Sunday, 1 December 2019

Chama cha Walimu Tanzania Kujenga Kiwanda Cha Mikate Lishe Simiyu

...
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kinatarajia kujenga kiwanda cha mikate lishe kupitia kampuni yao inayosimamia Maendeleo ya Walimu ya biashara (TDCL), katika eneo la Ng’hami wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Akimkabidhi  Katibu wa Chama cha Walimu Nchini, Mwl. Deus Seif hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2), Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe amesema wilaya imetoa kiwanja hicho bure, ikiwa ni moja ya njia ya kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda ambapo kumhakikishia upatikanaji wa malighafi ya kiwanda hicho (viazi lishe)

“Tumejipanga kuzalisha viazi lishe vya kutosha vitavyotumika kama malighafi ya kiwanda hiki na tayari wakulima wamepewa mbegu za viazi hivyo, niendelee kuwakaribisha CWT wilayani Maswa, kama kuna uwekezaji mwingine mnahitaji kufanya karibuni, hata kama ni tawi la benki yenu ile ya walimu tunawakaribisha sana,” alisema Dkt. Shekalaghe.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Simiyu amesema kukamilika kwa kiwanda hicho kutasaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa lishe ambalo limekuwa ni changamoto kwa  Mkoa wa Simiyu.

Aidha, Mtaka amesisitiza Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashautri na wataalam wa kilimo wahakikishe mbegu ya viazi lishe inapatikana kwa wingi ili wananchi wanapohitaji waipate

 Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Taifa, Mwl. Deus Seif amesema chama hicho kinaunga mkono sera ya Tanzania ya Viwanda huku akibainisha kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utaenda haraka kwa kuwa tayari kampuni ya CWT inayosimamia miradi imeshaanza kulifanyia kazi suala hilo.

Ameongeza kuwa pamoja na kujenga kiwanda cha mikate lishe, chama hicho pia kinatarajia kuchukua uwakala katika Kiwanda cha Chaki cha Maswa ili kusambaza chaki zinazozalishwa wilayani humo katika shule zote nchini.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger