Monday 9 December 2019

KAULI YA MBOWE LIVE MBELE YA RAIS MAGUFULI KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA UHURU

...

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowea,amehudhuria maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru katika Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni hakuvaa sare maalum za chama wala kombati ambazo zinatumiwa kama vazi maalum chama chao lakini amepigilia suti nyeusi, shati jeupe na tai.


Taarifa ya kushiriki kwenye maadhimisho kwa Mwenyekiti wa CHADEMA ilitolewa juzi na Kamati Kuu ya chama hicho kwa kumuagiza Mwenyekiti wake kwenda kukiwakilisha chama hicho kwenye Sherehe hizo za Uhuru. Hii ni mara ya kwanza kwa CHADEMA kushiriki kwenye maadhimisho ya Uhuru tangu mwaka 2015.

Akizungumza baada ya kupewa nafasi na rais Magufuli leo,Mhe. Mbowe ametoa kauli zifuatazo

"Nimekujua kuhudhuria maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru kama Uthibitisho wa Ulazima wa uwepo wa maridhiano,uwepo upendo,uwepo mshikamano katika taifa letu.

Nawapongeza sana Watanzania kwa siku ya leo na namuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama taifa la watu wanaopendana,tuvumiliane,tukosoane turuhusu demokrasia tujenge taifa lenye upendo na mshikamano 

Na Mhe. Rais kwa nafasi ya pekee tuna nafasi ya kuweka historia ya maridhiano katika taifa kwani kuna wengine wanalalamika,wengine wanaumia,Mhe. Rais tumia nafasi ukaliweke taifa katika hali ya utengamano" - Mbowe

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger