Monday 2 December 2019

Afya Moja Kutumika Kuimarisha Afya Ya Binadamu Kwa Magonjwa Ya Sokwe

...
Afya Moja ambayo ni dhana inayojumuisha sekta ya Afya ya binadamu, Mifugo, Wanyamapori na Mazingira katika kujiandaa, kubaini, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri sekta hizo, hivi karibuni umezinduliwa  Mradi wa kimkakati wa kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya  binadamu na wanyama hususan Sokwe,  ujulikanao kama Bush to Base, mradi huo utatekelezwa mkoani Kigoma katika Halmashauri ya wilaya ya Uvinza kwa 18 vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa  milima ya Mahale.

 Lengo la mradi huo unaosimamiwa na kuratibiwa na  shirika lisilo la kiserikali la Bush-To-Base (B2B),  ni  kuongeza kasi ya ushirikiano kati ya Wizara za Kisekta na kuongeza uelewa wa dhana ya Afya Moja miongoni mwa wataalamu na wadau wengine wa sekta za afya ya wanyama, binadamu, kilimo na mazingira ili kuwa na mikakati shirikishi ya uchunguzi, utambuzi na udhibiti wa magonjwa.

Akiongea wakati wa kuzindua Mradi huo mkoani Kigoma, Katibu Tawala wa mkoa wa Kigoma, Rashid Mchatta alifafanua kuwa Mradi huo ni muhimu katika kuimarisha usalama wa afya ya wananchi wa mkoa wa Kigoma na taifa kwa ujumla kwa kuwa  Kume kuwa na mwingiliano mkubwa kati ya  watu na wanyama katika mazingira yao hivyo dhana dhana ya afya moja haina budi kutumika kwakuwa ni utaratibu ulioratibiwa kwa kushirikisha sekta zote za Afya.

“Kwa kuwa tafiti zinabainisha kuwa vimelea vingi vinavyo sabababisha magonjwa kwa binadamu zaidi ya 60% vinatoka  kwa wanyama pori na mifugo na maambukizi yanatokea pale binadamu anapoingilia maskani ya wanyama hao bila tahadhari, hatuna budi kuongeza ushirikiano na mawasilaino katika nyanja za afya ya binadamu, wanyama na mazingira ili kuwa na ufanisi katika kudhibiti magonjwa yanayoambukiza” alisistiza Mchatta.

Kwa upande wake Rais wa  shirika lisilo la kiserikali la Bush-To-Base (B2B), Dkt Teresa Sylvin amefafanua kuwa  mradi huo unajikita katika matokeo ya tafiti za kisayansi kuhusu afya ya Sokwe katika Hifadhi ya Taifa milima ya Mahale ambazo amezifanya kwa zaidi ya miaka 25.

“Kimsingi huu mradi unakusudia kutumia dhana ya afya moja kwa kutumia matokeo ya tafiti ili kuweza kuzishirikisha sekta za afya ya wanyama, binadamu, kilimo na mazingira ili kuwa na mikakati shirikishi ya uchunguzi, utambuzi na udhibiti wa magonjwa yatokanayo na Sokwe kwenda kwa binadamu. Lakini tunalenga kuishirikisha jamii ambayo inaishi katika mazingira ya mradi huu, naamini kwa kutumia afya moja tutafanikiwa ” alisema Dkt.Teresa

Mradi huo utakaotekelezwa kwa miaka mitatu mkoani Kigoma utakuwa ukifanya kazi za uratibu kwa kushirikiana na Ofisi yaWaziri Mkuu, Kupitia Dawati la Afya moja, tayari umepata ufadhili kutoka serikali ya Marekani chini ya Mfuko wa Sayansi na mwingine unajihusisha na Samaki na Wanyamapori.

MWISHO.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger