Halmashauri ya jiji la Dodoma imeshaanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli alilotoa Nov.25 mwaka huu la kulipa fidia kwa wananchi 1526 wanaopisha eneo la Jeshi la Wananchi Jijini Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Nov.30,2019 jijini Dodoma mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema kiasi kinachotakiwa kulipwa kwa wananchi hao ni Tsh.Bil.3.399 na ukubwa wa eneo zima ni ekari elfu tano na eneo linalopaswa kulipwa fidia ni ekari elfu 3 mia 4 na 31 na kinachotakiwa kwa wanufaika ni kufungua akaunti za benki huku uhakiki ukiendelea.
Aidha,Bw.Kunambi amesema ofisi ya mkurugenzi jiji la Dodoma imeshaanza kuwasaidia wananchi kusaidia kufungua akaunti za benki na kuanzia wiki ijayo wananchi wataanza kulipwa fedha zao.
Ikumbukwe kuwa Nov.25,2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli wakati akiweka jiwe la Msingi eneo la Jeshi la Ulinzi alitoa agizo kwa halmashauri ya jiji la Dodoma kuwalipa fidia wananchi 1526 wanaopisha mradi wa eneo la jeshi la Ulinzi.
0 comments:
Post a Comment