Saturday 7 December 2019

Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) yatekeleza agizo la Naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe.

...
SALVATORY NTANDU
Siku chache baada ya Naibu waziri wa kilimo, Husein Bashe kuiagiza bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kugawa mbegu za pamba kwa mkopo kwa pamba kwa wakulima wote nchini, hatimaye agizo hilo limeanza kutekelezwa katika wilaya ya mbogwe mkoani Geita.

Mahitaji ya mbegu kwa wilaya ya Mbogwe  ni tani 200 na mbegu ziliyopokelewa ni tani 126.5 kwa AMCOS ambazo zitakopeshwa kwa vyama vya msingi (AMCOS) 35 kwaajili ya msimu wa mwaka 2020.

Akipokea mbegu hizo kwa niaba ya wakulima katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita jana, mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Matha Mkupas alisema mbegu hizo zimeletwa kwa wakati muafaka na zitasaidia kuongeza uzalishaji  kwa msimu huu.

“Wakulima walikuwa wamekata tamaa ya kulima zao la pamba kutokana kuuziwa mbegu na kampuni za ununuzi wa pamba lakini baada ya serikali kuagiza zikopeshwe kwa wakulima mwitikio wa ukopaji umekuwa ni mkubwa zaidi”alisema Mkupas.

Mkupas aliwataka viongozi wa vyama vya msingi kuhakikisha mbegu hizo zinawafikia wakulima wote kwa haraka ili kwenda sambamba na msimu wa kilimo ambao umeshaanza sambamba na kudhibiti wakulima kulisha mifugo mbegu hizo kwa msimu uliopita.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Pamba wa wilaya ya Mbogwe, Atupele James alisema morali ya wakulima wa pamba kulima zao hilo kwa mwaka huu ilikuwa chini kutokana na kulazimika kununua mbegu kwa sababu baadhi yao bado hawajalipwa fedha.

“Wapo wakulima ambao mpaka sasa bado hawajalipwa fedha zao baada ya kuuza pamba katika msimu uliopita na kampuni zilizonunua mazao yao na kusababisha kushindwa kuendelea na kilimo ila kupatikana kwa mbegu hizi zitawahamasisha kulima”alisema James.

Simon Mtagwa ni mmoja wa wakulima wa pamba katika wilaya ya Mbogwe alisema kucheleweshwa kwa malipo yao baada ya kuuza pamba kumesababisha kushindwa kufanya maandalizi ya msimu mpya wa kilimo kutokana na kushindwa kunua mbegu.

Novemba 29 mwaka huu Naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe kwenye kikao cha wadao wa pamba  aliiagiza wakulima  nchini wakopeshwe mbegu ili kwenda sambamba na msimu wa kilimo wa mwaka 2020.

Mwisho.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger