na matokeo chanya.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger